Scramble for and Partition of Africa: With New Zeal, New Strength and New Speed! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Scramble for and Partition of Africa: With New Zeal, New Strength and New Speed!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LENGEJU BOB, Sep 3, 2011.

 1. L

  LENGEJU BOB Member

  #1
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uvamizi wa mataifa ya Ulaya na Marekan unaoendelea dhidi ya Mtaifa huru ya Africa. Walipokuja na ajenda ya kutufundisha “utu”. Wakaja na divai ya ‘ustaarabu’ ndani ya kiriba cha utumwa/ukoloni. Na sasa wanakuja na divai ya “Demokrasia” ndani ya kiriba cha uvamizi. Bila aibu na mchana kweupe, waasi wa serikali halali wanaungwa mkono. Huku viongozi wetu Africa wakinywea kama kuku wa mdondo.
  Hapa ndo utaona ombwe la kizazi cha viongozi wa kaliba ya Nyerere, Nkuruma, Mugabe, Mandela… Enzi za hao wanaume hawa makaburu wasingetamba hivi.. Juzi Mugabe kamfurusha balozi wa Libya aliyethubutu kupeperusha bendera ya waasi. Huku kwetu jamaa wamepandisha pendera ya waasi, Membe kawaandalia chai ikuli na kuwabembeleza washushe kidogo….Wakagoma….

  Hivi kwanini tunawabembeleza hao? Tutapoteza nini tukifukuza hata hao wamarekani na waulaya? Tutapoteza hizo dinner part za white house? Au tumisaada twa kebehi kwenye semina elekezi na ukimwi? Walitumika zaidi ya $300 bilioni kwenye vita ya Iraq wakati midaada ya maendeleo kwa Bara lote la Africa kwa miaka mitatu (2008,2009, 2010) haikuzidi $ 4 bilioni. Wakati wametumia mabilioni hayo kuiharibu Iraq leo wanaomba misaada, wanafanya haraambee ya kusaidia kuijenga upya. Pesa za kubomoa wanazo ila za kujenga hawana.. Tusipojipambanua sasa kwamba hatukubaliani na ubeberu wao watatusumbua sana siku ikidhihirika kuwa Tanzania ni hazina ya mafuta na Uranium kama inavyosemekana.. Watatuvamia na hakuna anataye tutetea!
   
 2. K

  Kampini Senior Member

  #2
  Sep 3, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu upo sawa kabisa,kinachoendelea sasa hv hakina tofauti na enzi za mkoloni,matabaka yamejichomoza kila pahala,dalili zote za uporaji wa uchumi wa mataifa yanayoendelea upo wazi,viongozi wetu wamegeuzwa vibaraka wa magharibi,ukweli kwao ni ule uliosemwa na mzungu na si Muafrica,Kwao mkoloni yuleyule sasa wamemvua gamba wanamwita mwekezaji. Inauma sana kuona viongozi wamesahau walikotoka,walipo na hata waendako hawakujui.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tena na hii serikali yetu legelege naona watagawana kila kona ya nchi yetu under the umbrela of misaada na mikataba kama aya akina Mangungo wa msovelo
   
 4. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Yani hapa sijui unaongea kitu gani? hivi unawaambia wananchi au viongozi?kama unawalenga wananchi nadhani ungeyageuza yawe ya viongozi?unaposema waasi wa serikali "halali" halali wanaungwa mkono...hivi hao viongozi wa "serikali halali" wanafanya nini kuhakikisha hawawi wakoloni ndani ya nchi zao?Washakuwa mabwanyenye wanajilimbikizia mali na kuwasahau wananchi hapo unadhani wananchi wanafurahia tu?Viongozi waache kuwafanya wananchi wao waliowapa kura ni wajinga.Wakibadilika sidhani kama kutakuwa na haya mabo ya uasi.Na kama wazungu wanakuja kututawala basi wanatumia udhaifu wa viongozi wa "serikali halali"
   
Loading...