Sekretarieti ya Ajira ichunguzwe, kuna dalili za rushwa!

Pambafu! sasa hapo kwenye nyekundu umeandika nini? kama tu kuandika shida, utaweza kuandika CV na cover letter yenye ushindani kweli!

We keali unaukalia, Hiyo inaweza kusema sijui kuandika. Acha useeee
 
wana JF habari zenu??
Hivi karibuni nimeona serikali imekuja na mfumo mpya
wa kuajiri watumishi wa umma kupitia Secretarieti ya Ajira utumishi
wa umma, Je nini ajenda nyuma ya pazia?
Je watoto wa wakulima wasio kuwa na godFathers wataweza tena kupenya?
najikuta najiuliza haya maswali kutokana na uzoefu wa hapo nyuma!
mathalani tumekuwa tukiona matangazo ya masoma ya juu nchi za
nje (China) kupitia wizara ya Elimu na hata mamlaka nyingine za
serikali cha ajabu nafasi zimekuwa zikibanwa sana na pengine watu kwenda
wasiokuwa na sifa, au kutokwenda kabisa kwa sababu wahusika wamekosa
ndugu zao wa kuwapeleka!, waalimu wa Kiswahili waliwahi kuhitajika
katika baadhi ya nchi za kiafrika, lakini nafasi zilibanwa, matokeo yake
wakenya wakazinyakua fasta! tumeona scholashipu za BTC zilivyoleta
mkanganyiko mpaka zikasimama mwaka jana!

Hofu yangu: huu mfumo mpya usijeukawa unatumika kuwaneemesha
watoto wa "Walala Hai" na kugandamiza haki ya watoto wa "Walala Hoi"!

nawakilisha!!!
 
wana JF habari zenu??
Hivi karibuni nimeona serikali imekuja na mfumo mpya
wa kuajiri watumishi wa umma kupitia Secretarieti ya Ajira utumishi
wa umma, Je nini ajenda nyuma ya pazia?
Je watoto wa wakulima wasio kuwa na godFathers wataweza tena kupenya?
najikuta najiuliza haya maswali kutokana na uzoefu wa hapo nyuma!
mathalani tumekuwa tukiona matangazo ya masoma ya juu nchi za
nje (China) kupitia wizara ya Elimu na hata mamlaka nyingine za
serikali cha ajabu nafasi zimekuwa zikibanwa sana na pengine watu kwenda
wasiokuwa na sifa, au kutokwenda kabisa kwa sababu wahusika wamekosa
ndugu zao wa kuwapeleka!, waalimu wa Kiswahili waliwahi kuhitajika
katika baadhi ya nchi za kiafrika, lakini nafasi zilibanwa, matokeo yake
wakenya wakazinyakua fasta! tumeona scholashipu za BTC zilivyoleta
mkanganyiko mpaka zikasimama mwaka jana!

Hofu yangu: huu mfumo mpya usijeukawa unatumika kuwaneemesha
watoto wa "Walala Hai" na kugandamiza haki ya watoto wa "Walala Hoi"!

nawakilisha!!!

Nakuhunga mkono katika hilo mkuu, watu hawa wa UTUMISHI wamekwamisha sana nchi yetu kwa kufanya mambo ya ndio sivyo - kwa bahati mbaya nasikitika kusema naona hawajabadirika chochote, wapo radhi kupoteza nafasi za Watanzania kusoma nje simply wakiona walio omba nafasi hizo kama hakuna ndugu,rafiki zao basi nafasi hizo wanazikalia au wakati mwingine wanazituma kwa taasisi husika wakijuwa waombaji hawatapata muda wa kujaza form na vitu vingine before deadline!

Watanzania sisi ni watu wa ajabu sana, mimi nilipata bahati ya kupata scholarship na kwenda kusoma nje, kitu kilicho nishangaza ni pale wafadhili walipo kuwa wanalalamikia Tanzania kwamba inapewa nafazi nyingi kwa ajili kuwasomesha raia wake, lakini ni watu wachache wanaojitokeza kwa hiyo wafadhili wameamua ku-scale down offers zao kwa Tanzania na kuwapa mataifa mengine kwa kuwa tunaonekana hatuna interest!

Kwa hiyo mimi siwezi kushangaa kama tabia hii inaendelea hata katika mambo ya ajila.
 
Ni kweli tunahitaji mabadiliko makubwa sana. Hata scholarships za Uholanzi utaratibu wa kuomba ulibadilishwa kutokana na hao hao na wengine wa nchi kama za kwetu.
 
Mojawapo ya matumaini makubwa ya kuanzishwa kwa sekretarieti ya Ajira nchini kwa mujibu wa sheria ni kusaidia kuajiri katika utumishi wa umma kwa niaba ya waajiri katika utumishi wa umma. Jambo hili lilionekana kuwa huenda ikaondoa ukandamizaji wa rushwa pamoja na upendeleo uliokuwepo wakati waajiri walivyokuwa wanaajiri wenyewe. Lakini cha kusikitisha mno ni pale hata sekretarieti hii imeingia kwenye mkumbo huo huo wa kutumia magumashi katika zoezi lao la kuajiri. Rushwa hii ipo hasa kwenye nafasi nyeti na kubwa kulinganisha na zile nafasi ndogo (direct entry). Utashangaa kuona watu wanaitwa kwenye interview kupitia magazeti mnaenda kwenye interview lakini matokea hamyaoni mnasikia tu fulani ameshaitwa kuanza kazi mbali na utaratibu unaojulikana kuwa mnafanya interview anayefaulu anatangazwa kama kawaida na ambao hamkuyaona majina yenu kujihesabu kuwa hamkubahatika. Hii kwa nini kama mtu amefaulu asitangazwe kwa utaratibu kama nafasi nyingine? Na si mara ya kwanza kuona mambo haya katika sekretarieti hii. Ukitaka kujua wameshacheza faulu zao utaona kimya majibu ya hiyo nafasi hayatatoka kama nafasi nyingine. Mfano mzuri ni interview iliyofanyika kati ya tarehe 14-23 May 2012. Wanakuja na majina kadhaa wanasema wasiona majina yao wajihesabu hawakufaulu. Je mbona nafasi hizo hazionekani kana zilipata watu au zitarudiwa????? Mapungufu mengine ni kama 1. Kutokuwa na special pannel ya kuinterview professionals. Utakuwa wazee wa agano la kale wasiojua kabisa kitu ndo wanafanya interview unaweza kujikuta unaoverqualify kuliko wao 2. Katibu wa sekretarieti hii pia ni tatizo kwa ubabe wake usiozingatia taratibu za interview 3. Siri kuvuja hata kabla ya matokeo kutoka 4. Wafanyakazi wa sekretarieti kutozingaziti viapo vya uadilifu wakati wa interview
 
Hivi ni wapi ktk sirikali hii hakuna rushwa?
Ukitaka kula na kipofu vunja lako jicho..... Tafuta anaepokea hizo pesa, halafu toa dau kubwa kama kweli uko serious na kazi. Otherwise acha wenye meno watafune. Hii ndo sirikali tuliyoichagua.
Next time kumbuka na hamasisha wadau wote kuacha kuipa madaraka sisiem.
 
Habari wana jamvi,
Ni mara ya kwanza kuitwa hawa watu kwa ajiri ya Interview. Ila kile kilichojitokeza jana kikiachwa kiendelee tutakuwa tunaendeleza ugonjwa uleule na kupoteza dhana nzima ya kuanzishwa kwake.
Nilibahatika kuingia kwenya mtihani wao wa maandishi ukilinganisha nawale ambao hawakupata nafasi ya kufanya mtihani huo, kwasababu zisizo na msingi za kukosa vyeti halisi vya elimu zao. Ikiwa matokeo ya mfumpo mbovu wa vyuo vyetu.
Kinachonisikitisha ni namna gani wanasahihisha hiyo mitihani yao kupata washindi kwa ajili ya Oral interview. Kwa mtihani ambao nimeufanya sijaona tatizo na kosa la kunifanya nisirudi kwa Oral interview.
Na sisitiza hii taasisi iangaliwe kwa macho mawil.i Nachelea kusema kuwa kuna dalili za Rushwa, Makisi za huyu kupewa mtahlniwa mwingine, Kuna ukabila.
Taasisi ichunguzwe kabla watanzania hatujapoteza imani nayo. Kwawale wamepata ajira kupitia taasisi hii kwa kubebwa watabeza ushauri huu.
Kwa wale waanga kama mm tujipe moyo tumaini linakuja.
IF YOU CANNOT KILL YOUR, BUY HIM

Huna hoja, kubali kushindwa kaa pembeni. Huna ushahidi wa rushwa, majungu ndio yamekutawala
 
Hongera ndg, Na lazima utamke haya na mi sikatai ila nia angalizo tu hiii taasisi kuwepo kwake kuna lengo kubwa kwa taifa hasa sisi vijana. Lakini kama nyumba inavuja ni lazima uzibe tundu kabla ya nyumba haijabomaka. Bado nina Imani ni taasisi ni mambo madogogo madogo inatakiwa yawekwe sawa. Mtihani niliofanya ulikuwa una maswali matano ambao nimefunga safari kutoka mbali kwa ajili yake.

Na juu ya hiyo kwa Interview ya 19/04/2012 pekee yake kuna zaidi Thread yangu inawalaumu hawa watu. So mpaka kufikia hapa ni Watanzania wangapi hawasemi ni ANGALIZO tu mkuu.

Kabla watanzania walio wengi hawajapoteza imani kwa taasisi hii


Wale waleeeee!!! Mkikosa mkubali kushindwa na siyo kuulizia dini yao au kabila zao! Haya ndo mambo nisiyotaka kabsaa!
Jipange sawa sawa, mwombe mungu pia na kama una vigezo utapata; me nilishaitwa pale mara mbili na nikakosa na niliridhika na kutopata. Haya mambo bana!!!!
 
Back
Top Bottom