Chosen man
JF-Expert Member
- Dec 30, 2017
- 520
- 722
Shule ya sekondari ya Kemebos iliyopo Bukoba mkoani Kagera haipaswi kuwa inaonekaka katika "Top ten schools" kwa sababu kimsingi hakuna shule inayoitwa Kemebos.
Katika shule ya Kaizirege ndipo ambapo wanafunzi wote hufundishwa na wakati wa mitihani ya kitaifa huchukuliwa wanafunzi bora kadhaa kutoka Kaizirege na kuwasajili kama Kemebos kwa lengo la kuuhadaa umma wa Watanzania wasiojua.
Kimsingi hizi shule mbili ni shule moja na walimu ni hao hao na watoto wanasoma pamoja isipokuwa hutenganishwa siku za mitihani pekee.
Matokeo yake utasikia eti Kemebos imekuwa ya kwanza ilhali ni ujanja ujanja mtupu na baadhi ya walimu wanaonekana katika orodha ya walimu bora wa masomo kumbe si kweli. Matokeo halisi yanapaswa kuchanganywa ya KAIZIREGE na KEMEBOS pamoja ndio uhalisia utaonekana.
Nahitimisha kwa kusema "HAKUNA SHULE INAITWA KEMEBOS"