Sekretarieti ya CCM yazuru kaburi la Hayati Dkt. Magufuli wilayani Chato

Na Mwandishi Wetu
Kutoka Chato.

Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuyaenzi mema yote yaliyoanzishwa, kusimamiwa na kutekelezwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tano Hayati John Pombe Magufuli...
Keshalala huyo bado zamu yetu
 
Na Mwandishi Wetu
Kutoka Chato.

Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuyaenzi mema yote yaliyoanzishwa, kusimamiwa na kutekelezwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Tano Hayati John Pombe Magufuli.

CCM inaendelea kusisitiza kuwa Jina la Dkt John Pombe Magufuli litabaki kwenye Kumbukumbu, mipango na fikra za Chama kwa kufuata mazuri yote ambayo ameyaanzisha wakati wa uhai wake ambayo yamekuwa alama za utumishi wake kwa Taifa.

Leo, Jumatatu, Mei 17, 2021 miezi miwili tokea kufariki kwa Hayati John Pombe Joseph Magufuli wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Tanzania bara Ndugu Christina Mdeme wamefika kuzuru na kufanya sala ya kumuombea, kaburini, Wilayani Chato Mkoa wa Geita.

Chama Cha Mapinduzi kimeridhishwa na hatua inayoendelea ya kuboresha na kutunza eneo ambalo Hayati John Pombe Magufuli amezikwa na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuthamini, kujali na kuenzi mchango wa Hayati John Pombe Magufuli.

"Chama kinaipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa maono na jitihada kubwa za kuitunza familia ya Mpendwa wetu Hayati John Pombe Magufuli lakini pia kuhakikisha eneo alilopumzishwa mpendwa wetu linatunzwa na kuwekwa katika mazingira bora. Huyu ni kiongozi wetu aliyetufanyia mema katika Taifa hivyo eneo hili ni muhimu sana kwani anahitaji sala na maombi yetu hivyo kila mtanzania na wageni mbalimbali hufika hapa kumtakia shifaa kwa Mwenyezimungu" Christina Mdeme.

Chama Cha Mapinduzi kimeridhishwa na hatua nzuri ya ujenzi unaoendelea ambapo kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Charles Kabeho, ujenzi huo ulianza tarehe 6 April 2021 na unatarajiwa kukamilika baada ya mwezi mmoja chini ya usimamizi wa Suma JKT.

Wakati ujenzi huo ukiendelea eneo la kaburi limezungushiwa uzio wa mabati ili kulitunza lisichafuke na kuepusha vifaa vya ujenzi vyenye ncha kali kusambaa na kuleta madhara kwa watu kwa vile pamoja na ujenzi kuendelea bado wananchi mbali mbali hufika kwa ajili ya kufanya maombi kwa Hayati John Pombe Magufuli hivyo Chama Cha Mapinduzi kimewataka watanzania kupuuza uvumi wowote ambao hauna nia njema kwa Mpendwa wetu Hayati John Pombe Magufuli na familia yake.

Bwana ametoa na Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe.

Apumzike kwa Amani Hayati John Pombe Magufuli


Imetolewa na;
Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa,
Itikadi na Uenezi
17 Mei 2021


Sawa ila ilo banda la mama ntilie vipi tena, Si muende hata pale machame kwa Mengi mkaone vile wapendwa walikufa wanavyo thaminiwa.

Sukuma Gang wanapambana kwa mihemko kumbe hata uwezo wa kumsitiri mpendwa wao hawawezi, dah eti jeshi limemjengea, Mwenda zake pale chato kuna ndugu zake amewapa miradi mikubwa sana wameshindwa hata kutoa fadhila ya kumjengea pumbavu sana
 
Back
Top Bottom