Sehemu Gani ya mwili wako hucheza kuashiria Kuna tukio linataka kutokea??

Miaka ya nyuma nikiwa napiga mishemishe za porini nikiwa napita njia fulani miguu ikiuma kwa ndani kama inachoma lazima nibadili njia la sivyo huko mbeleni nitakutana na hatari, na ilikua nikibadili tu uelekeo maumivu nayo yanakata.
 
Jicho la kushoto upande wa chini huwa linanipatia viashiria sahihi vya matukio mojawapo kati ya haya yafuatayo.
Msiba, tuhuma, wageni, tukio lisilokuwa la kawaida, mikwaruzano katika mahusiano.
Kiganja cha mkono wa kushoto kikicheza, ama tuseme kuwasha, ni lazima nipate pesa, iwe kwa kulipwa deni, kuuza kitu, kuokota, zawadi nk, ilimradi lazima nipate pesa.
Hiki kiashiria cha kucheza jicho hunikosesha raha kwa kuwa hubeba viashiria vya mambo mengi ambayo mengine hujikuta nipo mikononi mwa polisi.
Viashiria hivi huwa haviongopi, ni lazima viende na tukio moja wapo. Yaani ni lazima.
Imenitokea mwezi huu nasita sana
 
Niambie mimi yafuatayo:
1. Nitakuwa tajiri mkubwa
2. Hakuna mwanamke wa kunikataa

Kiongozi ntakudanganya
Maana hata mimi sijui ilitokea vile.
Uwa najisemea tu.
Ndo maana siku hizi nimeamua kutofanya utani wa mambo ya baadae.
Unaweza ukamwambia mtu kiutani kwamba utaumwa wewe.
Na kesho akaja kuumwa kweli atakuona mchawi.
 
Habari wakuu

Poleni nå majukumu,

Mwili wa mwanadamu una viungo vingi sana, na kila kiungo kina kazi yake, viungo vingine vina kazi zaid ya moja, na vingine tunafaham kuwa vina kazi zaidi ya moja,


Miaka michache iliyopita niligundua macho yangu yanatabia ya kunipa taarifa kwa mambo yanayotaka kutokea Siku chache zijazo, Lakini haikuwa rahisi kugundua, ilifokea karibia weak Nzima jicho la kushoto linacheza, nikawa najiuliza ni nini hii, sikupata jibu, kuna tukio lilitokea na jicho liliacha kucheza siku hiyohiyo, ikapita miezi kadhaa safari macho yote yalikuwa yanacheza na yaliacha pale tukio lilivyotokea
Hivyo tangu siku hiyo niligundua kazi nyingine ya macho yang,

Kuna viungo vinanipa taarifa za haraka, yaani tahaddhari, viungo hivi ni ngozi (vinyweleo) na moyo, viungo hivi ni rafiki sana kwa mwanadamu Maama hutoa taarifa za tahadhali, unaweza kupita sehemu ukajishangaa ngozi inasisimka, na moyo umekuwa na woga, Nawe ukapita kwa tahadali kubwa Mno, ujue kuna kitu kipo ambacho si kizur ila kwa macho hujakiona, kinaweza kikawa kimejificha Ili kisionekane au hakionekani kabisa

Nb kuhusu macho Kutoa taarifa
Si kila tukio, bali ni kwa matukio makubwa tu,

Je, ww ni kiungo gani kinatoa taarifa

Ni biological disorder tu hizo
 
Mi mkono ukiwasha wa kushoto huwa lazima nipate pesa, mwanzo nilitaka kuifanya kuwa
imani potofu, mdomo ukakataa lakini nafsi ikanisuta. Jicho limecheza la kushoto miezi 3
mfululizo sijaona chochote. Ila hapo kwenye mkono ndaani ya wiki tu namba zinasoma.
Kuna kitu chaja
 
Back
Top Bottom