Sea food gani unaipenda?

Mie hao wadudu ndo ugonjwa wangu kuanzia pweza,ngisi,kamba,crabs,lobster etc na mayai ya samaki pia
 
Mkuu utakuwa umekulia pwani
Ewaa,uko sahihi shekhe,mie mmasai lakini nimekulia kwenye ukanda huu wa pwani,jioni shurti upitie kwenye meza za pweza na ngisi na sea food nyengine ndo siku inakuwa imeenda vizuri.
 
Kambakochi, pweza, ngisi, konokono, kamba w kawaida duu baharini siachi kitu hapa wa bars lzm aisome
 
Sea foods; kamba kochi, lobster, ngisi, changu, tasi, kolekole, mlimba.....kuna mmoja nimesahau jina, ni kama mwenzie mlimba kwenye supu aiseee......iwe supu ya kienyeji, pita SOMANGA pale ufaidi hiyo supu
Kambakochi ndio lobster
 
Pweza tu na samaki dagaa mchele wale wakiwa na kile kikachumbari flani noma sana.
Uduvi (prawns) huwa wana harufu mbaya na ladha haieleweki siwapendelei sana.
 
Dagaa mchele wakikaangwa kwa ugali na bamia plus mboga ya maboga..
 
Cigale,Chaza,,Kamba,Kamba wakubwa,Pweza,Ngisi,kaa,Hao ndio seafood colective name.ChanguSongoro,Ngushi,Nguru,Jodari,sehewa,mziya,Kole kole hao ni samaki.
 
Nipeni location ya restaurant au cafeteria inayopika hizo sea food kwa ustadi wa kiwango cha lami
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom