Screen Protector kwenye simu ni aina nyingine ya Upigaji

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
3,477
2,000
Kuna siku isio na jina wala saa UTAJUA HUJUI
Mkuu hii comment imenifanya nitie neno. Simu yangu sijawahi kuiwekea protector, na nilikuwa mzee wa kutamba kama muanzisha uzi ila leo nikiwa nimeishika simu yangu mkononi, yani sijui ingekuwaje tu nashangaa ngoma iko chini kwenye tiles, kibaya zaidi imejifunika yani ninavyoandika hapa simu yangu nimeichukia kabisa☹️.
 
Mayu

JF-Expert Member
May 11, 2010
4,068
2,000
Hii Simu nilinunua mwezi wa 9 mwaka jana, mpaka inafika mwezi wa 12, nilikua nshaweka screen protector 3 (ya elfu 5, elfu 7 na elfu 10).

Ukisahau 100 mfukoni, au ukaichanganya na funguo, unakuta ishapasuka.

Nilikua najiuliza sana, inawezekanaje hii gorila glass iwe protected na plastic cover? Kuanzia mwezi wa 12 mwishoni niliachana na huo wizi wa kununua protector, na simu yangu sasa haina michubuko na inaonekana kama mpya, mwonekano wa kiwandani kabisa.

Wakuu, achaneni na hizi protector, ni aina nyingine ya wizi, CAG na au TBS wanapaswa kuchunguza. Hazina viwango na sidhani hata kama hata zinafikia hardess/kiwango cha gorilla glass 0.5. Kwanza hizi protector zinaharibu mwonekano wa simu.

Siku za kioo cha simu yako zinahesabika.......... utajuta

Nilikuaga na mtazamo kama wako
Siku nikaja kuiangusha Samsung yangu nilikua naipa sifa kibao sijui ina gorila glass......kwenye tiles khaaaaa
Ndio nikajua kila kioo kinapasuka
Sasa hivi sitaki ujinga navisha hadi na cover
 
Wiwachu

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
626
1,000
Mimi niliachana nazo mda sana now naweka ile ya karatas tu kuzuia kicbubuka.. Tunadanganywa kuwa inazuia simu kupasuka inazuiaje wakat protecter yenyewe sio imara??? Nasi tumekubal huo uongo... Never
 
KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,263
2,000
Mkuu hii comment imenifanya nitie neno. Simu yangu sijawahi kuiwekea protector, na nilikuwa mzee wa kutamba kama muanzisha uzi ila leo nikiwa nimeishika simu yangu mkononi, yani sijui ingekuwaje tu nashangaa ngoma iko chini kwenye tiles, kibaya zaidi imejifunika yani ninavyoandika hapa simu yangu nimeichukia kabisa☹️.
Kwa iyo ungekuwa umeweka karatasi ingedunda!?
 
KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,263
2,000
Siku za kioo cha simu yako zinahesabika.......... utajuta

Nilikuaga na mtazamo kama wako
Siku nikaja kuiangusha Samsung yangu nilikua naipa sifa kibao sijui ina gorila glass......kwenye tiles khaaaaa
Ndio nikajua kila kioo kinapasuka
Sasa hivi sitaki ujinga navisha hadi na cover
Ishu ni kwamba, hata nikiweka hizo plastic, siku ikindondoka kwenye kokoto, itakua sawa tu na ambavyo ningekua sijaweka.
 
masafi

JF-Expert Member
Aug 4, 2015
545
500
Mimi ujinga sitaki kabisa ninunue simu gharama kubwa harafu niizibe na macover, protector, siwezi naiacha uchi tu.
 
medieval2april2021

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
343
500
WEKENI PROTECTOR SIMU ZENU, NARUDIA WEKENI PROTECTOR SIMU ZENU!

Wakuu ninaandika hapa ni kijana mwenye uzoefu wa kupasua vioo vya simu zake, mpaka sasa nimepasua vioo vinne vya Samsung tofauti sababu kuu ni kudharau kazi ya PROTECTOR niliamini ni Upigaji na kuharibu Muonekano wa simu.

Nilishauriwa sana lakini nilikaza kichwa na kukaidi ushauri lakini nikajionea jamani,
10,000 ya PROTECTOR ilinigharimu Malaki ya Pesa.

Niliangusha NOTE 5, toka juu ya kitanda mpaka chini (kitanda cha Dabo Deka), asee ilizima palepale nilihisi uchungu wa kufa mtuu nikaapa sitarudia kudharau PROTECTOR. Nikaenda dukani kuulizia bei ya kioo ikanishinda nikaona heri ninunue Simu mpya.

Nikajiseti nikanunua SAMSUNG S6, kalikua na muonekano mzuri Wallahi kasimu kametuliaaa Mang'anyuu na karangi ka Gold, nilizidi kuipenda ile simu kila nilipoitazama yani hapa sikuweka PROTECTOR wala COVER, niliamini ningeharibu muonekano wa kasimu kangu.

Ikatokea siku iso na jina Ikaanguka ikiwa na wiki 3 tu au 4 toka ninunue, aseeeeeeeeeee niliumia sana. Lakini nikaapa sitanunua simu nyingine nitatengeneza ile na nitadumu nayo.

Kuulizia kioo nikaambiwa 160K kariakoo, siku hiyo rafiki yangu akaninunulia PROTECTOR kwa pesa yake akiamini ningeangusha tena. wakaniwekea kioo FEKI, aseeeeeeeeeee simu ilipoteza muonekano wadau wakawa wananicheka eti walidai hawaielewi simu yangu sio Tecno, Sio Samsung.

Nikatoa PROTECTOR, hatukukaa muda nikapasua kioo kwa kuegemeza kitu juu ya simu, wino ukivuja simu ikawa haieleweki tena, nikakomaa nikaenda k/koo nikatafuta kioo OG mpaka nikakipata fundi akafunga nikadunda nayo huku nikiapa kuwa Nitaitunza, nitailinda na kuitetea S6 yangu siku zote za maisha yangu. Bado sikuweka PROTECTOR ila nashukuru ilidumu mpaka nikaiuza.

Kwa mafunzo nlopitia nawasihi ndugu zangu muweke PROTECTOR simu zenu.

Nimalize kwa kusema 'Simu bila PROTECTOR ni sawa na kufanya Mapenzi bila KONDOM'

KAMA UNAIPENDA UTAILINDA!
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
24,068

kesi zako zinahitaji cover zaidi ya protactor.

cover linazuia simu kuumia au kioo kwa zaidi ya 85%,ila protactor inafanya kazi 2% tena inazuia kioo tu.
 
ankai

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
2,375
2,000
Endelea kujitapa mbele za watu siku haziko mbali nayo itakuadhiri mbele za watu ivyo ivyo wewe unadhani walio tengeneza protecter hawana akili sio ngoja utafurahia shoo ya upasukaji wa kioo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom