Seif atoa masharti ya kurejea CCM

Tukubaliane kuwa hata kama Seif kaamua kutoa porojo la Idd el fitri,bado watu kama yeye sio wa kizazi hiki kinachotaka mabadiliko ya kweli na chenye uchungu na hali ya nchi ilivyo.Mapambano haya yataendeshwa kwa dhati na watu ambao wanapinga utawala mbovu kwa manufaa ya WaTz na sio wale wanaopinga baada ya kutemwa na system.
 
Wazee hizo sio porojo za Idd. Hapa tayari kuna makubaliano na nadhani huyu bwana kishaahidiwa nafasi huko CCM sasa anatupa hint kinamna.
 
Wakati mwingine ni vizuri kusoma ujumbe wote kabla ya kuja na conclusion.

Anachosema Hamad ni kwamba hakiwezekani kwahiyo hawezi kurudi CCM.

Pia hata kikiwezekana? Basi hiyo haitakuwa CCM tena na badala yake itakuwa ni CUF au mawazo yanayofanana na mawazo ya akina Hamad.

Tuangalie hapa nasisi tusije tukawa kama akina Marando waliosema Nyerere ameambiwa wao ni mbwa (Go to the dogs) wakati maana ye Nyerere ilikuwa tofauti kabisa.

Unless mtu ana motive nyingine sioni kama alichosema Hamad sasa kinatofautiana na msimamo wake wa wakati wote.
 
I TOLD YOU GUYS CUF WANAJIMALIZA WANAHITAJI KULETA VIJANA ...UNAJUA KURUDI CCM KUNAAZA NA WAZO..kufikiria tu ni dalii.sembuse kuongelea..na kutoa masharti hata yakiwa magumu namna gani..ni dalili ya pili kuwa unaweza kurudi ..na kwa daliili hii hata usiporudi labda kwa kuhofia aibu..unabaki ccm kiimani...kwa hiyo huwezi kuwa kiongozi wa upinzani bora kubakia mwanachama tu!!!

Ni hivi, kama masharti hayo yakishindikana, atayalegeza mwenyewe Sefu. Ni suala la bargaining ndani ya nafsi yake mwenyewe. Nilipokuwa shule tulikuwa na msichana mmoja mzuri sana ambaye kila mtu aliusifia uzuri wake. Basi alikuwa anatamba kwamba kwa uzuri ule hawezi kukubali kuchafuliwa na mmatumbi, yeye wa kwake ni watasha tena wa class ya juu. Tukamaliza shule, JKT, chuo, bado anasubiri mtasha, hakutokea! Akapunguza masharti, akasema atakubali mswahili, lakini lazima awe handsome na amekwenda shule si chini ya masters, na awe wa class ya juu. Miaka ikasonga, hakutokea mtu huyo! Akaendelea kupunguza masharti, na sasa hivi niandikapo post hii ana mtoto mmoja ambaye amezaa na dereva wake ambaye ni mume wa mtu! Ujumbe: ni suala la muda tu, masharti hayo ya Seif yatayeyuka mojamoja kama barafu na baadaye yatatoweka kabisa, na atarudi CCM kwa utashi wake kama walivyorudi kina (marehemu) Chifu Abdallah Fundikira, Richard Tambwe Hiza, Salum Mbarouk Msabah, Abbas Zubeir Mtemvu, Dr Masumbuko Lamwai, Dr Amaan Walid Kabourou (alimsumbua sana Premji kule Kigoma huyu), na hivi majuzi Shaibu Akwilombe. Kama sikosei, hata yule Leo Herman Lwekamwa mwanzilishi wa TLP aliyekuwa na ile kesi maarufu iliyonunuliwa na Mrema ya "kuisigina" katiba ya nchi ati kwa kuwa ina rangi ya kijani alisharudi CCM kulamba matapishi yake!

Siku zote nimekuwa nikiamini kwamba wapinzani wa kweli na makini wapo, lakini sidhani kama Seif Shariff Hamad ni mmoja wao! Mwezi uliopita kwenye ile talk show maarufu Bongo ya Mzee Makwaia wa Kuhenga, Prof Lipumba katika kuelezea wanachama wake walivyo ngangari alidai hata Maalim Seif akirudi CCM, hakuna mwana-CUF hata mmoja atakayemfuata. Tamko kama hili linaashiria uwezekano wa mwenzie huyo kurudi CCM (tazama neno linalotumika ni "kurudi" CCM na wala si "kujiunga" na CCM.

Inanikumbusha wimbo huu tulipokuwa watoto:

"Watoto wangu eeh, Mimi mama yenu,
Sina nguvu tena, ya kuua simba,
simba ni mkali, aliua baba,
aliua babu, aliua bibi,
basi wanangu kimbieni!"
 
kumaanisha CUF imekwisha, na wataanza upyaaaaaaaa ! heheee, bado Mbowe ! kwanza mbowe nae atachoshwa weeeeee kama akina lipumba na seif then nae atasema vichekesho vyake !

Furahi mtetezi wa mafisadi na majina yako mengimengi humu
 
Furahi mtetezi wa mafisadi na majina yako mengimengi humu

Yaani nilipoona tu mtu wa mwisho kupost hii thread ni huyu shallow-m, nikajua tu atakuwa ameniquote ! i knew it !

Kama natumia majina mengi humu, kwa nini waliponiban nisingetumia hayo majina mengi niliyonayo kutetea hoja yangu huku nikijua fika kwamba nina majina mengi ? Kwanini sijipi thanks na ziwe nyingi ? Yaani i really dont see any way/benefits of me using a bunch of names other than hilo la KadaMpinzani. Au kuna watu wanakupinga sana kama mie ndio unasema watu hao ni mimi, kwa kifupi ni vigezo gani unavyotumia wewe kusema kwamba Kada ana majina lukuki humu !

najua hautojibu, utakimbia tu wewe !

Natumia jina moja tu na hilo ni KadaMpinzani, Kada'sAdvote jamaa nitampa baadae maana hajaamua kuja JF yet ! Kama nikiamua kuwa na majina mengi sishindwi na nitasema chochote kama ninayo hayo majina mengi maana sio kosa hivyo nisingeficha chochote ! Watu bana kwa kujifanya wanawajua watu, oooh !
 
Waungwana hata mfanye Tafsiri/Marekebisho ya namna gani ya "Kauli Tata" ya Mzee Seif,bado kuna ukweli usiopingika kuwa Maalim amekuwa Muflisi Kisiasa,na ni wakati mwafaka kwake kukaa kando na kuwaacha Vijana wakiendeshe chama.Mawazo na Kauli zake zinadhalilisha Chama.Waungwana wa CCM watatumia kauli hizo kuudhoofisha Upinzani haswa CUF.Washauri wa hawa Wakuu inapaswa kupitia maandiko yao kabla ya kuyaweka wazi hadharani,Kauli nyingine zinabomoa kabisa maana ya Upinzani!!.Tupo Vitani kuelekea Kwenye Mabadiliko,Yeyote anayeonekana kuwa kigeugeu ni lazima tumshushe njiani!,Tunataka watu wakakamavu na wenye Nguvu za kupambana na CCM,Na sio kuomba namna ya kurudi kwenye Gari la CCM.
 
Asante Mwawado...

message nzito hapa!
 
Katibu mkuu wa chama cha Wananchi CUF amesema atarejea kwenye chama tawala cha CCM

Heshima mbele wakuu, baada ya kuisoma hii kwa makini ukweli ni kwamba kama kweli unaujua mchezo wa siasa, basi unaelewa kuwa hayo juu ndio hasa iliyokuwa nia yake kuyasema, zaidi ya hapo anadanganya,

mimi ningekuwa member wa CUF, ningewaomba viongozi wangu kumfukuza huyu mkuu sasa hivi bado mapema kabla hajaendelea kutia more damages kwa CUF, kwa sababu ni clear bin wazi kuwa huyo mkuu tayari yumo ndani ya CCM,

Kule DC, huwa kuna Associates Press Dinner, ambapo viongozi wengi wa pande mbili yaani Democrats na Republican, huwa wanakutana na kufanya comedy like things, kwa mfano mara ya mwisho Karl Rove, alijifanya Snoopy Doggy Doggy,

pamoja na utani wote unaoruhusiwa usiku huo, sijawahi kusikia utani wa Karl Rove anataka kuingia Democratic Party, au James Carville na Begalla, wakisema wanataka kuingia Republican Party,

kwa hiyo reading between the lines huyo mkuu Seif, ni sell out!
 
Kwani huyu Seif aliondoka lini CCM?...
Hivi bado hamjaamini kuwa baadhi ya vyama vilianzishwa kuonyesha tu Upinzani na CCM ili misaada ishuke?..
Haya najua tu kinachofuata Wadanganyika mtataka ushahidi!
 
mie nimeenda kusoma tena kule nipashe habari yote.

kwa kweli inaonyesha nipashe walifanya mahojiano na maalim seif makao makuu ya cuf mtendeni zanzibar.

ktk mahojiano hayo kuna maswala na majibu na wameahidi kuchapisha mazungumzo yao ktk gazeti la jumapili sasa tusubiri ili tuone mazungumzo yote.

nnasema hivyo huwezi kujua format ya suala lilivyokuja hata akajibu suala hilo.

mie si msomi sana wa biblia ila kuna maandiko yanasema "upumbavu wa mungu si hekima ya mwanaadamu"

haimaanishi hata siku moja kuwa mungu ana upumbavu, bali hii ni lugha ya kuonesha kuwa mungu ana hekima nyingi.

au sisi zanzibar tuna nyimbo ya msewe:
" kama si kule kuswali ningegema
hatia tembo kinywani halewa vyema

tumbili matango yangu kayachuma"

sasa mtunzi wa nyimbo hakusudii kabisa kama atalewa ila anaonyesha wazi kuwa kuswali hasa hakupelekei kulewa.

nnasubiri mawazo ya wengine baada ya kuchangia ya kwangu
 
mwaga mashairi babu !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! ntu wa pwani hali chamaki nchaga hata iwego !
 
mie nimeenda kusoma tena kule nipashe habari yote.

kwa kweli inaonyesha nipashe walifanya mahojiano na maalim seif makao makuu ya cuf mtendeni zanzibar.

ktk mahojiano hayo kuna maswala na majibu na wameahidi kuchapisha mazungumzo yao ktk gazeti la jumapili sasa tusubiri ili tuone mazungumzo yote.

nnasema hivyo huwezi kujua format ya suala lilivyokuja hata akajibu suala hilo.

mie si msomi sana wa biblia ila kuna maandiko yanasema "upumbavu wa mungu si hekima ya mwanaadamu"

haimaanishi hata siku moja kuwa mungu ana upumbavu, bali hii ni lugha ya kuonesha kuwa mungu ana hekima nyingi.

au sisi zanzibar tuna nyimbo ya msewe:
" kama si kule kuswali ningegema
hatia tembo kinywani halewa vyema

tumbili matango yangu kayachuma"

sasa mtunzi wa nyimbo hakusudii kabisa kama atalewa ila anaonyesha wazi kuwa kuswali hasa hakupelekei kulewa.

nnasubiri mawazo ya wengine baada ya kuchangia ya kwangu

Mtu wa pwani nakubaliana na wewe kabisa na uchambuzi wako. Unajua waandishi au hawa wahandisi wanatapia ya ku pick and choose headlines za kuuza magazeti. Kwa kuwa hiyo interview itawekwa yote jumapili ngoja tuisome yote tujue walikotokea mpaka maneno kama hayo yakatamkwa.
 
I believe hii ni propaganda ya kui weaken CUF, it is unthinkable for seifu kurudi CCM, he is a formidable force Zanzibar na anajua ana support kubwa kuliko hata Abeid

At least it is something to believe never proved!!! let us believe so!!!
 
CCm ya JK ni jalala la takataka, kila amayetaka kuingia anaingia hata kama hana sifa.
 
Mimi Sioni Ajabu Maana Huyu Bwana Ni Mmoja Wa Mafisadi Waadilifu,
Ukienda Zanzibar Ndipo Utajua Huyu Bwana Ni Nani;;ametofautiana Na Wenzake Kwa Kuwa Fisadi Muadilifu;;mwambien Tutamchora Alichojilimbikizia Kule Oman,nk,,,,,,sishangai Fisadi Kurudi Kwenye Chama Cha Mafisadi,,mtoto Wa Nyoka Si Nyoka Jamani....baby Akililia Wembe Mpe .....karibu Uonje Kaka ..labda Watakupa Nafasi Ya Balali
 
Una ushahidi gani? Tuletee basi the dataz, maana kusema mtu kajilimbikizia utajiri Oman bila kuleta angalau ushahidi mdogo nafikiri tunarudi kule kule kwenye kashfa za Salim ambazo karibu zote zilikuwa uzushi kwa ajili ya kumchafua.

Pamoja na mapigo yote ya CCM, sijawahi kusikia wakisema Hamad kajilimbikizia mali sehemu.

Kinachonitisha ni hii tabia ya sasa ambayo kila mwanasiasa basi sio msafi. Huenda ikawaogopesha watu waadilifu kuingia kwenye siasa. Lazima tutofautishe makosa ya kila mtu na sio kuwalundika wote pamoja.
 
samahani wakuu ngoja kwanza nimalizie kucheka maana nimeisoma hii habari kwenye nipashe ya trh 12/10/07 imeniacha hoi kweli kweli. Okay ngoja uhondo kwa kukandamija habari kamili (kicheko kimeisha)

katibu mkuu wa chama cha wananchi cuf amesema atarejea kwenye chama tawala cha ccm kama atapewa nafasi ya kuwa makamu wa rais na kuitisha kwa uchaguzi ndani ya miezi mitatu na kuwa rais wa muungano. (kicheko kinaendelea)

alisema kama ccm itakuwa tayari kufanya mambo hayo yuko tayari wakati wowote kuanzia sasa kurejea kwenye chama hicho kwa vile atatekeleza ahadi aliyoitoa kwa wananchi ya kuwaletea maendeleo.

Aliyasema hayo wakati akiongea na nipashe kwenye kumbukumbu ya kifo cha nyerere. Aliendelea kusema kuwa hajui ni lini atajiuzuru siasa maana mpaka sasa hajawatekelezea wananchi aliyohaidi, ambayo ni kuleta mabadiliko kiuchumi na kisiasa.

Mzee ameongea mengi ila hayo ndiyo niliyo yaona kuwa niyamsingi, natumaini sitahukumiwa kwa maneno niliyo acha ambayo siyo ya msingi. Haya kazi kwenu kumchambua mimi nimemaliza. ( ngoja nimalizie kicheko maana huo mtihani mgumu inabidi shein atolewe kafala halafu afuate jk sijui kama inawezekana but i believe below the sun nothing is impossible)
naomba kutoa hoja waheshimiwa....wana.....jf

hatimae yametimia kashaupata umakamu wa rais kwa ccm-b kumbe tangu 2007 alisharudi ccm
 
Back
Top Bottom