Sekondari ya Kata yapokea wanafunzi 'vimeo'

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Kuna taarifa kuwa wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari ya Mgololo iliyoko Wilaya ya Mufindi, Iringa hawajui kusoma wala kuandika
Mkuu wa shule amemwandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kumlalamikia kupelekewa wanafunzi ambao hawajui kujua kusoma wala kuandika na akapendekeza wapelekwe shule ya msingi. Habari hizi zimeeleza kuwa watoto hawa 10 wako kati ya kidato cha pili na cha nne. Maelezo yanasema kuwa jitihada za kuwa rudisha shule ya msingi limekuwa kuwa gumu kwani sera ya elimu hairuhusu mwanafunzi aliyehitimu shule ya na 'kufaulu' kurudi tena shule ya msingi. Mmoja wa watoto hao aliyepata alama 166 kati ya 250 katika mtihani wake wa darasa la saba hakuweza kusoma sentensi zifuatazo- "Bibi anakula chakula" au "Mama analima bustani" . (Habarileo 18.9. 2011)

Naomba tutafakari hili kwa kina. Hivi hapa shida ni nini?
 
Wakulaumiwa ni serikali au waalimu wa primary na wazazi kwakukubali kumsogeza mtoto mbumbu.
 
Hili ni janga la kitaifa. Inabidi serikali ielekeze nguvu zake katika kuimarisha elimu ya msingi na kuacha blah blah. Hivi miaka ile ya 60 na mwanzoni mwa 70 tuliwezaje? Tunapaswa kutafakari na kufanya maamuzi sasa kabla nchi yetu haijaangamia.
 
Back
Top Bottom