Second President of the Republic of Kenya, Daniel Toroitich Arap Moi dies at 95

Nimeona video Moi akiagwa na Rais Kenyatta mwili ukiwa umelazwa juu ya meza!, kwanini wasingemuweka kwenye jeneza?

Sent using Jamii Forums mobile app

IMG_4620.JPG

Sio Moi tu hata Mzee Jomo Kenyatta Aliagwa hivo hivo bila ya mwili kuwekwa kwenye jeneza



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
jd41: utaona picha ya juu ni mzee kenyatta wakati anaagwa na yapili ni mzee moi inaonekana ni taratibu zao za uagaji


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Poleni sana Ndugu zetu wa Kenya kwa kuondokewa na Rais wenu Mstaafu wa Awamu ya Pili Mheshimiwa DANIEL TOROITICH ARAP MOI.

Maandiko matakatifu yanasema kuwa kila Nafsi itaonja mauti. Jirani yako akipata matatizo kama jirani lazima uungane naye katika hayo majonzi.

Nimewaona Marais majirani wakiwafariji hilo ni jambo jema sana. Narudia kusema POLENI SANA.
 
Daud1990,
Tena sio siri, sema wakenya wanajizuia tu maanake kwenye mila na desturi za kiafrika sio jambo la busara kumsema vibaya mwendazake. Ila kiuhalisia ni kwamba Moi aliwatesa sana wakenya na udikteta wake, kwa miaka 24. Tena alikuwa muuaji ambaye alitengeneza 'torture chambers' pale Nyayo House hapa jijini Nairobi za kuwatesa wapinzani wake.

Uhuni ambao alimfanyia nyota ya Kenya, Kenneth Matiba, mercury poisoning ambayo ilifanya apatwe na stroke utamuandama hadi Jehanam. Kenneth Matiba ambaye alishinda uchaguzi mkuu 1992 aliaga dunia akiwa tayari amemsamehe Moi bila hata ya Moi kuomba msamaha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom