Sekeseke la Katiba Mpya ilikuwa ni ajenda ya CHADEMA?

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,205
15,162
Wasalaam Wakuu!.

Leo CHADEMA walikuwa na jambo lao waliloliita KATIBA DAY ambapo viongozi wao wakuu wa Chama pamoja na wanachama wao mashuhuri walihudhuria katika kongamano hilo.

Suala la Katiba mpya ni lenye umuhimu kwa maslahi mapana ya taifa letu..

Lakini, tujitafakari! Hii ilikuwa agenda ya CHADEMA tangu hapo awali ama wamebadili gia baada ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan kugusia juu ya swala lenyewe?

Je, endapo mwendazake angekuwa hai mpaka leo agenda hii ingefanikishwa? Ama ndo wasingethubutu kulizungumzia?

Mwendazake alishwahi kutamka kuwa suala la Katiba siyo moja ya vipaumbele katika awamu yake. Na kamwe CHADEMA na vyama vingine, havijawahi kuthubutu kutamka ama kuthubutu kutoa miguu yao kujaribu kushinikiza kupatikana kwa katiba mpya.

Kwa nini iwe sasa hivi? Ni baada ya kupima kina cha maji na kuona Mh Rais na taasisi zake zimepoa?
 
Bwana Compact, inawezekana Tanzania nzima yenye watu zaidi ya milioni sitini wanaoona umuhimu wa Katiba Mpya ni Chadema peke yao? Kama hivyo bora Marehemu Kleist Sykes angezaliwa Kenya na sio Tanzania!
 
Chadema ni Kama ndege mitini.

Angekuwa hai hayati JPM kamwe wasingeleta "pang'ang'a zao hizo"...

Dawa yao ni "kuwakazia tu".

#UkichekaNaNyaniUtakulaMabua
 
Ujinga aliyoufanya mwendazake kwenye uchaguzi (uchafuzi) wa 2020 ndiyo uliyopelekea jiwe kufa na hili vuguvugu la kutaka katiba kuwa kubwa mno.

Sasa rais SSH asijiribu kwenda kinyume na matakwa ya wengi. Yatamkuta.
 
Swala la katiba mpya lipo tokea siku nyingi. Mwendawazimu ndie alieua mchakato wote na kuua demokrasia hapa nchini. Sasa kwakuwa ameshaenda kwa mashetani wenzake hatuna budi kurudi katika zama za kujitambua na kuelewa umuhimu wa katiba mpya kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu kwa sasa kwa vizazi vijavyo

Ukiona mtu anapinga katiba mpya huyo hana uzalendo na nashauri apimwe mkojo labda ni mhutu sio Mtanzania.
 
Wasalaam Wakuu!.

Leo CHADEMA walikuwa na jambo lao waliloliita KATIBA DAY ambapo viongozi wao wakuu wa Chama pamoja na wanachama wao mashuhuri walihudhuria katika kongamano hilo...
Uchaguzi wa 2005 ilani ya CHADEMA ilikuwa na agenda ya katiba mpya.

Uchaguzi wa 2010 Ilani ya CHADEMA ilikuwa na agenda ya katiba mpya.

Uchaguzi wa 2015 ilani ya CHADEMA ilikuwa na agenda ya katiba mpya.

Uchaguzi wa 2020 ilani ya CHADEMA ilikuwa na agenda ya katiba mpya.

Mwaka 2010 CHADEMA walifanya maandamano pale Arusha yaliyochochea rais Kikwete kutangaza kuanzisha mchakato wa katiba mpya.

Bado swali lako halijapata majibu ?
 
Wasalaam Wakuu!.

Leo CHADEMA walikuwa na jambo lao waliloliita KATIBA DAY ambapo viongozi wao wakuu wa Chama pamoja na wanachama wao mashuhuri walihudhuria katika kongamano hilo...

Magufuli alikuwa rais muovu, na muovu yoyote hataki miongozo ya haki. Pamoja na kutumia mabavu bado watu waliendelea kuongelea katiba mpya, na hata wakati wa kampeni za ule uchafuzi ulioendeshwa na yule ibilisi, bado watu walizungumzia katiba mpya. Huenda wakati hayo yakizungumzwa ulikuwa jela.

Na kwa taarifa yako hata kama angekuwa hayuko motoni, bado katiba mpya tungeiongelea kwa njia mbalimbali. Tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule mtu muovu bila damu kumwagika.
 
Bwana Compact, inawezekana Tanzania nzima yenye watu zaidi ya milioni sitini wanaoona umuhimu wa Katiba Mpya ni Chadema peke yao? Kama hivyo bora Marehemu Kleist Sykes angezaliwa Kenya na sio Tanzania!
Mkuu Cliffhanger

Sibishi kuhusu umuhimu wa Katiba Mpya. Ninachodadisi ni kwamba mbona imekuwa ghafla sana katika miezi minne ya awali ya Rais Samia?

Je, JPM angekuwa hai haya yanayoendelea sasa hivi yangefanyika? Au kwa sababu mama mtaratibu?
 
Ujinga aliyoufanya mwendazake kwenye uchaguzi (uchafuzi) wa 2020 ndiyo uliyopelekea jiwe kufa na hili vuguvugu la kutaka katiba kuwa kubwa mno.

Sasa rais SSH asijiribu kwenda kinyume na matakwa ya wengi. Yatamkuta.
WEWE UNA AKILI TIMAMU?
 
Uchaguzi wa 2005 ilani ya CHADEMA ilikuwa na agenda ya katiba mpya.

Uchaguzi wa 2010 Ilani ya CHADEMA ilikuwa na agenda ya katiba mpya...
Katika miaka ya hivi karibuni (2016-2020), CHADEMA kwa namna yeyote hawakuanzisha vuguvugu lolote la kudai Katiba Mpya.

Wala hawakuwahi kulizungumzia. Angalau tume huru ya Uchaguzi waliigusia. Lakini kamwe juu ya katiba walikuwa kimya kama maji chunguni.

Walikuwa waoga? Ama wanapima na nyakati za kuanzisha vuguvugu?
 
Nyie ndo wale mnaofanya Watanzania waonekana mabingwa wa kujadili petty issues!

Katiba Mpya ni ishu ya wananchi.

Hivi hujui kuwa CDM nao wanawakilisha wananchi wenye hitaji hilo?

Hivi unajua kuwa agenda ya Katiba Mpya ilianza tangu vuguvugu la vyama vingi lilipoanza nchini miaka ya 90 mwanzoni kabisa??
 
Suala la kudai katiba mpya kwa CHADEMA ni jambo la kudumu, toka CHADEMA inazaliwa 1990s mpaka leo hii agenda yao kuu ni Katiba mpya. Huwezi kuitenganisha CHADEMA na harakati za kudai katiba mpya hapa Tanzania, na huwezi kuwatenganisha watanzania wengi na dai la uwepo wa katiba mpya.
 
Back
Top Bottom