Sekretarieti ya ajira mambo yatakuwa safiiiiiiiiiiiiiiii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sekretarieti ya ajira mambo yatakuwa safiiiiiiiiiiiiiiii

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by kibakwe, Apr 25, 2012.

 1. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [TABLE="align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"] [TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"][/TD]
  [/TR]
  [TR]

  [TD="class: Marquee"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"][/TD]
  [/TR]
  [TR]

  [TD="class: Marquee"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  SEKRETARIETI ya Ajira imesema kwamba inaamini katika miaka 10 ijayo, utumishi wa umma nchini utakuwa safi kwa sababu ya kudhibiti ubora wa watumishi wanaoajiriwa serikalini.

  Aidha, tangu ianzishwe takriban miaka mitatu sasa, imekwisha tangaza nafasi za kazi 4,285 kwa waajiri 156 na hadi kufikia robo ya mwaka wa fedha 2011/12, imeendesha usaili wa maofisa watendaji wakuu 99 na wataalamu 662.

  Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira, Bakari Mahiza alisema suala la kuhakikisha utumishi wa umma unakuwa na watumishi wazuri ni jukumu la pamoja la wadau mbalimbali wa Serikali, lakini kwa upande wao, jukumu kubwa ni kuboresha mchakato wa ajira ili kupata watumishi wanaokidhi sifa na vigezo.

  Mahiza alisema mbali ya kutangaza nafasi za kazi 4,285 kutoka kwa waajiri 156, pia Sekretarieti ya Ajira imeanza kutumia kanzidata yake kujaza nafasi mbalimbali katika utumishi wa umma; hivyo kuongeza ufanisi na kupunguza gharama kwa Serikali. Kanzidata hiyo kwa sasa ina waombaji 200.

  Aidha, alisema tangu kuanzishwa kwake, wamekuwa wakishirikiana na wataalamu maalumu kwa ajili ya kufanya usaili kulingana na mahitaji, na tangu Machi, 2010, wameshaunda majopo 215.

  Alisema katika majopo hayo 215, majopo 30 yalihusisha usaili wa nafasi za maofisa watendaji wakuu, wakurugenzi/wakuu wa Idara na Wakala wa Serikali na wakuu wa vitengo ambapo nafasi 17 za maofisa watendaji wakuu, 21 za wakurugenzi/wakuu wa Idara na nafasi mbili za wakuu wa vitengo zilishindanishwa.

  Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti hiyo, Xavier Daudi, wamefanikisha upatikanaji wa watendaji wakuu wa taasisi za Wakala wa Barabara (Tanroads), Taasisi ya Uhasibu Arusha, Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Chuo cha Ustawi wa Jamii.

  Aidha, Mahiza aliyataja baadhi ya mafanikio ya kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira kuwa ni wataalamu 514 na watumishi walio katika masharti ya kawaida kuajiriwa katika mwaka 2009/10 na kwa mwaka 2010/11 ni wataalamu 1,921 na watumishi walio katika masharti ya kawaida 206 waliajiriwa.

  Kuhusu changamoto, ilizitaja kuwa ni upungufu wa miundo ya utumishi wa umma ambayo haikidhi mahitaji ya sasa; ufinyu wa bajeti na kutofahamika vya kutosha na wadau.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...