Secondary Leaving Certificates'; je kuna utaratibu mpya wa kuipata miaka ya sasa hivi?

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,212
2,808
Inawezekana hapo juu sijaeleweka vizuri lakini fuatana nami utaelewa tu,

Shule moja hivi ipo Wilaya ya Kilindi Tanga... vijana waliohitimu mwaka jana wakifuata leaving zao wanakuta hazijakamilika huku chini basi wanapewa hiyo kitu na namba ya simu kisha wanaambiwa waende Songe (makao makuu ya wilaya) wakifika wamtafute huyo mwenye namba hiyo kwajili ya kwenda kutype sehemu iliyobaki

Tena na gharama headmaster anawatajia kabisa kuwa ni buku basi vijana wanafika kule wanaambiwa gharama ni buku 4. Tena afadhali angekuwa mtu wa serikali hata, laa! Ni mtu binafsi tu.

Baada ya hapo ndipo wanalazimika kurudisha shuleni cheti hicho kwajili ya kusainiwa na mhuri. Kwa maelezo hayo na nikikumbuka enzi zetu za kupewa leaving certificates siku ya mahafali ndomaana nauliza siku hizi huo ndo utaratibu au ni ?

Jambo lingine (nachomekea) hivi kwanini siku hizi kuna baadhi ya miaka hakujatolewa vyeti vya kuhitimu elimu ya msingi. Yaani madogo kila wakienda shuleni kuulizia wanaambiwa havijatoka, au ndo habari ya elimu ya msingi mpaka form four inachukua hatamu mdogo mdogo?
 
School leaving certificate kwasasa havitoki shule kama miaka ya nyuma maana mtu anaweza pewa kiujanjaujanja japokuwa hakina msaada mkubwa huko mbeleni.

Kwasasa lazima vipitie wilayani then madogo ndyo waje wachukue

Nakuhusu primary nao utaratibu umebadilika navyo sio shule tena kama zamani.

ndiyo maana unaona madogo wanaangaika tofauti na miaka ya nyuma enzi za mitiani mitatu mnafaulu wanafunzi watano tu toreo la Kwanza.
 
Back
Top Bottom