Sekondari Rugambwa yaungua ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sekondari Rugambwa yaungua !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bw.Ukoko, Sep 5, 2009.

 1. B

  Bw.Ukoko Member

  #1
  Sep 5, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimepata taarifa hivi punde kuwa bweni la sekondari kongwe ya wasichana iitwayo Rugambwa iliyoko Bukoba imeungua moto leo saa 7 mchana.

  hata hivyo hakuna aliyekufa wala kujreruhiwa,ingawa magodoro na mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea kwa moto.

  kikubwa ni kuwa wanafunzi wamelazimika kuwabeba wafanyakazi wa kikosi a zima moto cha manispaa ya Bukoba ambao wamefika hapo dk 10 tu mara baada ya moto kulipuka na wameweza kuazima moto huo .

  chanzoi cha moto bado hakijafahamika

  Hivi ni kwa nini kasi ya mabwweni ya wasichana kuungua inaongezeka ?
   
 2. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hii trend inashangaza, mabweni ya wasichana yanugua mara kwa mara. Ukifuatilia utakuta kuna miongoni mwao wanajipikilisha na zikitokea ajali wanasingizia hitilafu ya umeme.

  Poleni sana watoto wa Rugambwa!
   
 3. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Kakalende!
  Kwanza natoa pole kwa watoto na wazazi waliounguliwa bweni matokeo ni kupotea mali na matarajio ya sehemu za kuweka mbavu. Kila siku mimi nawashikia Bango CCM kwani kwa miaka 48 ya utawala wa CCM wamekuwa wasanii na kuweka sera zinazopita bila ya tathimini na kuanda mfumo endelevu.

  In a nut shell kwa kuwa hakuna mfumo kila kitu chajiendea kwa staili ya kuzima moto. Majengo hayafanyiwi ukaguzi kila baada ya miaka mitatu kama inavyotakiwa katika taratibu za mipango miji na makazi. Halmshauri, municipal or City authorities wanakimbizana bila kutekeleza jukuumu lao la kuhakikisha majengo yote kuanzia viwanda maofisi na mashule yanakaguliwa kufuatana na taratibu au by laws walizoziridhi kutoka kwa wakoloni wao wako tayari kuweka bylaws zinazoweza kuwapatia pesa za kuendesha vikao chapu chapu kwa staili ya vodafasta.

  Hadi hapo the GVT structure itakapomka na kuacha politic kwenye maisha kuungua kwa majengo yawe ya watu binafsi au serikali wataendelea kusingizia umeme as if nobody has ever gone to school!! Hata kama banda halina umeme utasikia hitilafu ya umeme.

  There are over 20 quick causes of fire na kubwa ni uchakavu , matumizi yasiyo sahihi ya majengo na kutokuwepo na risk assesment katika maisha ya Wtz. Hiyo faya tender ilitakiwa itoke umbali gani na barabara ziko je? Kwa nini tusijiwekee hata local fire fighting systems which are user friendly badala ya kulalamikia fire brigade. Kwa mfano moto unatokea Kimara au hata Mabibo kutoka pale faya hadi Ubungo kwa msongamano uliopo wa magari kwenye barabara ya Morogoro hiyo nyumba itakuwa jivu basi tujipange upya lakini count me out kama CCM bado wako madarakani hilo haliwezekani msahau. Kama kwa miaka 48 wameshindwa hata wakipewa miaka mingine 100 hawawezi.
   
Loading...