Sekretarieti ya CCM yagonga hodi kwa Dkt. Shein Zanzibar

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Cde Daniel Chongolo akiongozana na wajumbe wa Sekretariet ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wamewasili Zanzibar Jumapili 4 Julai 2021 kwa ziara ya kikazi ya Siku mbili.

Mara baada ya mapokezi mafupi katika bandari ya Malindi Cde Chongolo na ujumbe wake walifika kusalimiana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein katika makaazi yake Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Wakati wa mchana Cde Chongolo atahudhuria mapokezi rasmi katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kiswandui kisha kuzungumza na wanachama, wapenzi na wakerekwete wa CCM mikoa mitatu ya Unguja.

#KaziInaendelea#
#ChamaImara#
IMG-20210704-WA0044.jpeg
IMG-20210704-WA0043.jpeg
IMG-20210704-WA0042.jpeg
IMG-20210704-WA0041.jpeg
 
Naona kama huyo katibu mwenezi wake anaonekana mjuaji flani sijui kama wanafanya kazi kwenye mazingira murua.
 
Back
Top Bottom