Sekeseke la mafuta, kushuka kwa bei ya mbaazi na hekima za Franklin D Roosevelt

Benittotz

Member
May 24, 2018
68
150
SEKE SEKE LA MAFUTA,KUSHUKA KWA BEI YA MBAAZI NA HEKIMA ZA FRANKLIN D ROOSEVELT.

Mnamo mwaka 1933 mtikisiko wa uchumi ukiwa umepamba Moto huku Vita vya pili vya dunia vikiwa mwanzoni. Mzee mmoja akiwa ndio kwanza amekabidhiwa dhamana ya kuliongoza taifa kubwa duniani huku akiwa kwenye kiti Cha matairi Cha kutembelea. Matatizo yaliyosababishwa na polio mwaka 1921. Mzee huyu anavuta karatasi na kutoa kalamu kisha anawaita wabobezi wake wa uchumi na kitu wanachoandika kinatoa taswira mpya katika uchumi wa Marekani na dunia kwa ujumla. Mtu huyu anafahamika kwa jina la Franklin Roosevelt raisi wa 32 wa Marekani na aliyeongoza kuanzia mwaka 1933 mpka 1945 mauti yalipomkuta. Takribani miaka 12 madarakani.

Wakati Roosevelt anaingia madarakani kulikuwa na mtikisiko mkubwa wa uchumi, hivyo akaamua kunitumia siku zake 100 za kwanza madarakani kuleta ufumbuzi wa tatzo Hilo. Moja kati ya vitu alivyotengeneza kwa wakati ule kupitia mpango wake wa New Deal ilikua ni Agricultural adjustment administration. (AAA) Hii ilihusika na kununua mazao yaliyozidi kwa wakulima ikiwa NI nafaka au mifugo. Kutafuta masoko na kuwalipa fidia wakulima wachache waliobaki sokoni kutokana na athari za mtikisiko wa uchumi ili wasilime baadhi ya sehemu za mashamba yao. Kwa kuwazuia kulima kulisaidia kupunguza kiwango Cha bidhaaa sokoni na kuipandisha Bei ya bidhaaa husika.

Walitoa Wapi Fedha Za kuwalipa ilihali uchumi ulikua mbovu na taasisi za kifedha ziliamuriwa kufungwa kwa wakati ule ili kulinda Amana isitolewe?
Kupitia Sheria hii ya usimamizi wa kilimo kulikua pia na taasisi iliyoundwa kusimamia usambazaji wa fidia hizi na ununuzi wa mazao hayo. Fedha za kuwalipa wakulima zilitokana na Kodi maalumu iliyokusanywa kutoka kwa makampuni yaliyokuwa yananunua mazao hao Kama malighafi kwa ajili ya kuzalisha bidhaaa zao.

Tukiachana na hadithi hiyo iliyotengeneza historia ya moja Kati ya viongozi waliopata kuwa maarufu Sana duniani. Hapa nyumbani kwetu Tanzania kumekuwa na sintofahamu kuhusu ongezeko la Bei ya mafuta ya kula na kushuka kwa Bei ya mbaazi kwa kiwango kikubwa. ( zipo bidhaaa nyingi zinazoathiriwa au kuathiri ulaji kwa mabadiliko ya Bei ila ningependa kuzungumzia hizi mbili zaidi,mafuta ya kula na mbaazi).

Kumekuwa na hadithi nyingi mitaani, kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na kutoka katika mijadala ya bungeni pia. Wakati baadhi ya wabunge wakilalamikia kushuka kwa Bei ya mbaazi na athari hizo kwa wakulima ambao ni wananchi wao, huku wakiomba serikali kuingilia Kati. Upande mwingine wafanyabiashara, walaji na wabunge wengine pia wamekua wakipigia kelele ishu ya kupanda kwa Bei ya mafuta ya kula.

Wakizidi kwenda mbele zaidi na kudi pengine urasimu unaotumika kuhakiki mafuta yaliyokwama bandarini Kama NI ghafi au nusu ghafi unachangia kwa kiasi kikubwa mfumuko huu wa Bei.
Kwa tafsiri nyepesi ya kiuchumi mfumuko wa bei huashiria kushuka thamani kwa fedha inayotumika kufanya manunuzi na kwamba kipimo kile kile au pengine kidogo Zaid kitanunuliwa kwa fedha nyingi Zaid ya ilivyokuwa awali.
Swali la haraka haraka la kujiuliza ni je wakulima wa alizeti na ufuta nchini hawawezi kuzalisha kiwango Cha kutosha kutengeneza mafuta yanayokidhi mahitaji ya nchi? Kama wanaweza? inashindikana Nini kuweka msisitizo katika viwanda vya usindikaji na kutengeneza mafuta haya pasi kuuza malighafi zetu na kuagiza bidhaaa kutoka nje kwa Bei juu? Kama viwanda vipo ila changamoto ni malighafi basi ni hatua gani zimetumika kukuza uzalishaji wa zao hili?
Na kwa kuwa uzalishaji mkubwa si jambo la usiku mmoja basi ni hatua gan zimechukuliwa kuhakikisha mafuta ghafi au nusu ghafi yanaingia nchini kwa kiwango na Bei ambazo hazitamuumiza mlaji wa mwisho Bila kuathiri faida ya muuzaji?
Kama Roosevelt na wanauchumi wake walikaa chini na kufanya maamuzi yaliyosimamiwa vyema na kuleta matokeo chanya katika wakati mgumu Kama ule sisi tunakwama wapi ilihali Hali yetu bado si mbaya kulinganisha na ile ya 1933?

Vipi kuhusu mbaazi? Bei iko chini sawa na bure. Gharama za mkulima hazirudi, faida haionekani. Kifanyike nin kuokoa hili jahazi. Tuendelee kumwachia mkulima na mbunge wao wapambene na Hali zao wenyewe? La! kwani naamini kuathirika kwao NI kuathirika kwetu pia.So serikali yetu inampango gani katika kutafuta soko, kutoa mbinu na kuja na mbadala utakaoondoa kilio hiki.
Kwa ufahamu wangu mdogo wa Mambo ya UCHUMI ningependekeza yafuatayo:

1. Serikali itengeneze Sera rafiki zitakazo well mkazo katika ukulima wa kidigitali hivyo kuwa na uzalishaji mkubwa wa malighafi hususani kwenye ishu ya mafuta na kuondoa changamoto ya kuagiza mafuta ghafi kutoka nje Kama hili linasababishwa na uzalishaji duni nchini.

2. Kuboresha Sera,kuanzisha mazungumzo na kuweka msisitizo katika kuwekeza katika viwanda vya kusindika nchini na hivyo kuepuka usumbufu wa kucheleweshwa, kupatikana kwa uchache au namna yoyote ile inayopelekea kupanda kwa Bei kwa sababu ya ku import mafuta.

3.Kufanya utafiti wa taarifa za masoko. Hii itawasaidia wazalishaji kupata masoko kwa urahisi na kwa bie poa. lakin taarifa hizi zitatoa muongozo wa kiwango gani kinahitajika sokoni hivyo kuepuka tatizo la kuzalisha kupita kiasi ( Kama ilivyo katika mbaazi)au chini ya kiwango Kama ilivyo katika mafuta. Baada ya kulijua vyema soko la ndani n mahitaji yake itakuwa rahisi kufahumu kiasi gani Cha kupeleka nje na katika nchi gani.

4 .Kuwekeza katika ushindani wa kweli .

5. Kupunguza au kuondoa baadhi ya vikwazo vya kibiashara katika baadhi ya mahitaji muhimu. Vikwazo hivi ni Kama leseni, Kodi, au quota. (ukomo wa kiwango cha bidhaa kinachopaswa kutoka au kuingia nchini).

Kwa kuhitimisha makala hi fupi mbayo NI dhahiri haijagusa kila Kona ya Jambo hili ukizingatia ukubwa wake ulivyo, niseme tu kuwa kila changamoto inayokuja mbele yetu inakuja kwa sababu uwezo wa kuitatua tunao. Tanzania Ina vijana wengi wasomi na wabobezi katika Mambo haya. Tuwape nafasi,tuone mawazo yao mapya yataleta mabadiliko gani na tuwasupport kwa kuwa wote lengo ni kutengeneza kesho iliyobora. Tukipunguza urasimu, kuacha kufanya vitu kwa mazoea na mihemko ya kisiasa ni wazi tutakamajenga uchumi imara na kufikia lengo.

KAMA UNA MAONI, NYONGEZA, AU MAREKEBISHO SEHEMU AMBAYO UMEONA TAARIFA HAIKO SAWA USISITE KUSASILIANA NAMI NA MAWASILIANO NILIYOWEKA HAPO CHINI.

IMEANDIKWA NA
BENSON FLEXON SHIRIMA
MHITIMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM SHULE YA BIASHARA.
Email ; bensonflexon@gmail.com
Facebook; Benson Flexon to
Instagram @benitto_tz
Twitter Benittotz
Watsap [HASHTAG]#0654859954[/HASHTAG]
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom