Sehemu ya kwanza: Nikiwa Rais wa Jamhuri ya watu wa Tanzania

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Habari Tanzania!

Sifa nzuri na safi ya kuwa Rais wa Tanzania inanogeshwa zaidi endapo unaifahamu ardhi yote ya taifa; haiba za raia; matakwa ya taifa; lengo la maendeleo; ustawi wa jamii na ubora wa maisha ya ndoto za waliowengi.

1. Viwanda

Tutaanzisha viwanda vipya vidogo vyenye tija na uhitaji vya kimapinduzi, kimaarifa na teknolojia kila KATA kwa nchi nzima; visivyopungua viwanda 3; viwanda vitaweza kuchukua nguvu kazi ya watu kuanzia 100 mpaka 300; uwekezaji wake utatugharimu 30 milioni kwa mradi. Hii itachochea uchumi wa moja kwa moja kwa wananchi na ukuzaji wa mapato kwenye halmashauri zetu na kuchochea maendeleo ya miji au vijiji vyetu.

Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira nitaiboresha kwa kuhakikisha wanapatikana maafisa kazi 10 (5 wanawake+ 5wanaume); wasomi wa eneo husika kwa Kata husika; watahusika katika huduma ya taarifa, utawala na usalama kwa watumishi na viwanda tajwa.

Viwanda hivi vitahusisha mafungamano ya wananchi wa Kata, Serikali na Watu au Sekta binafsi katika kuviendesha na kuratibu mambo yote ila sharti litakuwa 50% kwa wote.

Viwanda vitakavyopendekezwa

1. Uzalishaji mayai na Kuku

2. Urembo na mapambo ya nyumba/ binadamu

3. Kilimo cha mboga mboga na matunda

4. Kilimo cha mpunga, ngano na mahindi

5. Utengenezaji vifaa vya umeme wa majumbani na viwandani


Itaendelea........,.
 
Nitatengeneza mambomba ya kutoa maziwa nchi nzima.

Yaani DAWASCO nitaigeuza na Kuipa jina MAZIWASCO.
 
Back
Top Bottom