Seif al-ISLAM (gadafi's son) yuko wapi?

madukwappa

JF-Expert Member
May 7, 2014
1,888
1,500
Wakuu salaam! Mara ya mwisho mwaka jana huyu mtoto wa pili wa marehemu col. Muamar Gadaffi nilisikia amefutiwa hukumu yake ya kifo kule Libya, baadaye ikasemekana alitolewa gerezani lakini bado ikawa haina uhakika mahali aliko.
Mwanzoni mwa mwezi Mei, 2017 ikasemekana alishambuliwa na wana mgambo wa Libya lakini akanusurika kuuawa.
Inasemekana bado yuko Libya lakini haijulikani yuko libya maeneo gani hasa.
Kuna wengine wanadai bado yupo gereza la Zintan alikofichwa kwa ajili ya usalama wake.
Kama mnavyojua, Seif al Islam ndye mtoto wa pekee wa Ghadafi mwenye elimu kubwa maana ana Phd. Aliyoipata pale London School of Economics mwaka 2007.
Aidha, seif el Islam ni mtoto wa pekee wa Gadafi mwenye ushawishi mkubwa katika 'legacy' ya marehemu Gadafi.

Je, Seif al Islam anaishi wapi hasa?
Je, Seif al Islam atarejea kuiunganisha Libya kurudi katika mstari?
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,200
2,000
Usinikumbushe mitoto ya madikteta ilivyokuwa na nyodo; walikuwa na uwezo wa kuwabaka wadada warembo and thereafter kuwachinja live at their pleasure bila kuhojiwa na yeyote yule - Uday na Qusay wa Saddam Hussein hao. Inshaallah, Mwenyezi Mungu atusaidie enzi za madikteta zitokomee mbali huko.
 

Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
4,447
2,000
Kwasasa kuna Mazungumzo yanaendelea katika pande za makabira yanayosigana huko Libya, mazungumzo hayo yatasaidia kuteua kiongozi Mpya wa kuiongoza Libya, inasemekana mpaka sasa US wanaona walifanya kosa kubwa na hivyo wanashauriana Saif achukue serikali aunde ile nchi upya, bado analindwa huko Zintan na taarifa za uhakika kutoka kwa Dr Moussa Ibrahim ambaye nafahamiana nae in person huyu bwana atateuliwa kuiongoza Libya baada ya haya Mazungumzo..haitakua kazi rahisi kwake kuijenga nchi ile ila kwa kuwa jina la Ghadaf bado linaheshimika sana Libya tukiacha ile propaganda ya uzushi ya US na wenzie manake ataweza kuiweka sawa ile nchi...Mungu awasaidie na kwa kuwa cha moto walishakiona manake wataheshimu utawala wa Saif...
 

madukwappa

JF-Expert Member
May 7, 2014
1,888
1,500
Aseh, hata mi natamani sana jamaa achukue dola, nilikuwa napitia historia yake hapa na mchango wake wa kimaendeleo utawala wa marehemu ghadafi.. Kiukweli yuko vizuri, kama ndivyo basi itakuwa hatua nzuri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom