Seif anatumia nafasi yake katika SUK kuvitaka vyombo vya dola kumshughulikia Hamad Rashid? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Seif anatumia nafasi yake katika SUK kuvitaka vyombo vya dola kumshughulikia Hamad Rashid?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Dec 28, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Katika Mwanahalisi la leo kuhusu sakata la CUF, kuna sehemu ya habari imenishtua:


  Sehemu husika ya habari:

  Awali akiandika kwa Prof Lipumba, Maalim Seif anasema, "Nimefurahi kwa mahojiano yako na DW (kituo cha redio cha Deutsche Welle) kuwa ukatibu Mkuu hautafutwi kwa mbinu za kimafia."

  Anasema tayari Mtatiro ametahadharisha jeshi la polisi mkoani Tabora juu ya Hamad Rashid na wenzake. Maalim anasema Mtatiro ameeleza mkuu wa polisi wa mkoa wa Tabora (RPC) na mkuu wa polisi wa wilaya ya Urambo kuwa wanaokwenda mkoani mwao kufanya mikutano ya hadhara ndio waliosababisha fujo jijijini Dar es Salaam.

  Barua ya Mtatiro ya 15 Desemba 2011 kwenda kwa mkuu wa polisi mkoa wa Tabora, inatuhumu viongozi wawili waandamizi wa chama hicho Khassan Doyo na Amir Kirungi kuzunguka wilaya zote nchini bila kuzijulisha mamlaka za chama zilizowekwa kikatiba na kuhamasisha wanachama wake wakihame chama.


  My take:


  1. Inawezekana Maalim Seif anatumia nafasi aliyonayo katika serikali ya umoja wa kitaifa (SUK) kutoa agizo/ushawishi kwa vyombo vya dola vya serikali ya CCM (polisi) kumshughulikia hasimu yake HR? Kama ni hivyo hii siyo haki kabisa, kwani ni yaleyale Maalim aliyokuwa akiyapinga huko nyuma, kwa polisi kutumiwa na wanasiasa wa CCM kukishughulikia chama chake.


  2. Penye red: Suala la viongozi wa CUF (au chama chochote cha siasa) kukiuka katiba ya chama linakuwa ni suala la polisi? Inakuwa ni jinai?

  Tafadhalini tujadili hili na tusilete mambo mengine yasiyohusika na mada hii kama vile ya udini nk. Wako wavurugaji humu ndani. Tubakie kwenye mada, please!

  Nawasilisha.


   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Maalimu Seif alishajifia kisiasa siku nyingi.
   
 3. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Tusubiri tuone mwisho wa hii sinema
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Hata mimi linanipa picha hiyo unayosema -- kwamba Maalim anatumia vizuri nafasi yake katika serikali ya CCM kumminya HR. Kwa kweli ni tamthiliya ya kusisimua sana hii inayoendelea na ni ukweli ile methali kwamba kimya kikuu huwa kina mshindo mkuu.
  Tofauti na vyama vingine CUF imekuwa kimya muda mrefu sana tangu ule mgogoro wa James Mapalala. Lakini mie nilihisi tu, kwamba baada ya kufanya hovyo uchaguzi mkuu, na hovyo tena huko Igunga, kamwe CUF isingeendelea kuwa kimya.

  Tusubiri tu mshindo wake.
   
 5. k

  kkitabu Senior Member

  #5
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hamad Rashid karibu tujenge chadema Pemba. Muache Maalim na CUF yake.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kuna mengi Maalim kisha jifunza kutoka CCM ambayo yuko tayari kuyatumia dhidi ya wale walio tishio kwake katika CUF. CCM wamepata mafanikio sana kwa kutumia polisi wake, na hivyo Seif naye anataka iwe hivyo kwake.
   
 7. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2011
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  usimseme vibaya hivyo maalim s,huyo ni mtume wa mnyaazi mungu
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli inasikitisha sana,sipati picha hii nchi inakwenda wapi kidemokrasia!
   
 9. Bablii

  Bablii Senior Member

  #9
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Another crap thread...

  SUK ipo Zanzibar si Tanganyika, kwa mujibu wa habari yako alotoa ripoti polisi ni Mtatiro (katibu mkuu msaidizi) sio maalim seif, na huyo mtatiro ametoa ripoti kwa polisi wa mikoa ya Tanganyika (uloitaja), Maalim seif na SUK wanaingiaje hapa? Mbona hakuna correlation kati ya hiyo hadithi yako na accusation zako juu ya matumizi ya nafasi yake (maalim) katika SUK dhidi ya Hamad Rashid!

  Hizo zako ni chuki binafsi!
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Another silly response! Acha kutoa povu!!! Kwanza CCM inayotawala Zenji (part of SUK) ni tofauti na CCM ya huku? Au una maana serikali ya CCM ya huku haitambui wadhifa wa Seif katika CCM? Nilimuona Kilwa akihutubia mkutano akiwa na Mkuu wa Mkoa.
  Unafikiri Maalim mwenyewe anaweza kutoa agizo directlyi kwa polisi wa hapa? Lazima atamtumia mtu kama Mtatiro katika kuunganisha, you moron!
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na hapo ndipo hawa CUF wanapenda kutuzuga -- kuhalalisha kwamba bado ni chama cha upinzani huku bara! Wanataka tuamini eti CCM ya kule Zenj haina uhusiano na CCM ya huku Bara!
   
 12. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hamad c aliitwa kwenye kamati ya mahojiano,kumetoka maamuzi gani magumu huko?
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwanza habari za huko Mars. Wote hawajambo?
   
Loading...