SEDITIOUS: CCM na Nyie Tokeni Nje Bungeni..... Mnadhalilisha Professional Yenu ya U-Kiume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SEDITIOUS: CCM na Nyie Tokeni Nje Bungeni..... Mnadhalilisha Professional Yenu ya U-Kiume

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waberoya, Feb 8, 2012.

 1. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Unajua mkiwa wawili tu mahali fulani, mara ghafla hali ya hewa ya mahali hapo ikachafuka…aliyeichafua lazima atakuwa hana amani maana anajua hakuna mwingine wa kufikiriwa ila ni yeye.

  Kwa hali ya sasa ya nchi inavyoenda hakuna wa kufikiriwa kuwa nani anayumbisha nchi! Hauhitaji kufikiria kuwa nani anasababisha haya, ukifikia hatua ya kufikiria hivyo basi ujue kuwa unahitaji daktari haraka sana…kama atapatikana!

  CCM inajua Kikwete nchi imemshinda, CCM inatambua kuwa Pinda mtu ni sanamu, Pinda halisi hawezi.Lakini katika hali hii ya kuchafua hali ya hewa hivi inawezekana kweli mtu mzima na akili zako , ukakalia mabenchi ya bunge na viti vya maofisini comfortably wakati nchi inakwenda mrama?

  Nauliza hivi, ni lini wabunge wa CCM wanaweza kuamka, hata kama si wote bali wawili au watatu kuwa hawakubaliani na nchi inavyoenda? Ni lini mtawaiga chadema kuonyesha uume(wingi: nyume zenu au mauume yenu), ashakum si matus, ukiume wenu kuwa na nyie mnaweza? Subiri, nauliza hivi, kuwa chama kimoja maana yake kukubaliana katika kila jambo? Kuwa chama kimoja maana yake hamuwezi kusema rais hapa umekosea? Je ni courage gani aliyonayo m'bunge wa CCM nchi hii, anaweza kufanya nini na wapi, kwa maslahi ya nani?

  Nauliza hivi, ni lini wabunge wa CCM wataamka na kusema Kikwete sasa basi!!Msiposema Kikwete hatukutaki tena yeye atasema hawataki kwenye nyadhfa zenu mlizonazo!! Mbaya zaidi hata bunge linaweza kuvunjwa kwa utashi wake. Kikwete atadanganya umma wa watanzania, atabadilisha baraza kana kwamba akifanya hivyo..sukari na mchele vitapungua! Ndiyo uwezo wake, ndiyo nguvu aliyonayo
  Thamani ya binadamu ni nini?

  Thamani ya binadamu ni kuhakikisha binadamu wengine katika sayari hii na hasa mahali unapoishi wanafaidika na kuishi kwako (You have to add value in human life). Ukipata privilege ya kuwa kiongozi ndio haswaa una exercixe your gift that all human are born leader…at the same time una add value katika maisha ya kila siku ya binadamu hapa duniani!


  Thamani ya kiongozi si kuvaa suti nzuri, kuendesha gari nzuri,kula chakula kizuri, kupaya huduma nzuri ya afya na kutembelea posh cars, Thamani ya kiongozi siyo ku-consume resources za dunia hii while you are adding zero!

  Nimeona mbwa Ulaya akila chakula kizuri, akipata huduma za afya superb, tena pengine zaidi ya mawaziri na wabunge wetu, nimeona mbwa akitembea ndani expensive vehicles Tanzania hakuna……nimeona mbwa wakiishi maisha ghali kuliko viongozi wetu… Kwa kifupi no matter ataishi vipi, ATABAKI MBWA TU…

  Kwani kuna tofauti gani ya mbwa wa mfano huu na viongozi wa aina hii?? Tofauti iko wapi?

  Hivi hakuna kati yenu ambaye anaitwa baba nyumbani, akigubikwa na utukufu wa ndevu kidevuni na kutoa koo la mitetemo ya kiume? Hakuna ambaye ana fimbo zinazoshikwa na mayai mawili ya ubaba? Ubaba huu unaonyeshwa wapi na kwenye nini? Kikwete kweli ni wa kuwaendesha kiasi hicho? Yaani anaweza kufanya lolote , kusema lolote, kutaka lolote na mka kaa kimya, simply kwa sababu mnalinda matumbo yenu??

  Hivi Kikwete kwa style hii anaweza kwenda umbali gani kutimiza atakacho?? Hivi ukiwaza mbali si kuwa ana weza kusimama kwenye mimbari mahali fulani akaamlisha kila mtu avue suruali na mkakubali? No sina lengo baya hapa..tuelewane …ni mfano tu, mtu asiwaze vibaya! Japo katika kuwaza vibaya unaweza ukawa sahihi pia!


  Ni hivi…viongozi wa CCM mnatia aibu, mnajidhalilisha nyie na vizazi vyenu, mnadhalilisha professional yenu ya ukiume, mnaboa.

  NB in these paragraphs it has asssumed women are not existing
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuna wabunge wanawake pia je hawa hawamo au neno uume wao (siyo zuri sana)ni inclusive yaani wanawake na wanaume?
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,496
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Maneno mazito sana mkuu Waberoya! Wabunge wengi CCM walipewa ubunge! Fadhila zao ndio hizi "ndiyo mzee!"
   
 4. Pipiro

  Pipiro JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 307
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Sasa kama wamepewa ndio ziwafanye wasijali utu na kukubali kuonekana vituko kwa jamii ? Hivi wanafikiri watabaki kuwa viongozi mpaka wafe ? Ukifadhiliwa ndio ukufanye ukose sauti na kufanya maamuzi sahihi? Unajua hata mtu aliyekufadhili atabaki anakuheshimu iwapo utakuwa na msimamo wako pale atakapokuwa amekosea ila atakudharau atakapokuona huna msimamo unayumbishwa tuu kisa amekubeba....

  Ni kweli kabisa umefika wakati wa kusema enough is enough. They need to do something to rescue the situation which has come from bad to worse. You have a chance to do something NOW than no other time... Utafika wakati wananchi wanaweza kuamua kujichulia vilivyo vyao kama mtashindwa kuwaongoza. Bahati mbaya wanaweza kuanzia kwenu, wakachukua vyao kutoka kwanu na kuyahatarisha maisha yenu. Kumbukeni wananchi watafika mahali watakuwa hawana cha kupoteza. Watakuwa na imani moja tuu kuwa kama wameanguka then wanaogopa nini kudondoka ? Hakuna tofauti hapo.
   
 5. kholo

  kholo JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 411
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu Waberoya, ukistaajabu ya musa utaona ya firaun kwan wahenga walisema 'meno ya mbwa hayaumani' ndugu yangu.
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hakuna tofauti asilani!
   
 7. MANI

  MANI Platinum Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu hayo uyasemayo mazito ingawa yanahitaji tafakuru!
   
 8. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu Waberoya,
  Ni wewe kweli?

  Offtopic kidogo:
  Hiyo quote hapo: Kuna jamaa aliwahi kuchafua hali ya hewa wakiwa wawili tu lakini kila mmoja akawa anamsingizia mwenzie.


  Back to topic:
  Nikuulize swali moja tu mkuu. Kama wabunge wetu ndo hivyo, Rais naye kwa nini asichukue maamuzi magumu? Amepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria ya katiba, wabunge wake wameugomea. Na bado anawachekea tu!

  Na hao wabunge bado wana mawazo ya enzi zileeee......eti maamuzi yote lazima tukubaliane kwanza kwenye chama chetu.
  Walileta mambo ya uccm kwenye majadiliano ya muswada huo sasa yamewageukia....wanajuta kwa nini waliwazomea chadema. Najua kuna wengi walikuwa wanazomea lakini ungemuuliza sababu angekwambia hajui.

  Dhambi ndo hiyo tena inawatafuna.

  Katika hali tuliyonayo sasa, wakulaumiwa ni wananchi.
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0


  Tuendako ni mbali sana. Mtu wa aina hii anapigania haki na usawa Tanzania, wakati hawezi hata kuonyesha usawa katika makala yake yenye aya chache
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ingawa nimekuwa nikitofautiana na wewe hapa kila siku kuhusu vita yako kwa CDM hususan chuki dhidi ya Slaa na Mbowe.Lakini kwa hili mkuu Weborya nakuunga mkono mia kwa mia.Tuko Pamoja.
   
 11. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu Waberoya,

  Nani amfunge paka kengele??
   
 12. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  critical thinking and argurmentation .. (ninawaza naliuza nimemkaa mkao gani nimekaa mkao wakula si unacheki hii sura) ...
  wakiume dhamira zao dhati tumeshazijua hawa nidhamu za uoga zinawachimbia kaburi hawa...
  hojaa imeafikiwa ndiyoooooooooooooo waliosema ndiyo wameshinda kwa hivyo basi hoja imepita bila kupingwa
   
 13. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2012
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  MKUU WAB, hawa wabunge ni zero member F=0N IN truss System DAAH
  kwao uongozi ni ulaji dhamiri zao za ndani ni mfu kabisa utu hawana hawa
  wanatia hasira mnooooo
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Mkuu Waberoya, ukweli ni kuwa wabunge wa CCM wamejipambanua kuwa ni wachumia tumbo, posho kwa kwenda mbele hayo mengine hayawahusu.Mimi naona hapo ni mpango mahsusi wa Mungu kuwapiga upofu hawa manyang'au wajisahau ili wananchi hata wenye uelewa mdogo kiasi gani wawafahamu vizuri wabunge wao na vipaumbele vyao ili ukifika wakati wa kufanya uchaguzi wafanye maamuzi sahihi.
   
 15. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu Wabe umesahau kuwa zaidi ya 80% ya wabunge wa CCM wako pale kwa ajili ya matumbo yao...
   
 16. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #16
  Feb 8, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Taifa linakabiliwa na tatizo kubwa. Lakini kwa bahati mbaya mitazamo ya watu wengi inaelekeza mijadala yao hailengi kutatifiti chanzo cha tatizo hilo. Mimi siamini kuwa iwapo serikali itatekeleza MADAI YOTE ya madaktari, nchi itabaki kuwa na amani. Kitakachotokea ni mlipuko wa kada mbalimbali za utumishi wa umma zikija na madai yanayofanana na ya Madaktari!, madai ambayo kwa kulingana na hali halisi ya uchumi hayatatekelezeka hata km nia itakuwepo. Tatizo Kwa maoni yangu ni HATUA YA WAHESHIMIWA WETU tuliowachagua kutuwakilisha bungeni kutuasi na kuanza kuwakilisha maslahi yao binafsi kiasi cha kujipangia ongezeko kubwa la posho zao, na sababu iliyowapelekea kufanya hivyo, ni hulka zao za kujiona ni tofauti na wanaowawakilisha, na hivyo lazima waishi katika mfumo wa maisha wa kipekee...ili wafikia huko wamelazimika kwa hiari yao, na bila kuwashauri wapigakura wao, kuingia katika mikopo mikubwa ya kibenki ili, pamoja na mambo mengine wanunue mashangingi, ambayo bei zake ni mbaya, wakope benki za biashara wengine tunaambiwa hadi sh. milioni 300, ili kurekebisha 'mambo yake' yafanane na ubunge. Lakini ambacho hawakukijua ama kwa maksudi au kwa kupuuzia tu, ni kwamba mikopo hiyo lazima irejeshwe kwa makato kutokana na mishahara na marupurupu yao; na kweli makato yalipoanza kukatwa wengi wamejikuta fedha wanayobakiwa nayo haikidhi mahitaji yao; na pa kukimbilia ni kutaka posho ziongezwe ili kuziba pengo la kujitakia kwa gharama za wapiga kura kwa raha zao waheshimiwa. Na kibaya zaidi ongezeko la posho hizo wanadai kwa mabavu na kwa kum-blackmail Rais, kuwa asipopitisha watakuwa wanakwamisha kila hoja za serikali zitakazoletwa bungeni. Hali hiyo ndiyo iliyowafungua akili Madaktari na kada nyingine za utumishi wa umma kuwa kama kuna fedha za kubariki matakwa ya wabunge, serikali itakosaje fedha za kutatua madai ya madaktari?, walimu, na sekta nyingine?. Hivyo km si keherehere cha wabunge cha kushinikiza posho mpya hali iliyopo hivi sasa isingekuwepo, ama isingejitokeza kama ilivyojitokeza. Lakini hoja kubwa kuliko zote ambayo wadau wanapaswa kuijadili ni kuwa Hivi kuna uhalali gani kwa mtumishi wa umma anayelipwa mshahara halali kwa kazi aliyeajiriwa kudai posho ya kufanya kazi anayolipwa mshahara kila mwezi...TUJADILI!
   
 17. MANI

  MANI Platinum Member

  #17
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Umenena Mkuu lakini unategemea hio posho ya vikao kufutwa katika serekali hii ?
   
 18. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  viongozi wa bovu huchaguliwa na wananchi wabovu,nyie wenye upeo ukiambiwa kapige kura unasema unamambo mengi ya msingi,sasa mnabaki na forum kulalamika,kaka subiri 2015 tung'oe huu mdudu ccm na utakuwa mwisho wa kudanganyana kama mtoto wa kuku
   
 19. tanira1

  tanira1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu umepiga msumari wa kichwa lakini haya yamelaanika hayasikii matumbo yao yanawadhalilisha mwache hayaburuzee watoto zao heti wanjivunia wana baba eti thubutu!
   
 20. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
   
Loading...