Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma IFUTWE/IVUNJWE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma IFUTWE/IVUNJWE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mussa Loth, Apr 27, 2012.

 1. M

  Mussa Loth Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 132 imeweka msingi wa kuundwa kwa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kwamba Ibara ya 70 kuwasilisha taarifa ya mali na kifungu cha 71 kinataja sababu za kukoma kuwa mbunge kutokana na kukiuka masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa umma; hivyo sekretariati inapaswa kupanua wigo wa kutimiza majukumu husika ya kikatiba.


  Kwa hiyo, pamoja na kufanya zoezi la kawaida la kuhakiki fomu za tamko la mali na madeni kwa viongozi wa umma; kwa kuwa sekretariati imetangaza kuwa itafanya kazi kwa uwazi na kwa kuzingatia sheria basi iweke kipaumbele katika kutumia mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa sheria husika vifungu 18(4) na 22 (4) kufanya mchakato muhimu zaidi wa kufanya uchunguzi wa tuhuma juu ya ufisadi uliofanywa na unaoendelea kufanywa na viongozi wa umma ambao wametajwa kwa nyakati mbalimbali kwenye mikutano na katika vyombo vya habari.


  Izingatiwe kuwa pamoja na uchunguzi wa awali unaoweza kufanywa na Sekretariati kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 kifungu 22(2); uchunguzi kamili unafanywa na baraza ambalo kwa mujibu wa kifungu 26(5) linapaswa kufanya uchunguzi wake hadharani ili umma uweze kufahamu.

  Kushindwa kutoa tamko lolote pale ambapo mbunge/ wabunge wanapoonekana na kumiliki mali ambazo uhalali wake haueleweki, na hivi karibuni mbunge mmoja imefahamika amenunua nyumba yenye thamani kubwa, pamoja na mali nyingine, je sekretariati ya maadili ya viongozi wa umma kuna haja ya kuwepo,na nini msaada wake kwa umma kama kuna haja ya kuwepo.
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nakuelewa sana had the same idea ... lakini nikaingia kwenye big dilemma... Hivi Tanzania ya sasa utamweka nani baada ya kuwatimua hao waliopo?
   
 3. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,447
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 180
  Nakuunga mkono asilimia mia moja, niliwahi kulisema hili hapa jamvini na toka nimelisema nimelichunguza kujua kwa nini hii tume haifanyi kazi. kiongozi wake anachaguliwa na kiranja mkuu ambaye kwa pamoja kama ilivyo kwa maige wanafanya kolabo ya nguvu kucheza madili yao, hii sekretarieti ni mlinzi wa mafisadi na ndio mwavuli wao mkuu. Nasema hivi kwa kuwa siamini kama ni kweli kabisa katika uongozi wa jk hakuna kiongozi hata mmoja ambaye hajakikuka au kwenda kinyume na matakwa ya hii sekretarieti. Hatua zipi zimechukukliwa? hakuna! Chezea Tanzania wewe!!!! Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,075
  Trophy Points: 280
  Haya Mh. Jaji (Rtd.) Salome Kaganda unalo. Sijui kama utaweza huu mziki manake wengi mnachukulia hivi vyeo kama ulaji tu badala ya uwajibikaji.
   
 5. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ...lakini inapunguza tatizo sugu la ajira nchini.
   
 6. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Inapunguzeje tatizo la ajira?
   
 7. m

  mchukiaufisadi JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 538
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kwa kuwepo kwake watu wanapata ajira eg drivers, secretaries, Dr Kaganda na wasaidizi wake.

  Hii tume ni bure kabisa.

  Mimi nalia na PPF, Wakurugenzi wake ni mabilionea, wana majumba makubwa kuliko ya akina Maige lakini walichokitaja kwenye tume ni chini ya 10% ya hali halisi. Tume ilidokezwa lakini hawakufanya chochote.

  IFUTWE KABISA maana ni mzigo kwa taifa.
   
 8. B

  BULOLE BUKOMBE JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Haiwezi kufutwa kwa sababu hata aliyewateua hana maadili ya uongozi kwa hiyo kizazi cha nyoka nacho ni nyoka upuuzi mtupu tutaonana 2015 kama Mungu akitujalia uhai.
   
 9. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,714
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Sheriai iliyounda chombo hiki ina mapungufumakubwa, waliounda hawakuwa na dhamira ya dhat, watendaji na watumishi wake wanaweza wakawa na dhamira ya dhati lakini wakakwamishwa makusud na ndicho kinachofanyika ikiwa pamoja na kutopewa bajet ya kutosha. sheria ilitakiwa ifanyiwe mabadiliko lakin mpaka leo inapigwa danadana 2, utashi wa kisiasa haupo.
   
 10. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Kwa kweli hii tume ni sehemu ya tatizo, nadhani CAG pekee anatosha maana kazi yake japo haitaji madudu yote lakini imetufungua macho tulio wengi. Nadhani hii tume ingetafutiwa kazi nyingine ya kufanya, labda ikawa tume ya kusimamia maboresho ya UMISHUMITA NA UMISETA ili kuibua vipaji vya watanzania katika fani ya michezo.
   
Loading...