Segerea: Wabunge wa CHADEMA Ester Bulaya, Ester Matiko na Halima Mdee waachiwa. Wasema sasa ni saa ya ukombozi Tanzania

Hiyo iliku
Viongozi watatu; Halima Mdee (Mb), Esther Bulaya (Mb) na Esther Matiko (Mb), wametoka magereza asubuhi ya leo na watazungumza na wanahabari leo katika Ofisi za CHADEMA makao makuu Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Polisi wamewablock viongozi wa CHADEMA Mheshimiwa Halima Mdee, Ester Matiko na Ester Bulaya mda Mfupi baada ya kutoka Gerezani Segerea baada ya kulipa Faini iliyotakiwa na Mahakama.

Watazungumza na Watanzania kupitia waandishi wa habari, saa 5 Asubuhi, leo Alhamis. 12/03/2020, baada ya kutoka gereza la Segerea jijini Dar es salaam.
View attachment 1385386

Hii ndio taarifa mpya kwa sasa

Mungu ibariki Chadema
View attachment 1385509
View attachment 1385553
Hiyo ilikuwa ni slogan ya the famous Mtikila. Saa ya ukombozi ni sasa! Leo hii tena hao akina Halima wanaidandia!

huu ni mwaka wa uchaguzi boss.Kila mbunge anajidai kujitambua.
 
Na wakome! Wajifunze kuwa wazalendo na waache kutumiwa na mabeberu kuvuruga amani ya nchi kwa kisingizio cha Democrasia na wingi wa watu katika kutenda uhalifu wakidhani mkono wa sheria utawaogopa!

Wakirudia wataadhibiwa kwa adhabu kali ili akili ziwakae kichwani! Badala ya kujenga hoja wananchi tuwaelewe wanaazisha vurugu za maandamano?
Tatizo la wazembe hawa, wanadhani kifungo ni mtaji. Sijui kama watamfikia Mtikila. Je alifanikiwa?
 
Huna hoja zaidi ya kutetea siasa za kipuuzi, ruzuku ya chama kutokutumika kuwalipia hao waliohukumiwa kwa uoneve, ndio udhibitisho kuwa inatumika vibaya? Kutokuwa na ofisi yenye hadhi ya cdm hilo ni kweli, lakini mada hii haihusiani na ubora wa ofisi ya cdm. Hii ni dalili kuwa umeishiwa hoja, hivyo unarukia jambo lolote ili kuufanya utetezi wako wa uovu uonekane una hoja za msingi. Sijaanza kujitambua jana wala leo, bali niko vizuri sana kwenye eneo hilo.
Sijashangaa na majibu ya hoja yangu kwa kuwa hujitambui kufuata maneno na matendo ya wanasiasa wachumia tumbo. Watu kama wewe mnatumika kufanikisha agenda na malengo yao.

Karibu viongozi wote waliohukumiwa na kuwekwa gerezani ni wabunge ambao wana mishahara na malupulupu kibao ya kuwwawezesha kulipa faini zao. Kuchangisha ili walipiwe ni mbinu za siasa uchwara huku wakiwaumiza kiuchumi wanachama na wafuasi wao, ambao wamekuwa wakidai Serikali haiwajali, hadi vyuma vimekaza.
 
Sijashangaa na majibu ya hoja yangu kwa kuwa hujitambui kufuata maneno na matendo ya wanasiasa wachumia tumbo. Watu kama wewe mnatumika kufanikisha agenda na malengo yao.

Karibu viongozi wote waliohukumiwa na kuwekwa gerezani ni wabunge ambao wana mishahara na malupulupu kibao ya kuwwawezesha kulipa faini zao. Kuchangisha ili walipiwe ni mbinu za siasa uchwara huku wakiwaumiza kiuchumi wanachama na wafuasi wao, ambao wamekuwa wakidai Serikali haiwajali, hadi vyuma vimekaza.

Kwa hoja hii nimegundua ww una siasa za bendera fuata upepo. Kimsingi hao wabunge wamechangiwa na wapenzi na washabiki wao kwa hiari, na hilo ni jambo la kawaida sana kutokana na hulka za kibinadamu. Hilo halijalishi kama hao wabunge wana mishahara au la. Mbona huko makanisani waumini masikini wanatoa sadaka, huku viongozi wa hayo makanisa wakiwa na hali nzuri kuliko hao waumini watoa sadaka?

Ungelikuwa na hoja iwapo wachangaji wangekuwa wamelazimishwa kufanya hivyo bila ridhaa yao, tena wakipangiwa na kuwango. Hata Nyerere alichangiwa na masikini kwenda kudai uhuru. Hayo ni mambo ya kawaida sana kwenye jamii. Sio mara moja au mbili tunaenda kwenye misiba ya matajiri na tunatoa rambirambi kwa ridhaa yetu. Kwenye harusi pia tunachangia mpaka matajiri, itakuwa hao watu wenye hisia zetu?

Ngoja nikupe ya mwisho ujue kuwa ww ni bendera fuata upepo na huna lolote ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu. Hawa viongozi wetu wote wana mishahara mizuri na vipato vikubwa, lakini wakiugua wote wanatibiwa kwa gharama za kodi za wananchi masikini, kwanini wasijitibu na mishahara yao? Mfano mrahisi Ndugai alienda kutibiwa India, kwa mabilioni ya shilingi kwa fedha za umma, kwani asitoe kwenye mshahara wake, na hiyo pesa wakaenda kutibiwa masikini?
 
Back
Top Bottom