kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,416
- 7,199
Kila nikimsikiliza rais Samia kuhusu mtazamo wake kushirikisha sekta binsfsi kutoa huduma kwa umma nakua na mashaka.
Sekta binafsi ni watafutaji wa faida. Dhana ya kusema serikali ishirikiane na sekta binafsi kutoa huduma kama afya elimu etc lazima itafsiriwe vyema isiweze kutumika vibaya ambapo vigogo Serikali wanaweza kushirikiana na watu binafsi kufanya ubadhirifu na wizi wa fedha za umma huku wananchi wakinyonywa na kupata huduma duni au watu binafsi wakitoa huduma hewa huku fedha ya serikali inaliwa.
Kinachotakiwa ni kampuni binafsi zenye uwezo kupewa fursa kutoa huduma ziada huku serikali ikifanya udhibiti kuona kuna bei wananchi wanazimudu kutokana na sekta binafsi kuendeshwa kwa tija.
Huko nyuma kuna mifano mingi ya ubabaishaji wa sekta binafsi kwa kufanya uhuni. Tunakumbuka richmond, iptl na ziko kampuni binafsi kibao za kujenga miradi ya maji iliyojenga miradi feki bila hata kutoa maji huku wakilipwa mabilioni ya fedha.
Kinachotakiwa ni serikali kufanya kazi kwa tija na kutimiza wajibu wake na sio kujidai kushirikiana na sekta binafsi ili kuwapa fursa wapigaji kuibia umma.
Tunataka sekta binafsi yenye tija uwezo wa mtaji na ujuzi kushirikiana na serikali sio wababaishaji na wahuni.