Sehemu zinazopata wapinzani wa nguvu Tanzania zinaadhibiwa kwa kunyimwa maendeleo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,347
Mikoa ya Kusini ilimtoa mpinzani wa kweli, aliyepinga siasa za Ujamaa na Kujitegemea, Marehemu Oscar Kambona R.I.P. Kambona alipinga waziwazi ujio wa sera za ujamaa. Matokeo yake aliishia kuwa mkimbizi Uingereza. Mikoa ya kusini iliadhibiwa kwa makosa ya Kambona.

Kusini kuna idadi kubwa ya wasiojua kusoma na kuandika. Hii inapelekea wengi kuchaguliwa viongozi wakati wa kupiga kura kwani wanahitaji msaada. Hili tatizo la high illiteracy level Kusini liangaliwe mara mbili. Linachangia kuzorota kwa maendeleo. Watoto kuachishwa shule na kuchezwa unyago.

Rufiji ilimzalisha mpinzani machachari Mwana mama Bi Titi Mohamed. Huyu alikuja enzi za Chama Kushika Hatamu, Njia pekee ya kushindana na chama tawala ilikuwa ni kwa jaribio la kupindua serikali. Hili kosa lilighrimu safari ya Bi Titi kisiasa na maendeleoya Rufiji.

Watu wa Kawe wamebahatika kumpata mbunge imara, Halima Mdee, bahati mbaya hatokei chama tawala. Hii imewagharimu wana Kawe kupata barabara zenye hadhi la eneo lao.

Tatizo la maji Singida Mashariki lilifahamika kwa muda mrefu. Kosa lao mbunge wao alikuwa Tundu Lissu ambae hatokei Chama Tawala.

Ili tupate maendeleo ni lazima tuchague wabunge wa chama tawala? Tutajuaje Kama huyu mgombea wetu sisi chama chake hakitashinda uchaguzi huu?
 
Je Arusha,Iringa,Mbeya kunaongozwa na wabunge wa chama tawala mbona kuna maendeleo chini ya wabunge wa upinzani.
Maendeleo ya Mbeya Ni jitihada za Wana Mbeya wenyewe.

Serikali kuanzia ya awamu ya kwanza ilikusahau Mbeya.

Shule za serikali zilizoko Mbeya Mjini ni tatu tu Mpaka Kikwete anaingia madarakani, Iyunga, Loleza, na Mbeya Secondary.

Lakini shule binafsi za Wana Mbeya zilikuwa lukuki na kusambaa kila Kona.

Mbeya Referral Hospital haijajengwa na serikali ya Tanzania 🇹🇿, imejengwa kwa msaada wa malkia.

Uwanja wa Sokoine / Uwanja wa MAPINDUZI ulijengwa na wananchi wa Mbeya bila mchango wa serikali.
 
Hahaha maendeleo gani tena? Kwani kuna sehemu yoyote Tanzania hii iliyoendelea?!
Hayo maendeleo yanayopelekwa huko, hutoka wapi?!

Kwasasa Tundu Lisu kesha fika, tusubiri akipitishwa kugombea , basi uzi wako uufute, maana utapingana na kauli ya Chadema ya maendeleo kwa wote.

Au vipi Chadema nao watafanya hayo?!
 
Mifano yako hailingani na Hali halisi. Dodoma tangu enzi Ni CCM Tena usipime. Umasikini Ni wa kiwango Cha bomu la nyuklia. Watu wake Ni masikini wa kutupwa na wanaongoza kwa ombaomba. Kusini wameng'ang'ania CCM ona matokeo yake, wamenyang'anywa korosho wasemaji wa kuwatetea wslifyata baada kutishiwa mashangazi wao kuchapwa. Sauti ya kuwasemea hakuna sababu tu CCM.

Kaskazini usipime, maendeleo kila Kona. Hawalii njaa, miundombinu ya barabara imeboreka na huduma za kijamii shule na mahospitali Zina Hali nzuri.

Wewe endelea kukumbatia ujinga na hiyo CCM yenu mnatumika Kama mpira wa ....
 
Maendeleo ya kaskazini ni yapi ? Mbona tunaona wamasai wa Monduli, Longido na Ngorongoro wakiishi kama enzi za ujima. Aidha barabara nyingi za kwenda milinani huko Same, Mwanga, Moshi vijini na Rombo ni shida wakati wa mvua maana ni tope la udongo wa mfinyanzi kila mahali. Sasa hayo maendeleo unayotaka kuwadanganya watanzania ni yapi ?
Mifano yako hailingani na Hali halisi. Dodoma tangu enzi Ni CCM Tena usipime. Umasikini Ni wa kiwango Cha bomu la nyuklia. Watu wake Ni masikini wa kutupwa na wanaongoza kwa ombaomba. Kusini wameng'ang'ania CCM ona matokeo yake, wamenyang'anywa korosho wasemaji wa kuwatetea wslifyata baada kutishiwa mashangazi wao kuchapwa. Sauti ya kuwasemea hakuna sababu tu CCM.
Kaskazini usipime, maendeleo kila Kona. Hawalii njaa, miundombinu ya barabara imeboreka na huduma za kijamii shule na mahospitali Zina Hali nzuri.
Wewe endelea kukumbatia ujinga na hiyo CCM yenu mnatumika Kama mpira wa ...............
 
Wagogo siyo maskini, kila familua wana ng'ombe, tabia yabkuomba ni jadi tu wala siyo umaskini
Mifano yako hailingani na Hali halisi. Dodoma tangu enzi Ni CCM Tena usipime. Umasikini Ni wa kiwango Cha bomu la nyuklia. Watu wake Ni masikini wa kutupwa na wanaongoza kwa ombaomba. Kusini wameng'ang'ania CCM ona matokeo yake, wamenyang'anywa korosho wasemaji wa kuwatetea wslifyata baada kutishiwa mashangazi wao kuchapwa. Sauti ya kuwasemea hakuna sababu tu CCM.
Kaskazini usipime, maendeleo kila Kona. Hawalii njaa, miundombinu ya barabara imeboreka na huduma za kijamii shule na mahospitali Zina Hali nzuri.
Wewe endelea kukumbatia ujinga na hiyo CCM yenu mnatumika Kama mpira wa ...............
 
Acha stori za kutunga we umetembelea Dodoma ukaona umaskini uliopo kule au umeenda Bukoba vijijin watu wanakunywa maji ya vumbi....wapinzani wengi wanaongoza Bukoba Mjini / kila kitu kimependeza ni ujinga tu wa mtoa mada.
 
Nitajie majimbo ya ccm yenye maendeleo sanasana huko vijijini tunawaona wanakunywa maji ya chooni yenye vyura ITV kila siku wanaonesha, au angalia Ukonga kwa waitara Barabara zimejaa mbavu za Mbwa.
 
Nitajie majimbo ya ccm yenye maendeleo sanasana huko vijijini tunawaona wanakunywa maji ya chooni yenye vyura ITV kila siku wanaonesha, au angalia Ukonga kwa waitara Barabara zimejaa mbavu za Mbwa.
Chato
 
Maendeleo ya Mbeya Ni jitihada za Wana Mbeya wenyewe.
Serikali kuanzia ya awamu ya kwanza ilikusahau Mbeya.
Shule za serikali zilizoko Mbeya Mjini ni tatu tu Mpaka Kikwete anaingia madarakani, Iyunga, Loleza, na Mbeya Secondary.
Lakini shule binafsi za Wana Mbeya zilikuwa lukuki na kusambaa kila Kona.
Mbeya Referral Hospital haijajengwa na serikali ya Tanzania 🇹🇿, imejengwa kwa msaada wa malkia.
Uwanja wa Sokoine / Uwanja wa MAPINDUZI ulijengwa na wananchi wa Mbeya bila mchango wa serikali.
Duh! kwa hizi data umetisha kamanda.
umenikumbusha CHADEMA ileee! kabla akina Lisu hawajanunuliwa na Lowasa.
 
wapinzani wengi wa kiafrika wamejenga dhana ya uadui kwa serikali coz wanazihujumu nchi zao kwa kutumika na mabeberu na hii ndo sababu kubwa ya kutengwa na serikali nyakati zote...

tizama wapinzani wa nchi za wenzetu ni wazalendo na wapo ajili ya kuzijenga nchi zao tofauti na wapinzani wa kiafrika ambao wanatumikia matakwa ya wazungu

hata leo wapinzani wa kiafrika wakiacha unafiki wa kutumika na wazungu nadhani maendeleo yatakua ya kasi kubwa sana afrika.

vyama pinzani afrika ni miongoni mwa vikwazo vya kuendelea kiuchumi coz kazi yao kubwa ni kupinga na kukoso tu as wao ni parfect mno.

kwa haya tuacheni ushabiki wa vyama ili tuwakumbushe wapinzani kua upinzani si uadui.
 
Uko very reasonable kwenye post zako nyingi. Kwenye hii hujafanya research nzuri, then very unreasonable jump!
Ground theories, quantitatively, qualitatively: Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Arusha zinaongoza sana kwa Upinzani Tanzania, na ndiyo mikoa yenye maendeleo chanya na ki elimu. Kusini Mtwara, Lindi na Ruvuma wako nyuma based in culture and religional social affiliation zaidi.
 
Siyo kweli nyie watu wa kusini ni wavivu sana, mbona Mangi mkuu alitaka kaskazini ijitenge na iwe nchi inayojitegemea na maendeleo yalipatikana? fanyeni kazi acheni uvivu hakuna serikali itakayo kuletea maendeleo kama wewe huwezi kujiletea.
 
Labda kuna ukweli, juzi kati nilikuwa Mkoa wa Kilimanajaro kusema ukweli umesimama kabisa kimaendeleao na tayari umeshapitwa na Mikoa mingi tu Tanzania, hiyo Barabara ya Moshi-Dar imechuja kabisa ni kama unatoka kijiji kimoja kwenda kingine mpaka ufike Pwani ndiyo uchangamfu unaanza tofauti na zamani trafic ni ndogo sana.

Sasa hivi mambo yote ni central region, nyanda za juu na Kaskazini, ukipita huko barabara zimejaa, shughuli za kimaendeleo ni nyingi sana, mimi mwenyewe nilijiuliza kwa nini kwa mfano Arusha City imefubaa hivyo? Sasa hivi Arusha hakuna tena kitu hata AICC kwisha sababu walijenga Ukumbi wa Kimataifa Dar ambao kwa maoni yangu lilikuwa ni kosa, kwani Arusha City ilikuwa inaponea hapo

Shule za Kimataifa za gharama zinafungwa maana yake i kwamba wenye uwezo wa kulipia hizo ada wameisha, hivyo sijui kama ni kweli wanaadhibiwa kama unavyosema lkn ukweli ni kwamba mkoa wa Kilimanjaro umesimama kimaendeleo kabisa na umeshafikiwa/pitwa na Mikoa mingine, lkn pia mbona Iringa City iko vibrant wakati ina Mbunge wa chadema siyo dead City kama Moshi, kwa nini Iringa City, haijaadhibiwa'' kama unavyosema ni kweli? ...
 
Back
Top Bottom