Sehemu gani nzuri ya kuanzia maisha kati ya Dodoma na Babati?

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,305
8,655
Wakuu habari, mimi ni mdau wa maswala ya ujenzi (civil engineer) nataka nifanye maisha ambayo kwa kiasi kikubwa yatakuwa yanahusiana na sekta ya ujenzi.

Je, kati ya Dodoma na Babati ni mji gani utakuwa poa zaidi?

Na je gharama za maisha kwa ujumla zikoje maeneo hayo.

Pia kati ya miji hiyo miwili Fursa za Maendeleo zikoje.

Nakaribisha maoni yenu huenda uzi huu ukawasaidia wengi.

Asanteni.
 
Karibu Babati kamji kanakua kwa kasi na Fursa za ujenz kwasabu babati ipo Center ya Arusha na Dodoma miji mikubwa hiyo
 
Asante sana Mkuu. Kwa fikra za haraka haraka sio rahisi kuamini ilo ila huenda ndio uhalisia!
 
Mkuu kwanini😂😂
Dodoma maisha yako juu sana! Tangu watangaziwe JIJI,mambo yamebadilika mno. Kila kitu bei juu kuanzia nyumba za kupanga, viwanja, nk.

Miuondombinu bado ni ile ile ya enzi za Manispaa! Barabara za mtaani ni mabwawa ya kuvulia samaki na madimbwi tu hasa msimu huu wa mvua! Mimaji ni ya chumvi!! Labda kwa hapo baadae. Ila kwa sasa Dodoma haina kabisa hadhi ya kuitwa JIJI.
 
Daah
 
Mkuu acha uongo bhana
 
Mkuu nakushauri nenda Dodoma. Kama ulivyosema unajihusisha na maswala ya ujenzi nenda huko hutojuta. Kwasasa Jiji la Dodoma lina muingiliano wa watu wengi sana. Hata ukianzisha mgahawa au any opportunity unatoboa mapema tu.

Juzi kidogo nilale nje. Nilipata lodge maeneo ya Town. Asubuhi nikarudisha ile lodge nikijua nitamaliza shughuli Zangu pamoja na kikao mapema then nirudi Zangu Dar. Cha ajabu mambo yalienda Sivyo. Ilipofika saa Kumi na mbili nikaanza kutafuta lodge. We we we weeeee nilizunguk Town nzima vyumba vimejaaa. Ikabidi niende maeneo ya Four way barabara ya Mwanza. Huko ndiko nilikolala
 
Mkuu nakushauri nenda Dodoma. Kama ulivyosema unajihusisha na maswala ya ujenzi nenda huko hutojuta. Kwasasa Jiji la Dodoma lina muingiliano wa watu wengi sana. Hata ukianzisha mgahawa au any opportunity unatoboa mapema tu.

Juzi kidogo nilale nje. Nilipata lodge maeneo ya Town. Asubuhi nikarudisha ile lodge nikijua nitamaliza shughuli Zangu pamoja na kikao mapema then nirudi Zangu Dar. Chaajabu mambo yalienda Sivyo. Ilipofika saa Kumi na mbili nikaanza kutafuta lodge. We we we weeeee nilizunguk Town nzima vyumba vimejaaa. Ikabidi niende maeneo ya Four way bara bara ya mwanza. Huko ndiko nilikolala
Aisee mbona Noma, anyways nitakuja kuzuru mitaa hio ya Dom nione ninaishije. Vipi kuhusu vyumba vya kupanga single.. Bei ya kawaida kabisa kwa Dodoma.
 
Back
Top Bottom