Elections 2010 Seif achukua fomu za kugombea tena CUF, akemea ving'ang'anizi wa madaraka

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
263
13
Sultan Seif Sharrif Hamad ameshachukua fomu za kugombea tena nafasi ya katibu mkuu wa CUF. Lipumba yeye amesema ataamua wiki moja kabla ya uchaguzi wa chama hicho ili kutowatisha wanachama wengine kuchukua fomu na kugombea.

Sambamba na hilo Seif ametangaza kuwa atagombea tena kwa mara ya nne urais wa Zanzibar. Mwenzie Lipumba bado hasema chochote kuhusu kugombea Urais mwaka 2010.

Akichukua fomu hizo mjini Zanzibar, Seif amewakemea viongozi waafrika kwa kuwa ving'ang'anizi wa madaraka kwa kumnyima uongozi kila aliposhinda Zanzibar mwakaa 95, 00, 05.

.....ndiyohiyo
 
Sasa hapa nani king'ang'anizi? na yeye si angewaachia damu changa ndani ya CUF? I thought charity always begins at home!
 
Mimi nadhani Maalim Seif ni viongozi wachache wa Africa ambao wanatakiwa waogopwe sana...

CCM ilishabadilisha kutoka Salim Amour, mpaka Aman Abeid Karume... na 2010 atakuwa pia Mgombea mwingine.

CUF since then 1995 till todate mgombea mmoja ...
 
king'ang'anizi wa madaraka ni yule anayelazimisha madaraka nje ya kanuni na taratibu, sasa kama Seif anafuata kanuni amabazo chama chenyewe cha CUF waliona zinafaa iweje ahesabike anang'ang'ania madaraka?. kudai kuwa CCM wameshabadilisha kutoka Salmin mpaka Karume ni mfano usiofaa, infact Salmin alitaka abadili katiba ili aendelee, seif yeye hajabadili katiba mahali popote pale ya CUF ili kuji'favour' kugombea uraisi. kitu kingine ni kwamba Seif ni big shot, chance ya kuupata uraisi zenji ni kubwa kuliko mtu mwingine atleast kwa sasa, kwa sababu anafahamika vyema.
anyway tuliangalie hili suala kwa uchambuzi akinifu, Seif hajawahi kuwa raisi, na wala hajawahi kubadili katiba ili impe favour, kwa hiyo siyo king'ang'anizi wa madaraka bali ndo kwanza anaweka juhudi ili ayapate hayo madaraka anayoyataka
 
Kauli yako ina walakini, wapo watu wengine ambao wana nafasi kubwa na nzuri kuliko Seif na kama huamini hilo subiri kipigo kingine 2010 tena kutoka CCM tena kwa mtoto mdogo aliyemlea mwenyewe.
'We need change that we can believe'
 
anyway tuliangalie hili suala kwa uchambuzi akinifu, Seif hajawahi kuwa raisi, na wala hajawahi kubadili katiba ili impe favour, kwa hiyo siyo king'ang'anizi wa madaraka bali ndo kwanza anaweka juhudi ili ayapate hayo madaraka anayoyataka

Na hawezi kuyapata-asilan. Ila anaziviza juhudi za CUF. Katika siku za hivi karibuni CUF imeonakana kubadilika na imeanza kuvuta sympathy ya watu katika yale maeneo ambako haikuwa ikukubalika ( Zanzibar Kusini na extreme Kaskazini). Lakini kwa kumrejesha tena Seif agombee -hiyo sympathy itapotea na watu watakuwa na misimamo ile ile ya kuikandia CUF. Angekuwa na busara na angelikuwa kweli anipenda CUF angewaachia wengine safari hii. Kwani mbona wapo tu vijana madhubuti ndani ya CUF.
 
Tatizo hapa mnafananisha fenesi na shelisheli,jamani uongozi wa chama hauna mipaka ,hauna muda,hauna pingamizi kuwa mtu akishatimiza kukaa katika madaraka ikiwa balozi ,katibu kata au mtungi kwa miaka fulani iwe basi,hilo halipo katika uongozi wa vyama dunia nzima, ondoeni chuki kwa binadamu mwenzenu ,yaani mtu na chama akipendacho,aliishi ccm na uongozi wa juu kabisa na ni kiongozi peke yake ambae aliwahi kuonyesha upinzani ndani ya Chama chake au ndani ya serikali akipingana na viongozi wenzake kwa uwazi kabisa tena kama haitoshi mbele ya Mwalim Nyerere,na kusema kweli Nyerere aliuona ushupavu wa Seif Sharif kwani kabla ya kifo cha Nyerere ,Mwalimu alimwita Seifu Butiama na kumtaka radhi,akimwambia na kumsifu Seif kuwa ni kiongozi wa kweli anaewapenda raia zake.
Seif alisimama mbele ya bunge mbele ya baba wa Taifa la Tanganyika na kumueleza kuwa Zanzibar haitanunua mafuta kutoka Tanganyika kwa fedha za kigeni na ikibidi itatafuta soko liuzalo mafuta kwa bei poa...Jambo ambalo ndilo lilimpandisha hasira Mwalimu ,na kuamua alivyoamua lakini binadamu hukaa na kufikiri na kujuta na Mwalimu Nyerere alikaa na kufikiri na ndipo alipofanya ubinadamu wa kumwita Seif Butiama au hamkumbuki mazungumzo ya private kati ya Mwalimu na Maalim.
Uraisi wa nchi usilinganishwe na uongozi wa chama cha siasa.Kiongozi gani mwengine alietokea kama Seif ndani ya serikali iliyopo ya Tanzania baada ya kifo cha Mwalimu,kiongozi ambae haoni haya kumueleza ukweli mkubwa wake wa kazi ? Zaidi ya kupiga kofi na meza wakionekana wamefurahi kumbe makeke yao nao wamo ndani ya ufisadi.
 
Seif kachemka,

Huwezi kutoa kauli oxymoronic kama hiyo.Kama kweli wewe huamini katika ung'ang'anizi kwa nini hupishi wengine kugombea? Pengine sababu watu ving'ang'anizi wa CCM wanaendelea kuwapo ni kutokana na wananchi kuona hata upinzani nako kuna ving'ang'anizi, hama mabadiliko, kwa hiyo uchaguzi unakuwa tuchague ving'ang'anizi wa CCM au wa CUF? Mwisho wanaona "Zimwi likujualo halikuli likakwisha".

Wapeni watu vijana wachanga wenye mbinu mpya wapambane na hao ving'ang'anizi halafu tuone kama watabaki.

Si umeona "Change We Can Believe In" ya Obama, wangerudi kina Edwards na Kerry nina shaka hata kama wangeweza kumshinda McCain.
 
kama ukisoma vizuri maandishi ya mtoa hoja, unaweza kuona kuwa kuna maana kubwa zaidi imejificha kwenye ujumbe wake.
Lakini for the frth time it will be same story CUF maalim atachaguliwa kuwa Rais, wana CUF watacharazwa viboko na wengine wachache kushughulikiwa na CCM itatawala, mchezo utakuwa uleule.
 
Seif kachemka,

Huwezi kutoa kauli oxymoronic kama hiyo.Kama kweli wewe huamini katika ung'ang'anizi kwa nini hupishi wengine kugombea? Pengine sababu watu ving'ang'anizi wa CCM wanaendelea kuwapo ni kutokana na wananchi kuona hata upinzani nako kuna ving'ang'anizi, hama mabadiliko, kwa hiyo uchaguzi unakuwa tuchague ving'ang'anizi wa CCM au wa CUF? Mwisho wanaona "Zimwi likujualo halikuli likakwisha".

Wapeni watu vijana wachanga wenye mbinu mpya wapambane na hao ving'ang'anizi halafu tuone kama watabaki.

Si umeona "Change We Can Believe In" ya Obama, wangerudi kina Edwards na Kerry nina shaka hata kama wangeweza kumshinda McCain.
Edward si alirudi bana, akashindwa kwenye primaries, Mcain naye alishindwa na Bush kwenye primaries lakini akarudi tena this time,kugombea zaidi ya mara moja kwa mwanasiasa siyo ishu, ishu ni kung'ang'ania madaraka kama Mugabe na Kibaki, au kubadili katiba ili ikupe favor kama Museveni
 
Ushawahi kujiuliza kwa nini wanaorudia rudia wengi wanashindwa?

Halafu Seif siyo tu "zaidi ya mara moja", Seif amekuwa mgombea wa CUF tangu kianzishwe.
 
Sultan Seif Sharrif Hamad ameshachukua fomu za kugombea tena nafasi ya katibu mkuu wa CUF. Lipumba yeye amesema ataamua wiki moja kabla ya uchaguzi wa chama hicho ili kutowatisha wanachama wengine kuchukua fomu na kugombea.

Sambamba na hilo Seif ametangaza kuwa atagombea tena kwa mara ya nne urais wa Zanzibar. Mwenzie Lipumba bado hasema chochote kuhusu kugombea Urais mwaka 2010.

Akichukua fomu hizo mjini Zanzibar, Seif amewakemea viongozi waafrika kwa kuwa ving'ang'anizi wa madaraka kwa kumnyima uongozi kila aliposhinda Zanzibar mwakaa 95, 00, 05.

.....ndiyohiyo

Seif Hamad akizungumza na vyombo vya habari, alionekana kuwa na haya/soni. Anapotamka "ving'ang'anizi" katika ujumbe wake, inaashiria kujihisi.

Kauli ya Lipumba ina ujumbe mzito. Pengine inaashiria kuna ung'ang'anizi wa madaraka kwenye chama, au mwenendo fulani ambao angepanda ubadilike.

.
 
Sultan Seif Sharrif Hamad ameshachukua fomu za kugombea tena nafasi ya katibu mkuu wa CUF. Lipumba yeye amesema ataamua wiki moja kabla ya uchaguzi wa chama hicho ili kutowatisha wanachama wengine kuchukua fomu na kugombea.

Sambamba na hilo Seif ametangaza kuwa atagombea tena kwa mara ya nne urais wa Zanzibar. Mwenzie Lipumba bado hasema chochote kuhusu kugombea Urais mwaka 2010.

Akichukua fomu hizo mjini Zanzibar, Seif amewakemea viongozi waafrika kwa kuwa ving'ang'anizi wa madaraka kwa kumnyima uongozi kila aliposhinda Zanzibar mwakaa 95, 00, 05.

.....ndiyohiyo

Ha ha ha ama kweli nyani haoni #%$@& yeye anayeng'ang'ania kugombea kila mwaka wa uchaguzi badala ya kuwaachia wanaCUF wengine hajioni!!!!
 
Habari za wakati huu.

Kwanza mfahamu Maalim Seif bado hajatamka kabisa kama atagombea urais 2010 ila alikwenda kuchukua fomu ya ukatibu mkuu wa chama cha CUF.

na kwa mujibu wa katiba ya CUF haijaweka mipaka ya umri au mtu atagombea mara ngapi ukiwa na sifa unachukua fomu na kuomba na baadae mkutano mkuu utakupitisha au kukukataa sasa yeye ametumia nafasi hiyo ya katiba ya chama chake lakini pia mwanachama yeyote anayo haki ya kugombea kama anataka kuchukua fomu na yeye amesisitiza hilo kuwa mwenye kutaka kuchukua fomu achukue bila ya kujali kuwa atapambana na naye kwa sababu kila mwanachama ana haki hiyo, ila kwa kuwa Maalim Seif anaheshimika sana ndio watu wenyewe hujirudisha nyuma na kuacha kuchukua hizo fomu lakini yeye hathubutu kuwakataza kwani kama atafanya hivyo ni kwenda kinyume na katiba ya chama chake.

kuhusu kuwaachia vijana sio vibaya kuwapa nafasi vijana kuongoza au kuchukua nafasi kama hizo lakini mfahamu kuwa vijana wachache ambao wanapopewa nafasi wanaziumia vyema wapo wengi tunawaona walivyokuwa na jazba na hasira na baadae kuharibu mambo na katika siasa za zanzibar hakuna kijana wala mtu mzima ambaye ataweza kutumia busara na hekima kama anavyotumia Maalim Seif jamani jamaa amepewa kipaji si mchezo wewe umeona wapi mtu kuibiwa kura mara tatu tena kwa ushidi vijana wake wanapigwa wanaadhibiwa lakini yeye anawaambia subirini Mungu yupo kwani mkilipiza kisasi mnaweza kuiingiza nchi katika balaa na machafuko. nani anaweza hilo jamani. Maalim mwenyewe ameshafunguliwa kesi akakaa miaka minne anakwenda mahakamani akirudi au hamna kumbukumbu nyinyi.

Maalim hawezi kuacha nafasi maana aliwaahidi watanzania kwamba atawatetea akiwa ndani ya CCM au nje ya CCM atawatetea akiwa ndani ya serikali au nje ya serikali kwa hivyo ahadi hayaitimiza bado mwacheni atimize ahadi yake thena atapumzika.

Issue sio kuwa CUF wakimuweka Maalim watashindwa katika uchaguzi no hata wakichukua mtu ambaye ameletwa kutoka mbinguni kwa CCM kutoa madaraka ni ngumu sana kwa hivyo yeyote atakayekaa madhali sio CCM hashindi kwa maana ya hapewi maana kushinda CUF tokea wakati wa dk salimin inashinda na hakuna hata mtu mmoja ambaye halijui hilo ila kupewa ndio hawapewi na ukiwapata CCM wale wakweli wanakwambia wazi wazi kwamba wao uchaguzi wa zanzibar bila ya wizi CCM hawawezi kushinda kabisa na hilo viongozi wote wa bara wanalijua ila haijafika siku yake tu likadhihirika lakini hakuna lisilo na mwisho kila kitu kina mwisho wake na hilo litajitokeza tu.

mnataka wapewe vijana waanze kupigana mawe kama kenya? nyinyi wacheni mchezo huo wa kitoto mwenye kutaka kuchukua fomu ajiunge na hicho chama na kama mwanachama basi mwache achukue fomu na yeye hajakatazwa.
 
Issue siyo vijana vs wazee, issue ni kuwapa wengine nafasi.Anafanya kama chama chake binafsi?

Zaidi ya hapo anakosa haya na kusema watu wanang'ang'ania wakati yeye ndiye hao hao? seif anashindania urais kila uchaguzi tangu 1995, ina maana hakuna mwingine? Kama wapo wengine kwa nini na yeye asiitwe king'ang'anizi?

Sio lazima ung'ang'anie urais, unaweza kung'ang'ania hata umonita wa darasa.
 
Kilichopo Zanzibar ni siasa za visasi, kwamba kwa vyovyote vile iwe isiwe ni lazima CCM waongoze Zanzibar na kiongozi yoyote atakaye wapa Zanzibar CUF basi ni msaliti. CCM zanzibar hata wakimsimamisha "NYAU" na CUF "BINADAMU" ni Lazima NYAU ashinde kwa kuwa ni CCM.

Na sasa wanabuni mradi wa electronic voting ndiyo kabisa one click, CCM Bingwa. Ili CCM Zanzibar ishindwe ni lazima wanzibar waungane kwa pamoja bila kujali itikadi yao na kuishutumu Bara, hapo ndiyo CCM itakuwa imefikia mwisha Zanzibar.

Ceteris Paribus, uchaguzi Zanzibar ni "Ze Comedi" ya kisiasa kuionesha Dunia kuwa nao wanafanya uchaguzi ila ile nchi ni ya kisultan na sultani wake ni CCM mwenye watoto wanachama wa CCM Zanzibar ambao ni warithi wa uongozi mmoja baada ya mwingine
 
Idadi ya wapiga kura huko Pemba na Mji Mkongwe ni wengi sana kuliko wa Ng'ambo na sehemu zingine za Unguja?
 
Ushawahi kujiuliza kwa nini wanaorudia rudia wengi wanashindwa?

Halafu Seif siyo tu "zaidi ya mara moja", Seif amekuwa mgombea wa CUF tangu kianzishwe.

Kushindwa kwao siyo kwa sababu wanarudia mara nyingi, bali ni kwa sababu wananchi hawakuwachagua au yes kuna wengine wanashinda lakini wanaletewa mizengwe. lakini vile vile wapo wengi wanaorudia na hatimaye kushinda, George Bush Senior aligombea kwenye primaries akashindwa na Reagan miaka minane baadaye akashinda primaries, Mwai Kibaki pamoja na kujitia doa hapa juzi aligombea mara kibao dhidi ya Moi lakini hatimaye akashinda.
ni lazima tutofautishe dhana mbili " kuyatafuta madaraka" na "kung'ang'ania madaraka", utang'ang'aniaje kitu ambacho huna?.

au kuweni specific kwamba Seif anang'ang'ania kugombea, lakini nalo siyo kosa kwa sababu kanuni na sheria na taratibu hazijakataza mtu kugombea mara nyingi, ni part ya demokrasia hiyo, kama mtu ana ubavu si ajitokeze amchallenge Seif katika vikao vya vyama ili achaguliwe yeye?
 
au kuweni specific kwamba Seif anang'ang'ania kugombea, lakini nalo siyo kosa kwa sababu kanuni na sheria na taratibu hazijakataza mtu kugombea mara nyingi, ni part ya demokrasia hiyo,

Na hao anaosema wanang'ang'ania je wanavunja kanuni ama taratibu zao ? Je kuna kanuni iliyomzuia Mugabe kugombea na akaivunja ? Ninavyoelewa ni kuwa wanang'ang'ania kwa sababu kanuni, sheria na taratibu zao zinaruhusu.
 
Back
Top Bottom