Elections 2010 SECRET PLOT REVEALED: Kikwete aongoza, Lipumba wa pili, Slaa wa tatu

Njia ya mwongo ni fupi ngoja tusubiri anga za Slaa zitakapoanza kutangazwa ndio tutajua mbivu na mbichi.
 
Mwisho wa ubaya ni fedheha. Waache wajifanye wajanja wanatumia mabavu
 
Alichosema Fareed i'ts absolutely true kwani kuna e-mail nimezinasa kati ya Januari Makamba na msemaji wa mambo ya nje wa cuf zinaashiria yote hayo na lengo ni kuidhoofisha Chadema kisiasa so bado ipo kazi wakuu. Nawasilisha.
 
Acha uongo matokeo yaliyotangazwa na NEC hadi saa 11 jioni ni haya.
Peter Mziray: Kura 4275 = 1.45 %;
Jakaya Kikwete: 186 1877 = 64.2 %;
Dr. Slaa: 578 636 = 19.95 %
Prof. Lipumba: 238 259 = 8.22 %
Mutamwega: 5690 = 0.2 %
Fahmi: 3435 = 0.12 %
Zilizoharibika: 163 562 = 5.64 %

we kweli luteni, kumbe hamjui hata mahesabu, kwenye red mbona figure na % hazifanani? yaani mnachakachua mpaka kwenye JF?
pili, naona mnajiliwaza eti slaa kaibiwa kura wakata tayari mwenyewe ameshajumulisha na anajua fika hata nusu hajafikisha, HIVI NIWAULIZE, KWANI TANZANIA NI KARATU NA MOSHI MJINI TU? kama ndivyo basi slaa kashinda, otherwise hata huko mwambao wote wa bahari wa TZ hakupiga kampeni na wala hakupata kura. watch it.

 
Yaaaaaaah ur right watu walishaliona hilo mapema wameanza kutangaza kule ambako CCM imeshinda ili kuwa demoralize watu kisaikolojia, kule ambako CHADEMA wameshinda hawatangazi ili waeze kucheza na kura na kuchakachua kwani watajua Rais anahitaji kura ngapi ili ashinde, NEC = CCM, na sasa tunataka NEC wajumbe wake wapitishwe na bunge, la sivyo hawafai.
 
Watanzania wa leo si wa kudanganyika hivyo. Huitaji kwenda darasani kutambua kuwa huo ni uhuni wa Bagamoyo. CHADEMA haiwezi kufa unless iongozwe na Lyatonga Mrema.
Watanzania wanajua kuwa CCM wana hila, na huko wanapotupeleka watajuta maana tutaanza na wao kwanza kwa vichapo, seriously tunajua wanakoishi.

Walijaribu mbinu zote wakashindwa, na hii vilevile itashindwa (Zab.23)
 
Usiumie sana, kwani kama wananchi tumetimiza wajibu wetu wa kupiga kura. Kumbuka yuko Mungu, amabye ndiyo mwanzo na mwisho wa kila jambo. Yeye ni Mungu wa haki. Na anasikia vilio vya watanzania, wazima kwa wagonjwa, wenye njaa na walioshiba, n.k. Hivyo kama ameridhia Kikwete awe rais, itakuwa hivyo ila kama hajaridhia it is just a matter of time. Kama unamwamini Mungu endelea kuomba na kuombea uchaguzi maana bado haujaisha.

Wakati mwingine mnamsingizia Mungu kwa kushindwa kutimiza majukumu yenu wenyewe. Mungu alipokupa utashi wa kuelewa jema na baya ni ili uweze kujitegemea na kufanya maamuzi yanayohusu maisha yako ya kila siku. Unapochagua kitu kibovu mwenyewe huku ukijua ni kibovu, au unapokubali kuonewa bila kudai haki yako eti unasema ni "mipango ya Mungu", then ni lazima ukubali kuendelea kuwa mtumwa wa mifumo michafu kama huo wa CCM. You need to stand up for your right, nobody will bring it on your door. Hii culture ya "Ni mipango ya Mungu" ndio imetufikisha hapo tulipo leo, tulitawaliwa kirahisi na wakoloni kwa sababu ilikuwa "mipango ya Mungu", leo Mafisadi wanaipeleka puta nchi kwa sababu ni "mipango ya Mungu", hata umaskini wetu utakwisha siku moja "Mungu akipenda". Duuh! Tuamke jamani kabla jua halijazama.
 
Matokeo ya Kiti cha Urais yanayotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi (nec) yanatia shaka kwa kiwango kikubwa sana. Kwa watu makini na waliofuatilia kwa ukaribu mwenendo wa kampeni, lazima watakuwa wanashangazwa sana kila wanapopata matokeo ya kura za urais yanayotolewa na nec. Ni dhahiri kuwa matokeo ya urais na pengine hata ya viti vya ubunge yamepikwa na ccm na washirika wake ili kukatisha tamaa kabisa nguvu ya umma iliyojidhihirisha maeneo karibu yote ya nchi kwenye mikutano ya chadema wakati wa kampeni. Kinachotushangaza wengi ni kuona kuwa Dr. Slaa anakuwa wa tatu nyuma ya hata Prof. Lipumba.

Ndugu zangu wananchi kama ni kuonewa tumeonewa kiasi cha kutosha na kama ni dharau basi tumedharauliwa kiasi cha kutosha. Viongozi wa chadema na watanzania wote wazalendo mnaoipenda nchi hii kwa dhati lazima tuchukue hatua thabiti kabisa ya kisheria na tupige kelele Dunia yote itusikie mpaka haki itendeke na matakwa ya watanzania yazingatiwe.

Siku zote Mungu hupigania upande wa haki. Kama ni urais mwaka huu, basi kikwete atambue kwamba ataongoza nchi kwa shida na taabu isiyo kifani.
 
Check hii jimbo la Tunduru Kaskazini

Kikwete amepata kura 22,261

Slaa amepata kura 1,965

Lipumba amepata kura 12,935
 
Are you serious? Hao wataalamu naanza kuhisi wanatumia excel program ambayo iko manipulated! i can do it even my self! You know what you get data from various places you feel the way they are but you can manipulate by establishing another column so that it can make deduction of certain percentage from Slaa and add to Kikwete and the total vote will remain the same. For those who know excel knows what i'm talking about.

Unajua hawa wataalamu wa kompyuta mwanahalisi iliwaripoti kabla na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na "usalama wa taifa". Hawa watu walishirikiana na miraji hapo upanga kufanikisha mpango wote. Kuna haja NEC kabla haijatangaza majumuisho ya mwisho tuone kama kula wanazojaza hapo tume zinacorrespond na zilivyotoka mikoani.

It is time to kick out Kilavu and Makame. They never learn from Kivuitu.

Now i begin to contemplate the fate of Miraji and Ridhiwan will not be different from that of Uday and Kusay the late sons of Sadam Hussein !!!!
 
Jamani wabunge wote wa upinzani waungane wajenge Mswada immediately, NEC ivunjwa halafu NEC nyingine ipitishwe na BUNGE na kupata imani na BUNGE kuwa ni HURU na HAKI, maana Kiravu kachaguliwa na JK unategemea nini? DR Slaa aliliona mapema hili, BUNGE lijalo haraka sana wabadilishe sheria ya uchaguzi kuhusu uteuzi wa NEC na wajumbe wake, Ni Bunge ndilo litaweza, la sivyo upinzani watabaki wakijaza maji gunia
 
Hii haikubaliki nasema kama noma na iwe noma

Matokeo Tunduru Kaskazini

Kikwete amepata kura 22,261

Slaa amepata kura 1,965

Lipumba amepata kura 12,935
 
NEC itapinduliwa lakini kura za urais lazima zihesabiwe upya tena kwa umakini mkubwa. Safari hii watanzania tusikubali. Matokeo hayo, yanapangwa tu kwa program maalum iliyosanifiwa kufanya hivyo. Chadema mkituacha wananchi tunaumia hivi bila kuchukua hatua mtakuwa mmetuvunja moyo sana.
 
Check hii jimbo la Tunduru Kaskazini

Kikwete amepata kura 22,261

Slaa amepata kura 1,965

Lipumba amepata kura 12,935

Nyie watu wa CHADEMA ni watu wa ajabu sana. kwani Lipumba kupata kura nyingi kuliko Slaa ni tatizo? au kwa kuwa kwenyehilo jimbo kuna waikristu wengi? Inajulikana uchaguzi wa mwaka huu ni Waislamu vs Waikristu inasikitisha sana ila matokeo ya urais yanaonesha hali hiyo.

Lete kura za ububge tulinganishe.
 
haitawezekana SLAA atakuwa wapili

source Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza

P.MZIRAY 50,675 J.KIKWETE 2469507 W.SLAA 736366 I.LIPUMBA 308597 H.RUNGWE 10120 M.MUHANYWA 6994 F.DOVUTWA 4321 KURA ZILIZOHARIBIKA 74,138

Jamani, tuwe makini sana. Siyo suala la SLAA kuwa wa pili au wa tatu. Kama kura zikihesabiwa kihalali bila wizi, kuna uwezekano mkubwa kuwa SLAA atakuwa wa kwanza na hivyo kuwa Rais wa Tanzania. Hapa CCM wanacheza na mind games. They are manipulating the results makusudi kuwakatisha tamaa wafuasi wa CHADEMA kuhusu SLAA kuwa Rais ili juhudi zao wazihamishie kuhakikisha SLAA anakuwa mshindi wa pili badala ya wa tatu wakati SLAA anaweza kushinda kuwa Rais. Narudia tena, matokeo yaliyotoka so far hayafiki hata kura milioni 1.5 na ni ya mikoa ambayo CCM na CUF ina nguvu. Zingatia kuwa watu waliojiandikisha kura ni 19.6 milioni. Turnout ilikuwa ndogo na huenda ikawa 50%, hivyo kura halali ni kama milioni 10. Mikoa ambayo SLAA kafanya vizuri sana na ina kura kama milioni 8 zilizobaki wamezuia matokeo na watayatoa very late haraka haraka ili huenda kesho usiku wamtangaze Kikwete Rais na ijumaa aapishwe fasta.

Nadhani hii strategy yao ya kutengeneza illusion kuwa Kikwete anashinda kwa kishindo kwa kutoa matokeo ya mikoa ambayo CCM iko strong imekuwa very effective. Watu wengi sasa mitaani na hata huku JF hawazungumzii tena ushindi wa SLAA na ukombozi wa Tanzania. Wanazungumzia 2015 na kujadili zaidi ushindi wa wabunge wa CHADEMA. Naambiwa hata baadhi ya viongozi wakuu wa CHADEMA wenyewe wameshakata tamaa.

We must not forget the bigger picture! Bado SLAA ana nafasi nzuri sana ya kwenda Ikulu iwapo kura kwenye mikoa mikubwa iliyobaki zitahesabiwa bila wizi. Tulinde kura za Urais kama tulivyolinda kura za wabunge wetu. Tushinikize matokeo ya kura za Rais kwenye mikoa iliyobaki ambayo SLAA amezoa kura nyingi yatolewe mapema na bila kuibwa kama tulivyofanya kwenye ubunge kwa mafanikio makubwa.

Timu kabambe ya wabunge teule wa CHADEMA isaidie pia kutoa shinikizo hili.

Tusikubali kuchezewa akili na kudanganyika na kukata tamaa kuwa Urais ni mpaka 2015. Huu unaweza kuwa mwaka ambao SLAA atashinda Urais tukiwa makini.

By the way, wanaosema CHADEMA iende mahakamani wakumbuke kuwa katiba mbovu iliyopo inasema kuwa NEC inapo tangaza matokeo ya Urais hayawezi kupingwa mahakamani au popote na ni final hata kama kuna ushahidi wa wazi wa rushwa, wizi wa kura au fraud yoyote. Matokeo yanayoweza kupingwa mahakamani ni ya Ubunge na udiwani tu.

Hapa suluhisho tu ni PEOPLE'S POWER!
 
My heart and soul are crying a lot asking God to rescue us since we have been suffered a lot!
 
Hii conspiracy theory inaweza kuwa ya kweli. Mimi nilishangaa sana kumuona jana Kinana anazungumza kwenye TV kuwa pamoja na kuwa NEC ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza ushindi, tathmini iliyofanywa na CCM yenyewe ni kuwa wameshashinda kwa kishindo. Akawapongeza upinzani kwa kujitahidi na kupata wabunge 29 bara mwaka huu ikilinganishwa na 2005 walipata 6. Huenda kama ilivyosemwa kuwa hapa CCM wanawaandaa Watanzania wakubali ushindi wa CCM uwe wa halali au la.

Pia, jana hiyo hiyo Makamba naye akaongea na waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa kugombea uspika kwa wabunge wa CCM wakati matokeo ya zaidi ya nusu ya majimbo 239 bado hata kutangazwa.

Zote hizi huenda ni sehemu ya mkakati huu wa kuonesha kuwa CCM tayari imeshinda ili wakichakachua matokeo muhimu yaliyobaki hakuna wa kuhoji na watajitetea kuwa kura za awali zilionesha tangu mapema kuwa wao wanashinda.
 
Achana na website za vilaza...wavivu wa kufikiri. Nimesusia upuuzi wowote unaotangazwa na watu wanaoitwa TBC eti ukweli na uhakika. nenda kwenye website ya mwananchi-www.mwananchi.co.tz
Nitaendelea kuliheshimu gazeti la mwamanchi kwa kulinunua kila ninapoweza.
 
Back
Top Bottom