Sekondari ya Ngudu ni shule ya serikali au ni ya kujifunzia ujasiriamali

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,344
Sikutegemea kama haya ninayoyaona katika shule ya Ngudu high school ningeweza kuyaona yakifanywa katika awamu hii ya Rais Magufuli.

Ya waalimu walioko mazoezi (field) kutumia muda wa kuanzia saa 11 jioni hadi saa 2 usiku na wakati mwingine muda wa kazi na katika majengo ya shule kufundisha tyusheni ya topic muhimu za kidato cha 5 na 6 na kisha kutoa majaribio na kutunga mitihani kutoka kwenye topic zile tu wanazofundisha tusheni ili kuwalazimisha wale wasio lipia walipie kusoma masomo hayo ya ziada.

Kwa kweli hata wale tulio na kauwezo kidogo tunaolipia tunaumia sana, hali hii haitupendezi kwa sababu inatuumiza kiuchumi na inatujengea matabaka ya makusudi na ya kijinga.

Cha ajabu kauli ya waalimu hawa ambao wameungana na waalimu wa ajira wa shule hii ni "Ukitaka vya bure rudi O level"

Kwa kweli huku ni kutunyanyasa tyusheni ya mwanafunzi kulipia mpaka laki moja watoto wa wakulima maskini wataitoa wapi?
Mheshimiwa Ndalichako tafadhali waokoe watoto hawa walioko shule hii kabla hawajafelishwa elimu na maisha na hawa waalimu wenye tamaa za kijinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aise Ngudu Kwimba... poleni sana vijana. Nilipita hapo 2006 - 2008.
 
mnh umejuaje yale wanayofundisha tuition,ndiyo wanayotungia mitihani?haujui kuna mtihani ambao ni standard kwa wote unakuja?
 
Someni tu,Ngudu ilikua na tatizo la walimu haswa wa science kwa A-level na sijui kama limeisha,kipindi nasoma hapo 2008-2010,tulikua tunajichanga na kukodi walimu toka Nganza.
 
Pole sana mkuu,nilikuwepo pale 2015 shule hiyo haifai kufundisha masomo ya science sio advance wala o level, Hakuna elimu pale hasikwambie mtu
 
Back
Top Bottom