Sekretarieti ya CCM mnafanya mikutano ya hadhara kama wabunge wa wapi?

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
526
583
“Kwa sasa tunaruhusu mikutano ya ndani, isipokuwa kwa wabunge wenye majimbo” Samia Suluhu Hassan, Madam President.

Sasa nyie Secretariat ya CCM mmeenda Zanzibar mkafanya mkutano huko mpaka watoto wadogo wakaanza vijembe kwa kina Mbowe.

Sasa mko Mikoa ya Songwe na Rukwa, huyu katibu mwenezi naona amefanya mkutano wa hadhara kama mbunge wa Wapi?

Adjustments.jpg
 
Mbona lipo wazi kwenye picha, hicho ni kikao cha balozi wa shina. Ambaye kimsingi anapaswa kuitisha kikao cha wananchi kwenye shina lake.

CHADEMA nao wasingesusia uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 wangekuwa na uwezo wa kuongea na wananchi kupitia vikao vya mitaa. Ila walivyo walafi wakazuia wenyeviti kugombea nchi nzima.

Ki ukweli wengi wao walikasirika sana. Maana kuna maeneo wenyeviti wa CCM walikuwa hawakubaliki.Lakini kwenye ubunge Mbowe and co. hawakususia. Ndio maana wananchi wakawaadhibu kwenye sanduku la kura 2020.
 
Mleta mada nadhani hukusoma hayo maelezo kwenye picha uliyotuletea

Kama ungesoma usingeleta hii mada.

Umedhihirisha kuwa watanzania wengi hatuna utaratibu wa kusoma.
 
CCM ndio wanao itawala nchi kwahiyo wao wana haki ya kutembelea kila kona ya nchi kuangalia utekelezaji wa Ilani
 
Mbona lipo wazi kwenye picha, hicho ni kikao cha balozi wa shina. Ambaye kimsingi anapaswa kuitisha kikao cha wananchi kwenye shina lake.

CHADEMA nao wasingesusia uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 wangekuwa na uwezo wa kuongea na wananchi kupitia vikao vya mitaa. Ila walivyo walafi wakazuia wenyeviti kugombea nchi nzima.

Ki ukweli wengi wao walikasirika sana. Maana kuna maeneo wenyeviti wa CCM walikuwa hawakubaliki.Lakini kwenye ubunge Mbowe and co. hawakususia. Ndio maana wananchi wakawaadhibu kwenye sanduku la kura 2020.
Hili ulichoandika hapa ni muendelezo wa mawazo ya kidikteta mliyonayo, hilo shina linaundwa na kina nani? ina maana hao wananchi kwenye hilo shina wote ni CCM? siamini.

Wapinzani nao wapo hapo, na wao wana haki ya kuandaa mikutano yao ili kuwaonesha wananchi wa shina husika mipango yao, ikiwa ni pamoja na kutafuta wanachama wapya.

Sasa mnavyowafungia wapinzani ndani mnataka hizo shughuli zao wazifanye vipi? haiwezekani nyie muendelee kueneza sera zenu wakati wengine mnawalazimisha kujifungia ndani, huu ni ushamba kwa taifa linalojiita la kidemokrasia.
 
Nampongeza Katibu Mkuu wa CCM na Chama Chake, kwa kupuza amri isiyohalali ya zuio la Mikutano ya hadhara, Natoa wito kwa Vyama vingine Vya siasa kuwaunga Mkono CCM kusimamia Sheria ya Vyama vya siasa na kuendelea na mikutano ya hadhara kwa Mujibu wa Sheria.
 
Acha unafiki wewe na unaotamani waigwe,dawa hapa ni katiba mpya tu,mwingine wote utakuwa ni uhuni tu.
 
Katazo fake kabisa
 
Acha unafiki wewe na unaotamani waigwe,dawa hapa ni katiba mpya tu,mwingine wote utakuwa ni uhuni tu.
Hiyo katiba mpya ikisema hakuna kuzurura na mikutano yenu mpaka wakati wa uchaguzi ndo mzurule hapo utasemaje?
 
Ni kweli ni muda muafaka kwa vyama vingine navyo kuanza mikutano ya hadhara.
 
Hiyo katiba mpya ikisema hakuna kuzurura na mikutano yenu mpaka wakati wa uchaguzi ndo mzurule hapo utasemaje?
Tunayo draft tayari ambayo inawafanya wanaonufaika na hii watokwe jasho Hadi la kucha,na ndio sababu ya kukataa hata kusikia habari ya katiba mpya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom