Secretary wa law school of tanzania jamani!!!

Pokola

JF-Expert Member
Jul 16, 2010
716
177
Jamani hizi ofisi zetu zenye uhusiano na serikali zinaajiri watu ambao ni incompetent kabisa, wananchi tunaichukia nchi yetu kwa ajili ya mambo haya. Hebu siku moja jitolee tu uende pale Law School of Tanzania Offices, Ubungo Plaza, umsalimu yule binti (yuko mmoja tu) wa reception kwa ukarimu, kisha pia umwulize swali lolote tu kwa ukarimu pia, kisha uone jibu utakalopokea! Kisha ujiulize kama unaishi katika nchi gani.
 
Nadhani sasa hivi ajira kama hizo zilizo nyingi hasa kwa mabinti hutolewa Guest house.

Kuna ofisi fulani ya mtandao wa simu naifahamu Customer Care yao inaajiri sana watu takriban kila miezi miwili hapakosekani watu kama 30-40 wanapata ajira pale, kuna jamaa wana utilize vilivyo hii opportunity, demu hajatoa penzi hapati nafasi. So ukiona hivyo mkuu utajua tu bosi wake kamweka hapo coz alimtafuna akampa ajira regardless ya elimu yake.

Nenda CRDB nako utashangaa teller wa kike anakukaripia kinoma mpaka unashangaa hivi kwa nini umeweka pesa yako pale, ukichunguza utaambiwa boss flani anapumzika pale, so demu hana wasiwasi wa kupoteza ajira.

Ndo maana hatuendeleiiiii
 
Jamani hizi ofisi zetu zenye uhusiano na serikali zinaajiri watu ambao ni incompetent kabisa, wananchi tunaichukia nchi yetu kwa ajili ya mambo haya. Hebu siku moja jitolee tu uende pale Law School of Tanzania Offices, Ubungo Plaza, umsalimu yule binti (yuko mmoja tu) wa reception kwa ukarimu, kisha pia umwulize swali lolote tu kwa ukarimu pia, kisha uone jibu utakalopokea! Kisha ujiulize kama unaishi katika nchi gani.

Wakenya wataendelea kuchukua ajira zenu mpaka mtakapojirekebisha..............
 
Bado tuna safari ndefu sana.

Katika ofisi zetu nyingi wahudumu wana lugha za nyodo sana. Wengi siyo waungwana kabisa na hawana utu wala staha. Ofisi fulani nilienda nikamkuta mdada mapokezi. Nikaulizia jambo fulani. Dah! Si jibu hilo! Ilibidi nimpe tuisheni kwa upole lakini kwa lugha nzito kwa dakika kama 2 hivi. Uzuri wakati nampa shule huyo mdada, akaja dada mwingine - ambaye alishaona hali yetu si nzuri - akaniuliza shida yangu nikamweleza. Akanisaidia bila shida. Nikaondoka zangu.

Huko maofisini kwa kweli bado kuna shida kubwa ya huduma. Lugha! Lugha! Kauli chafuu!
 
Nenda CRDB nako utashangaa tailor wa kike anakukalipia kinoma mpaka unashangaa hivi kwa nini umeweka pesa yako pale, ukichunguza utaambiwa boss flani anapumzika pale, so demu hana wasiwasi wa kupoteza ajira.

Ndo maana hatuendeleiiiii

Nadhani ulikuwa unamaanisha teller, lakini sio CRDB tu hata benki nyingine wahadumu wa kibri na kisirani cha ajabu. Hata watoto wa kiume nao, sijui labda bongo incompetency ni ugonjwa wa kuambukiza.
 
Nenda CRDB nako utashangaa teller wa kike anakukalipia kinoma mpaka unashangaa hivi kwa nini umeweka pesa yako pale, ukichunguza utaambiwa boss flani anapumzika pale, so demu hana wasiwasi wa kupoteza ajira.

Ndo maana hatuendeleiiiii

Yaani huko ndiko kunani-bore sana. Huko hakuna cha tellers wala accountants. In short professionalism hakuna kabisa Bank ya CRDB.

Kuna wengine wanadiriki hata kusema kuwa ati huyu jamaa anasumbua sana hapa wakati nataka huduma ambayo hata kuielezea hawawezi!. Hivi, ungekaa home kwako nani angekusumbua? Usumbufu wangu ndiyo ajira yako, nieleweshe niondoke na siyo kunifanya nirudi daily.

Hata sijui kama watendaji wakuu wanasomaga hapa JF kuona comments zetu ili ziwasaidie ku-improve?!
 
Nenda EXIM utakoma kabisa, sasa hao watoto wa kiume nao wako humohumo kwa pozi, hadi nasema hii sio bure itakuwa "si rikzi" tu hawa,,, nilienda hamisha pesa yangu yani simple swali anieleweshe; kwanza aliniangalia halafu jibu ikawa "kwani nitaiba pesa yako?" nilimjibu "kumbe mnajijua kwa pesa chafu?"
nshasema pesa yangu mtu asinisumbue itakuwa pesa ya kwaza kuilamba yote kitabuni kumalizia project yangu
shenzy sana
 
lakini tatizo wengine wakienda katika hizo ofisi hawaheshimu watu hasa wa reception jamani watanzania tuna hilo tatizo la kutokuwa heshina kwa baadhi ya kada
 
lakini tatizo wengine wakienda katika hizo ofisi hawaheshimu watu hasa wa reception jamani watanzania tuna hilo tatizo la kutokuwa heshina kwa baadhi ya kada

Umenena vema,tusiwe tunaangalia upande mmoja tu,hilo usemalo kweli lipo...kuna ulimbukeni fulani wa kuona mtu wa reception si chochote si lolote yaani kama vile siyo kazi,watu wanawadharau walio katika kada hii.
 
Ukimheshimu asipokuheshimu muwajibishe. Itasaidia sio kwako tu but hata kwa wenzio wanaokuja. Hili ni jukumu letu wote watanzania si la management flani. Nakumbuka kuna siku nilikwenda pale Kibasila Muhimbili kuna ndugu yangu alikuwa amelazwa akisubiria matibabu. Wagonjwa walikuwa wengi na nesi aliyekuwa mapokezi amekaa pale mlangoni akijipura huku akichat na simu (ilikuwa ni karibu na muda wa yeye kutoka amwachie mwenzie anayeingia zamu ya muda ule lakini alikuwa hajafika bado).

Si hilo lililonshangaza but mbele yake karibu kabisa na mlango kulikuwa na kitanda cha magurudumu chenye mgonjwa (mtoto wa kama miaka 7 hivi) amefunikwa nusu mwili i.e.kichwa na sehemu ya tumbo na mapaja but miguu ilikuwa wazi pamoja na mkono mmoja (ulokuwa na sndano zile za drip kwenye mshipa) mkono huo ulikuwa unaning'inia upande. Haikunichukua muda kutambua kuwa kiumbe yule alikuwa tayari mgeni wa MUNGU muda mrefu.

nikajifanya msamaria,, nikajongea reception nikamsalimia mdada wa watu akaniitikia vizuri tu. Nikamwuliza dada yangu mbona mambo ni vile pale mlangoni? Huyu mgonjwa kwa nini asiingizwe kwenye kitanda chake akapumzika vizuri (nkajifanya sijui kama amefasiki) Akanjibu ameshakufa huyo watakujamwingiza mochwari. Nikashtuka na kumwuliza nani wanakuja kumwingiza akanijibu huyo ajaye kwenye zamu mie nshamaliza muda wangu.

Nikamwomba amsogeze basi maana hata kwa bahati mbaya akatokea mamake au ndugu yake asomjua kama amefariki wawezasababisha kifo kingine. Nikajibiwa mbona wajifanya wajua sana sheria za hospital? Mie muda wangu waisha sasa na hivyo siwezifanya kasi ya mwenzangu. Weeeeeeeeeeeee sikuwa naujua uchungu wa mwana bali nilichomfanyia............aliingia store na kulivaa joho lake na kuitoa ile maiti pale mlangoni. Kifupi ni kuwa nilijivika vyeo na majina yote ya wakubwa wa wizara ya afya na kumjulisha kuwa kesho asubuhi akifika atakuta barua yake mezani kwa bosi wake.

Si nia yangu kueleza haya but nlitaka kusema tu sisi tu watanzania, watu wazima, unapofeel kuwa umekosewa na kunyimwa haki yako toa ushauri kwa upole ili uboreshe huduma.........asipokusikia chukua hatua. Ukikaa kimya si ajabu hata hizo managementi zao hazijui au kwa kuwa kaingizwa na boss ndo aharishie kibarua?? ampelekee dharau alomwajiri sio wateja tena kwa wale wanaofanya kazi sehemu ambazo hata sie tunachangia mishahara yao?? Nehi
 
Nimefurahi sana kukuta hii topic JF, yaani huyu dada anakera, sijui kasoma shule gani? hajui customer care kabisa, hafai kuwa receptionist maana hata kwenye simu anaongea vibaya. how can they employ unqualified person? yaani hata uongee nae vizuri bado atakukwaza tu.
 
lakini tatizo wengine wakienda katika hizo ofisi hawaheshimu watu hasa wa reception jamani watanzania tuna hilo tatizo la kutokuwa heshina kwa baadhi ya kada

Mkuu umesema kweli. Sidhani kama tuna ile tabia ya kuwaheshimu receptionists. Hili linaweza wafanya kuwa defensive wakati wanapodeal na watu. Hata havyo nao wanaweza kuwa wamesababisha hili tatizo. Kama receptionist anajiheshimu, ataheshimiwa na watu pia. Nakumbuka zamani ulikuwa ukienda kwenye maofisi unakutana na ma-secretary waliosomea hiyo fani na walikuwa wanajua wajibu wao. Siku hizi sidhani kama tulionao wamesomea hiyo fani. Wamewekwa tuu na wanaowajua baada ya kushindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali. Kwenye nchi ziloendelea receptionist ndio uso wa kampuni. They can bring in or turn off potential customers.
 
Back
Top Bottom