Sea Cliff itabomolewa kwa kukiuka sheria za kulinda fukwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sea Cliff itabomolewa kwa kukiuka sheria za kulinda fukwe?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Synthesizer, Jul 12, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Tulimlaumu sana Mkapa kwa kukiuka maadili ya uongozi na kujiuzia mgodi wa Kiwira. Aliitwa fisadi na kuzomewa hadi na watoto wadogo, na wengi hata tukitaka afikishwe mahakamani, na moto wa madai haya ukizimika pale tu JK alipoibuka na kumtetea.

  Lakini je, tumesahau kwamba Sea Cliff Hotel ilijengwa kwa kukiuka sheria zile zile zilizofanya nyumba za vigogo kuvunjwa hivi karibuni? Je, tumesahau kwamba Sea Cliff Hotel ilijengwa kwa mgongo wa Mwinyi ambaye naye alikiuka maadili ya uongozi kwa kutoa kibali kinyume na sheria za mazingira ili Sea Cliff ijengwe, ikisemekana kwa familia yake kupewa share katika hii hoteli?

  Kwa hiyo swali ni kwamba, Sea Cliff Hotel itavunjwa kama zilivyovunjwa nyumba nyingine kwa kutumia sheria ile ile ya ujenzi unaokiuka sheria za kulinda fukwe?
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
 3. 1

  19don JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  golden tulip je?
   
 4. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,341
  Likes Received: 2,666
  Trophy Points: 280
  Bongo hapa asilimia kubwa ya majengo yaliyokaribu na barabara au fukwe ujenzi wake umekiuka sheria ya umbali kutoka ukingo wa maji ya bahari au barabara
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nayo pia ipo zaidi ya mita 30:

  [​IMG]
   
 6. M

  Mundu JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ana Tiba alisema hivi katika moja ya maelezo yake kuhusu nyumba ama majumba yaliyojengwa ufukweni mwa bahari..."haiwezekani mtu na mkeo na watoto wako mujikatie eneo la bahari na kujenga nyumba, mkiwanyima watanzania wengine kupata madhari na upepo mzuri wa bahari..." na akawa na exception kwa mahoteli yenye kujengwa maeneo hayo kwa kuwa yenyewe ni public utilities...yaani, mimi na wewe na yeyote mwenye kuhitaji anaweza kwenda, kununua Soda na kufurahia mandhari na kupata upepo mwanana wa bahari.

  May be ilikuwa ni kauli ya kulinda miradi ya vigogo kama hotel ya Sea Cliff kuingia katika mkumbo wa kuporomoshwa.. Hivi ni nani anamiliki Sea Cliff Hotel?
   
 7. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Mkuu Zomba, naona labda unaongea "kilometre" na sio "meta"! Zote hizi ziko ndani. Mie nadhani ili kuepusha aibu angalau Tibaijuka anabomoe sehemu yeyote ya hoteli ndani ya meter 30, kwa mfano swimming pool au vibanda. La sivyo ataleta chuki sizizo na msingi kuona kuna watu wanapendelewa.
   
 8. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,394
  Likes Received: 6,578
  Trophy Points: 280
  kwa hili l ahoteli wakuu.si sawa kabisa..hat huko majuu mbona watu wanajenga tu mahoteli kando mwa bahari..ni hatari lakini ujenzi wa hoteli kando mwa bahari ni vivutio kwa watalii, sasa tukiziondoa , tunaondoa biashara tofauti na nyumba binafsi..tuzungumze facts...
   
 9. 1

  19don JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
 10. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  hili nalo neno. kuna GIRAFFE OCEAN VIEW pia, lkn ukirudi nyuuuma miaka ile enzi ya mwl kuna ile inaitwa KUNDUCHI BEACH HOTEL kuna wakati huko nyuma ilikaribia kumezwa na bahari, hata BAHARI BEACH HOTEL hizi ni tangu enzi ya Mwl. nafikiri huenda kuna sheria inayotofautiana kati ya makazi ya watu na hotel .ngoja tusubiri
   
 11. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
 12. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Mkuu ni mita 30 au 60?
   
 13. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sea cliff ivunjwe!?? Thubutuu..
   
 14. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  sheria yenyewe nadhani in mapungufu...mimi sioni kutojenga sehemu hizi kunavo hifadha zaidi ya kuachia erosion kuvamia kwa nguvu..
  Pale oysterbay coco beach bahari ilikua mbali zaid ya mita 500 miaka 15 iliyopita sasa ipo chini ya mita 100 kuja barabarani..
  Hizi sehemu ni nyeti zinaweza kuendelezwa bila ya kuaharibu mazingizra na zikachangia sana katika uchumi wa nchi
  sio sahihi ya kwamba tusiendeleze sehemu zetu za ufukweli kwa kisingizio hichi..ukweli watu wanatucheka sana..wakati nchi nyengine zina reclai bahari ili kuendeleza ujenzi ndani ya fukwe
  kinachotakiwa ni mchakato wa uwazi na business plan ya uhakika ambayo investor anapewa jukumu la kuendeleza lazima ayatelkeleze.
  Golden tulip na sea cliff ni moja ya sehemu nzuri na kuvutia ndani ya dar es salaam.
  Hii ni pamoja na kunduchi( wet an worls), bahari beach, nk
  pia tuna tatizo kubwa la uchoyo na roho mbaya ambazo zinakwaza maendeleo kwa visingizio vya hapa na pale
   
 15. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  sheria yenyewe nadhani in mapungufu...mimi sioni kutojenga sehemu hizi kunavo hifadha zaidi ya kuachia erosion kuvamia kwa nguvu..
  Pale oysterbay coco beach bahari ilikua mbali zaid ya mita 500 miaka 15 iliyopita sasa ipo chini ya mita 100 kuja barabarani..
  Hizi sehemu ni nyeti zinaweza kuendelezwa bila ya kuaharibu mazingizra na zikachangia sana katika uchumi wa nchi
  sio sahihi ya kwamba tusiendeleze sehemu zetu za ufukweli kwa kisingizio hichi..ukweli watu wanatucheka sana..wakati nchi nyengine zina reclai bahari ili kuendeleza ujenzi ndani ya fukwe
  kinachotakiwa ni mchakato wa uwazi na business plan ya uhakika ambayo investor anapewa jukumu la kuendeleza lazima ayatelkeleze.
  Golden tulip na sea cliff ni moja ya sehemu nzuri na kuvutia ndani ya dar es salaam.
  Hii ni pamoja na kunduchi( wet an worls), bahari beach, nk
  pia tuna tatizo kubwa la uchoyo na roho mbaya ambazo zinakwaza maendeleo kwa visingizio vya hapa na pale
  [
   
Loading...