Sehemu zenye wafanyakazi wengi wa nje wenye sifa sawa au pungufu ya zile za wazawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sehemu zenye wafanyakazi wengi wa nje wenye sifa sawa au pungufu ya zile za wazawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Chona, Jun 19, 2012.

 1. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 512
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko kuwa baadhi ya makampuni, NGO, Mashule, Taasisi, Viwanda na sehemu zingine za kazi kumekuwa na ongezekeo kubwa la wafanyakazi wa Kigeni, hali inayoashiria kuwa nafasi nyingi ambazo zingeweza kukaliwa na wazawa na kupunguza tatizo la ajira sasa zinakaliwa na wageni toka nje ya nchi.

  Lakini malalamiko hayo yamekuwa na msingi mkubwa kuwa watu hao wanaohudumu kwenye nafasi hizo wengi wanasifa ambazo watanzania wengi wanazo. Wengine wameenda mbali zaidi na kueleza kuwa wafanyakazi wengine wa kigeni wana sifa ambazo zipo chini ya zile walizonao watanzania.

  Lakini pia kumekuwa na manunguniko kuwa viwanda vingi vinavyomilikiwa na wahindi vimekuwa na idadi kubwa ya wahindi wanaeletwa toka Hindia na kuja kufanya kazi ambazo zingeweza kufanywa na watanzania. Imeripotiwa kuwa wengine wanaishi kwenye magodown ili wasionekane mitaani na hivyo kuhalibu deal.

  Tatizo lingine limekuwa ni kwenye payment inayofanywa baina ya hao watu toka nje na wale wa tanzania. Fununu zinasema kuwa wengi wanalipwa mishahara mikubwa ila amount zao hazipiti kwenye pay roll.
  Unakuta kwenye pay roll analipwa mshahara wa kawaida ila malipo mengine yanafanywa nje ya pay roll, kwamba anapewa fungu lingine kwenye bahasha. Na hii imekuwa ikifanywa ili kutozua manunguniko na molali ya kufanya kazi kwa watu wengine. Lakini pia kama hii inafanyika basi serikali inapoteza mapato kwa kutokata kodi kwenye hayo malipo mengine.

  Sasa basi maadamu hapa tunao watu wa kada mbalimbali ambao pengine wanaweza kushughulikia tatizo hili likapungua kama sio kuisha na pengine wao si rahisi kujua ujanja wote na mahali walipo hao watu. Nichukue fursa hii kukuomba wewe mtanzania mwenzangu ambaye kweli unaona ndugu zetu wanakosa nafasi za kazi wakati wanazosifa ambazo zinawawezesha kufanya kazi zinazofanywa na hao wanaoitwa wataalam (expert/ specialist fake)kwenye hizo sehemu ututajei mahali na idadi ambayo unahifahamu ya hao wafanyakazi wa kigeni wanao chukua ajira za ndugu zetu. Na hapa tuwe wazi tusiweke hisia zetu mbele tukasingizia tu, kiukweli zipo kazi ambazo bado tunahitaji wataalam toka nje.
  Lakini kwavile sisi ndo tunafanya nao kazi au tunaishi nao na tunajua taaluma yao ni dhahili kuwa tunajua kuwa huyo kweli utalaam wake unahitajika pale au utaalamu alio nao wapo wenzetu ambao wanaweza kufanya hizo kazi anazo fanya bila wasiwasi. Na hivyo yeye hastahili kuwepo mahali pale maana anaziba nafasi ya wenzetu.
  Uzi huu nataka uwafungue macho watu wa Wizara ya Kazi na Ajira wajue sehemu za kufuatilia working permit za watu na walizitoaje wakati kazi hizo zinaweza kufanywa na watu wetu. Lakini pia itasaidia Mmalaka ya uhamiaji maana nao imekuwa inalaumiwa kwa kutoa permit kama njungu. Mwisho Polisi na watajua sehemu za kufuatilia ili tulinde soko la ajira la ndugu zetu.

  Angalizo kuna watu huwa wanasema kuwa watanzania hawajitumi na hivyo upelekea watu kuajili watu wasiokuwa watanzania, nasema hapa si mahali pake pa kujadili hilo. Wengi wanakatishwa tamaa na tofauti ya malipo inayofanywa baina yao na wageni ingawa kazi ni zile zile. Tutajadili siku nyingine hilo. Tunahitaji kujua mahali ambapo hao wafanya kazi wa kigeni wamejificha au kufichwa kwa kisingizio cha kufanya kazi wakati hizo kazi zinaweza kufanywa na wazawa. Tuwafuchue, tufichue hizo sehemu zijulikane hili mwisho wasiku tulaumu vyombo vyetu kwa kukaa kimya bila kuchukua hatau kama tutakuwa tumewaorodhoshea hizo sehemu.
  Karibu kwa kutaja sehemu husika.

  Mpaka sana tuna list hii

  1. Odysei Internation Casino
  2. Legrand Casino
  3. Kilimanjaro Kempinsk Hotel
  4. Palm Beach Hotel
  5. Sea Cliff casino
  6. Future Group - Regent Estate. Intl Health NGO
  7. Ifakara Health Institute Research More Kenyans are hiding on false Tanzanian names n receive good posts and salary
  8. Imma World health- Regent estate
  9. Quality Group of companies- A lot of Indians imported on daily basis to work for Manjistu
  10. KCB
  11. Uchumi Bank- Kenyans are too many
  12. Barclays- Senior management and High post are exclusive for foreigners
  13. Banc ABC- To many Zambians,ZIM, Ghanians
  14. Delloitte & Touch Tz Ltd - Too many Kenyans
  15. African Barrick Gold- Buzwagi,North Mara,Bulyanhulu,Tulawaka- Too many South Africans who to some extent have not gone to school.
  16. Paradise Group of Companies- Too many SOmalis as we know they hv diverted form schools.
  17. Alliance One Tobacco T ltd. Morogoro- To many Foreigners on senior positions.
  18. Tanzania Road Haulage TRH.- Too many unnecessary indians
  19. Air Tel- Scouting too many ponjoros now on
  20. Jambo plastic- uki tokea tazara kama una kwenda uwanja wa ndege wapo wengi
  21. Tanzanite One wapo wengi sana toka nchi ya Nepel wanafanya kazi za ulinzi
  22. Kempinsik hotel kuna wafilipino wengi tu
  23. Viwanda vya karatasi maeneo ya mbozi road wameajili wakenya wengi tu
  24. Grumeti Reserves - Nafasi zote za juu zimeshikwa na waKenya + South Africa.
  25. Bonite Bottles - waIndi wamejazana utafikiri umeingia Punjap
  26. Serena Hotels - WaKenya wamejazana kama Nakuru utashagaa hata nafasi za wafagizi wanatoka Kenya.
  27. Mt Meru Petroleum - WaIndi ni wengi.Wapo waIndi wasioruhusiwa kutoka nje hawajui Arusha ina mvua au jua.
  28. TANELEC Nafasi zote za juu zimeshikwa na waKenya.
   
 2. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,093
  Likes Received: 1,477
  Trophy Points: 280
  tembelea New Africa Casino asilimia kubwa ya wafanyakazi ni watanzania lakini tembelea Casino za Odysei Internation wanamiliki Casino za Legrand,Kilimanjaro Kempinsk,Palm Beach na Sea Cliff casino kuna wafanyakazi wengi wa kigeni wanaofanya kazi hizo hizo ambazo New Africa Casino zinafanywa na watanzania.Uhamiaji wanajua,Bahati Nasibu wanajua lakini kinachofanyika wanapokuja kufanya msako hao watu wanafichwa kabla kwa maana nyingine wanapewa taarifa,nenda mahotel ya kitalii nenda kwenye recruitment agency wamejaa wakenya nenda kariakoo utakuta wasomali wamejaa wakichukuya nafasi za kitanzania orodha ni ndefu sana
   
 3. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 512
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Mkuu nashukuru kwa kutaja hizo sehemu ulizotaja kama Casino za Odysei Internation, Casino za Legrand, Kilimanjaro Kempinsk,Palm Beach na Sea Cliff casino.

  Hapo kwenye red ninataka kukumbusha kuwa lengo ni kujua hizo sehemu, hivyo itakuwa ni busara zaidi kama utazitaja kwa majina ili zifahamike kuliko ku generalize.
  Asante sana.
   
 4. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Future Group - Regent Estate. Intl Health NGO.
  Ifakara Health Institute Research- More Kenyans are hiding on false Tanzanian names n receive good posts and salary.
  Imma World health- Regent estate
  Quality Group of companies- A lot of Indians imported on daily basis to work for Manjistu.
  KCB- Onyangos are too many
  Uchumi Bank- Kenyans are too many
  Barclays- Senior management and High post are exclusive for foreigners
  Banc ABC- To many Zambians,ZIM, Ghanians
  Delloitte & Touch Tz Ltd - Too many Kenyans
  African Barrick Gold- Buzwagi,North Mara,Bulyanhulu,Tulawaka- Too many South Africans who to some extent have not gone to school.
  Paradise Group of Companies- Too many SOmalis as we know they hv diverted form schools.
  Alliance One Tobacco T ltd. Morogoro- To many Foreigners on senior positions.
  Tanzania Road Haulage TRH.- Too many unnecessary indians
  Air Tel- Scouting too many ponjoros now on
   
 5. Gele vaheke

  Gele vaheke Senior Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Daa kwanza nianze kwa kukupongeza kwa kuona hili nimepoteza fedha nyingi kwa ajili ya vitu wanavyo hitaji badala ya kupata kazi mwisho wa siku napata pesa ambayo hai kizi hata kunywa maziwa tu kutokana na mazara nayo pata kiwandani niliamua kuacha kazi na kuludi kijijini na kujishugulisha na kilimo tu. halafu una kuta mfanyakazi wa kihindi ametulia tu hana kazi yeyote wakati mmepangwa mashine moja kweli ina uma sana hawa jamaa wana tuzalau sana tena sana wapo jambo plastic uki tokea tazara kama una kwenda uwanja wa ndege wapo wengi pia hawana kazi asante
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naomba kujua ukishatajiwa hayo maeneo what next?
   
 7. M

  Mzee Kabwanga Member

  #7
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tanzanite One wapo wengi sana toka nchi ya Nepel wanafanya kazi za ulinzi hivi Tanzania hakuna watu wanaweza kufanya kazi za ulinzi . Mining wapo wengi sana . Nchi imekuwa jalala la wageni.
   
 8. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazeni buti,ipo siku mtafanikiwa!
   
 9. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,093
  Likes Received: 1,477
  Trophy Points: 280
  kampuni ya TRl nina rafiki yangu Mhindi lakini ni mhindi kwa asili ila ni mtanzania kwa kuzaliwa alinijulisha juu ya kampuni hiyo kuajili inspector attendant kutoka india kazi ambayo inawezwa kufanywa na watanzania hata wa form four Kempinsik hotel kuna wafilipino wengi tu wamejazana,kuna viwanda vya karatasi maeneo ya mbozi road wameajili wakenya wengi tu na hata Rais wakati anagombea mara ya kwanza alizungumzia hili swala kuwa hotel za Arusha alikuwa anahudumiwa na wakenya kwa kazi zinazoweza kufanywa na watanzania pamoja na kulionatatizo hilo bado hajachukua hatua yoyote
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  [1] Grumeti Reserves - Nafasi zote za juu zimeshikwa na waKenya + South Africa.

  [2] Bonite Bottles - waIndi wamejazana utafikiri umeingia Punjap.

  [3] Serena Hotels - WaKenya wamejazana kama Nakuru utashagaa hata nafasi za wafagizi wanatoka Kenya.

  [4] Mt Meru Petroleum - WaIndi ni wengi maofisa uhamiaji wanachota fedha za kutosha kila mwezi.Wapo waIndi wasioruhusiwa kutoka nje hawajui Arusha ina mvua au jua.

  [5] TANELEC Nafasi zote za juu zimeshikwa na waKenya.
   
 11. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 512
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Nimeeleza vizuri kwenye maelezo yangu hapo juu.
  Lakini pia unayo nafasi ya kuongeza ni nini unadhani kifanyike ili kuondoa tatizo hili.
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hili suala ni obvious nchi nzima kila kona watu wasio na vibali vya kufanya kazi wapo tuu.
  Nijuavyo expert wanatakiwa kuwa watano tuu labda kama sheria imebadilika.
  Kama wewe ni mhusika na upo Tanzania hili suala ni la kufanya follow up tuu!
  Mbaya zaidi wanaajiri watu ambao Tz wapo tena competent zaidi yao imagine mtu ana diploma kisa mzungu anakuja kuwa HOD wa mtu mwenye degree si uhuni huo!
  Na hawa uhamiaji wanatengeneza sana ela kwa kuwakeep hawa watu Tanzania.Just imagine utitiri wa wachina pale kkoo ivi wote wale wana hati halali za kukaa Tz
   
 13. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 512
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Hizo ndo tunataka uzitaje kwa majina ili kuweka kila kitu wazi.
   
 14. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Walaumu Immigration na wizara ya kazi kwa wafanyakazi wa kawaida na Bank of Tanzania (kwa mabenki hasa senior position ambazo zinakuwa vetted na BoT) hao ndio wanaotoa vibali kwa watu hao! rushwa rushwa rushwa kwa kwenda mbele.
   
 15. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,093
  Likes Received: 1,477
  Trophy Points: 280
  Nini kifanyike?
  Nimewahi kuambiwa kwa kenya watoaji vibali ni mkusanyiko wa wanataaluma tofauti kwa hiyo mgeni yoyote anapoomba kibali wale wanataaluma wanaangalia kama kazi anayoomba hakuna mtu mwenye ujuzi huo.
  Nashauri uhamiaji na wizara ya kazi wasihusike tena na utoaji vibali badala yake kazi hiyo waachiwe jopo la wataalamu wa fani husika ambao watathibitisha kweli hakuna utaalamu huo na pia wafatilie kama sheria inavyosema baada ya kipindi fulani lazima watanzania wapate mafunzo kwa fani husika kwani utoaji vibali umegeuka kuwa chanzo cha mapato yasioyo rasmi kwa idara ya uhamiaji na wizara ya kazi
  Pia waandishi wa habari wasichoke kuwafichua hawa watu kwani baadhi ya waandishi wakipewa habari wanachukua rushwa badala ya kuripoti
  lakini hata upande wa biashara kuna biashara nyingi zinafanywa na wageni ambazo zilitakiwa zifanywe na wazawa tena wale wasio na elimu kama uuzaji maua,viatu,nguo,computer sisi hatuhitaji wachuuzi tunahitaji watu wenye mitaji wawekeze watoe ajira hii ya kumkuta mchina amekaa dukani anauza maua au viatu inaweza kufanywa na mtu yoyote au wasomali wamekaa wanauza part of computer au printing inayofanywa na wapakistani
   
Loading...