• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Scott Peterson: Je ni kweli alimuua mkewe mjauzito wa miezi 8…?

Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000

Scott Peterson
....

Amber Frey nyumba ndogo ya muuaji Scott....

Enzi ya uhai wa Laci Peterson


Scott Peterson akiwa na mwanasheria wake Mark Geragos


Scott Peterson

Mnamo Desemba 25, 2002, Laci Peterson aliripotiwa na mumewe Scott Peterson kupotea kutoka katika nyumba yao iliyoko katika jiji la Modesto huko jimboni California nchini Marekani. Alikuwa na ujauzito wa miezi 8 ambapo alitarajiwa kujifungua hapo mnamo Februari 10, 2003, na walikuwa wamepanga kumwita huyo mtoto wao wa kiume jina la Conner Peterson.

Mbali na mumewe, watu wawili wa mwisho kuwasiliana na Laci kabla ya kutoweka alikuwa ni dada yake kwa mama mwingine aitwae Amy Rocha na mama yake Sharon Rocha.

Mnamo Desemba 23, 2002, Amy alimkata Laci nywele majira ya jioni. Amy alizungumza na Laci siku hiyo hiyo kwa njia ya simu majira ya saa 2:30 usiku.Siku iliyofuata yaani tarehe 24 Decemba majira ya saa 4:30 asubuhi, jirani mmoja aliona mbwa wa akina Laci aitwae macKenzie akizurura hapo mtaani akiwa na mkanda umening'ia shingoni jambo ambalo halikuwa la kawaida kwa mbwa huyo kuonekana mtaani peke yake. Jirani huyo alimchukua mbwa huyo na kumrejesha ndani ya uzio wa nyumba ya akina Laci.

Land Rover Discovery ya mwaka 1996 ya Laci ya ilikutwa ikiwa mtaani. Mkoba wake ambao ulikuwa na funguo na simu yake ya kiganganjani vilikutwa juu ya meza nyumbani kwake. Wakati Scott Peterson aliporudi nyumbani kutoka kuvua samaki jioni ya Desemba 24, mkewe Laci hakuwepo nyumbani. Kuna taarifa kwamba baada ya kukuta mkewe hayupo hapo nyumbani Scott alifua nguo zake, kisha akala pizza ya baridi, akasafisha jikoni kwake na kisha akaoga. Baadae majira ya saa 11:20 jioni alimpigia mama yake Laci, yaani Sharon Rocha na kumuuliza iwapo Laci yuko huko kwake. Alipomjibu kwamba Laci hayuko huko kwake, Scott alisema, "Laci amepotea." Baadae Sharon alisema kwamba alijua moyoni mwake kuwa jambo lisilo la kawaida limempata binti yake.

Scott alidai kwamba wakati alipoondoka asubuhi ya siku hiyo, mkewe Laci alikuwa amepanga kwenda kununua vinywaji kwa ajili ya maandalizi ya Christmas kisha amtembeze mbwa wao aitwae McKenzie katika eneo la karibu litwalo East La Loma Park.

Wazazi wa Laci walipiga simuPolisi majira ya saa 12:00 jioni kuwajulisha kuhusu kupotea kwa binti yao. Mara moja Polisi walianza msako wa kumtafuta Laci katika maeneo ya jirani. Polisi, majirani, marafiki na ndugu wa familia ya Laci walianza msako mkali katika meneo ya karibu kwa miguu. Magari ya doria, Helikopta iliyokuwa imefungwa taa maalum zenye mwanga mkali na kifaa cha kinachoweza kutambua mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na wataalamu wa kutafuta mwili ndani ya maji na mbwa wa kunusa walihusishwa na msako huo.

Taarifa zilisambazwa katika idara za upelezi na Polisi nchi nzima. Polisi waliamini kwamba kuna mchezo mchafu kwa sababu walikuwa na wasiwasi kwamba haiwezekani Laci atoweke siku ya Christmas bila kuwasiliana na yeyote. Katika mkutano na wandishi wa habari Detective Al Brocchini alisema, "Kutoweka kwake ni kinyume na aina ya maisha aliyokuwa akiishi."

Awali zawadi ya kiasi cha dola 25,000 kilitangazwa kwa mtu yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa Laci baadae kiasi hicho kikaongezwa hadi kufikia dola 250,000, halafu tena kikaongezwa na kufikia dola 500,000. Matangazo yalisambazwa kila mahali vikiwemo vipeperushi. Marafiki na wanafamilia na watu wengine waliojitolea walianzisha kituo jirani na hotel moja iliyoko katika eneo hilo iitwayo Red Lion ambapo kituo hicho kilikuwa kikirekodi maendeleo ya kumtafuta Laci kutoka maeneo mbalimbali. Zaidi ya watu 1000 walijitolea kusambaza taarifa za kupotea kwa Laci katika maeneo mbalilmbali nchini humo.

Wakosoaji walikejeli jitihada hizo kwa kuziita kama zimepewa uzito mkubwa na usiostahili kwa sababu tu aliyepotea ni Mzungu, "Missing white woman syndrome."

Walishangaa kwamba ilikuwaje kupotea kwa Evelyn Hernandez mhamiaji kutoka nchini Al Salvador ambaye hakuwa mzungu hakukupewa uzito na jamii na Vyombo vya habari kama ilivyo kwa Laci. Kama Laci naye Evelyn aliyekuwa na umri wa miaka 24 alipotea mnamo July 24, 2002, akiwa na ujauzito wa miezi 8 lakini akiwa na mtoto wake wa kiume wa umri wa miaka 5 katika jiji la San Francisco, jiiji ambalo liko katika jimbo hilo la California. Baadae mwili wake ulipatikana katika ufukwe wa San Francisco, na muuaji wake hakupata kujulikana.

Hata hivyo ilibainika kwamba ni jitihata binafsi zilizochukuliwa na familia ya Laci, kusambaza habari za kupotea kwake ndio sababu iliyopelekea habari zake kusambaa mithili moto nyikani. Kwa muda wa siku mbili, idadi ya watu wapatao 900 walikuwa wamehusika katika kumtafuta Laci kabla ya polisi na polisi jamii kujiunga katika msako huo huku vyombo vya habari vikifuatia katika kuripoti msako huo.

Je huyu Laci ni nani?

Laci Denice Rocha alizaliwa hapo mnamo Mei 4, 1975 katika mji wa Modesto huko California. Wazazi wake ni Dennis Robert Rocha na Sharon Ruth Anderson, ambao walikutana wakati walipokuwa wakisoma elimu ya juu na mara baada ya kumaliza masomo walifunga ndoa. Mtoto wao wa kwanza Bret Rocha alizaliwa mwaka 1971, Laci alikuwa ndiye mtoto wao wa pili alizaliwa mwaka 1975. Wazazi wake waliachana mara tu Laci aliposherehekea mwaka wake wa kwanza kuzaliwa.

Dennis baadae alioa mke mwingine na kujaaliwa kupata mtoto wa kike katika ndoa yake hiyo aliyemwita Amy. Laci alikua kwa umri na kimo huku akiwa na kawaida ya kumtembelea baba yake katika shamba lake la mifugo katika mji wa Escalon hapo California. Alisoma katika shule na vyuo mbalimbali huku akishika vyeo mbalimbali katika shule na vyuo alivyosoma. Alipokuwa chuoni alikuwa akisomea elimu ya mimea. Alikutana na Scott Peterson katika mghahawa mdogo uliokuwa katika eneo la Morro bay uliokuwa ukiitwa Pacific Café.

Mnamo Desemba 1996 Scott na Laci walifunga uchumba na walikuja kufunga ndoa rasmi mnamo Agost 9, 1997, miezi michache kabla ya kumaliza elimu ya juu. Kwa muda wa miaka miwili walichelewa kupata mtoto tangu walipofunga ndoa, na Laci hakufurahishwa na hali hiyo na alikuwa akizungumzia jambo hilo na mwenzake kuhusu kupata watoto. Mnamo Desemba 2000 waliamua kuanza kutafuta mtoto kwa njia yoyote. Kutokana na Laci kuchukua muda mrefu kubeba mimba, waliamua kujaribu njia ya kupandikiza na hivyo kufanya miadi na kituo kinachojishughulisha na kazi hiyo.

Hata hivyo Laci alibeba mimba kwa njia ya kawaida hapo mnamo Mei 2002. Walitarajia mtoto wao huyo ambaye walishajua ni wa kiume kuzaliwa Februari 10, 2003, na walipanga kumpa jina la Conner Latham Peterson.

Awali Polisi walishindwa kumhusisha Scott kuhusika na kupotea kwa mkewe kutokana na familia ya Laci ndugu na marafiki kumtetea kuwa hawezi kuhusika kupotea kwa mkewe kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwa mkewe.

Hata hivyo Polisi walizidi kumtilia mashaka Scott kutokana na jinsi alivyokuwa akijichanganya katika maelezo yake kuhusiana na kupotea kwa mkewe. Ilikuja kubainika kwamba Scott alikuwa na mahusiano nje ya ndoa yake. Uhusiano wa siku za karibuni ulikuwa ni kati yake na binti mrembo na mtaalamu wa kufanya masaji aitwae Amber Frey. Amber alikwenda Polisi kumripoti Scott ambaye ndio kwanza walikuwa wameanza kuwa na mitoko naye siku za karibuni baada ya kugundua kwamba alikuwa ameoa na mkewe ndiye aliyeripotiwa kupotea siku za karibuni na bado anatafutwa.

Baada ya taarifa hizo kutolewa, familia ya Laci ilijitoa kumtetea Scott. Baadae walisema kwamba hawakuchukizwa na kitendo cha Scott kutoka nje ya ndoa yake, bali ni ile kusikia kwamba Scott alimwambia Amber kuwa mkewe amekufa na Christmas inayokuja itakuwa ndio ya kwanza kuisherehea peke yake bila mkewe ikiwa ni siku 15 kabla ya Laci kupotea. Hata hivyo mama yake Laci, Sharon Rocha alioneshwa kushangazwa na kitendo cha Scott kudai kuwa mkewe amepotea mara tu alipomkosa hapo nyumbani kwao. "Nilishangaa kwa jinsi alivyotumia neno hilo la mkewe kupotea mara kwa mara muda mfupi tu baada ya kumkosa mkewe nyumbani." Alinukuliwa akisema mama huyo.

Kuanzia hapo Amber alikuwa ndiye shahidi muhimu katika kesi hiyo dhidi ya Scott. Amber alikubaliana na Polisi warekodi mazungumzo yake na Scott kwa njia ya simu wakati atakapojaribu kumdadisi ili akiri kuhusika na kupotea kwa mkewe, hata hivyo katika mazungumzo yaliyorekodiwa Scott hakukiri kuhusika na kupotea kwa mkewe. Kuanzia hapo Polisi walikuwa wakiendelea kumchunguza Scott kwa kufuatilia nyendo zake huku wakikusanya ushahidi.

Mnamo April 13, 2003, mtu na mkewe waliokuwa wakitembea na mbwa wao huko San Francisco kando kando ya ufukwe wa Richmond's Point Isabel magharibi mwa jiji la Berkeley waligundua mabaki ya mwili wa mtoto mchanga wa kiume ambaye alikuwa anaonekana hajafikisha umri wa kuzaliwa. Polisi walijulishwa na mara moja walifika katika eneo la tukio na kuchukua mabaki ya kichanga hicho.

Siku moja baadae mabaki ya mwili wa mwanamke aliyeonekana kuwa alikuwa mjamzito kabla ya kifo chake yaliokotwa maili kadhaa kutoka mahali yalipokutwa mabaki ya kichanga chake. Alikuwa amevaa gauni la cream wanalovaa wajawazito maarufu kama maternity. Sababu ya kifo chake haikuweza kujuliakana kutokana na mwili wake kutokamilika. Kwani mwili huo haukuwa na mikono yote miwili, unyayo wa mguu wa kulia haukuwapo na mguu wa kushoto kuanzia kwenye goti nao ulikuwa haupo.

Baadae taarifa ya uchunguzi wa kitabibu ulibainisha kwamba mwili huo ulikutwa na majeraha kadhaa, mbavu tatu zilikuwa zimevunjika ambapo ilielezwa kwamba inawezekana zilivunjika wakati au baada ya kuuawa. Hata hivyo iliripotiwa kwamba majeraha hayo hayakutokana na mwili huo kusukumwa na maji kutoka mahali ulipotoswa. Mwendesha mashtaka alisema kwamba kuna uwezekano Scott atakuwa alimnyonga marehemu au kumziba pumzi mpaka akafa. FBI na Polisi wa kituo cha Modesto walianza kufanya uchunguzi wa kitaalamu wakianzia nyumbani kwa wanandoa hao.

Scott Peterson alikamatwa rasmi hapo mnamo April 18, 2003 katika mji wa La Jolla hapo hapo katika jimbo la California akiwa katika eneo la kuegeshea magari katika uwanja wa kuchezea Gofu wa Torrey Pines, alipoulizwa sababu ya kuwepo katika eneo hilo alijibu kuwa alikwenda kuonana na baba yake na kaka yake kwa ajili ya kucheza gofu. Wakati alipokamatwa alikutwa na vifaa ambavyo havikuwa ni vya kuchezea gofu.

Alikutwana kiasi cha dola 15,000, simu za mkononi 4, alikuwa na kadi za malipo za kampuni tofauti tofauti za ndugu zake, vifaa vya kuwekea kambi porini na vifaa vya kupashia moto vyakula, turubai na vifaa vingine vya maji ya kunywa.

Alikutwa pia na viatu pea 4, nguo za kubadilisha, sururu ya kuchimbia, ramani iliyokuwa ikionyesha mahali alipokuwa akifanya kazi yule binti wa masaji Amber Frey, beleshi, kamba, paketi za dawa za usingizi , Viagra, na leseni ya udereva ya kaka yake.

Nywele zake zilikuwa zimebadilishwa rangi na kuwa za dhahabu, alipoulizwa kwa nini nywele zake zimebadilika rangi alidai kwamba ilitokana na kuathiriwa na kemikali za kwenye bwala la kuogelea la rafiki yake. Baaadae wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, rafiki yake alikanusha kumuona Scott akitumia bwawa lake la kuogelea.

Je huyu Scott Peterson ni nani?

Scott alizaliwa Octoba 24, 1972 huko San Diego jimboni California. Wazazi wake ni Lee Athur Peterson (alizaliwa Mei 9, 1939) na mkewe Jacqueline Helen Latham (Alizaliwa September 16, 1943). Baba yake alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni ya malori na baadae alianzisha shughuli zake mwenyewe. Mama yake anamiliki duka la mavazi katika eneo la La Jolla hapo hapo jimboni California linaloitwa The Put On.

Scott alisoma shule mbalimbali na vyuo mbalimbali na kuhitimu katika taaluma ya biashara kwa upande wa kilimo. Alifanya kazi katika mghahawa wa San Luis Obispo kama mhudumu. Ni wakati akiwa anafanya kazi hapo ndipo alipokutana na Laci Denise Rocha na hatimaye kuja kuoana hapo mnamo mwaka 1997.

Katika kesi hiyo Scott alikuwa akitetewa na mwanasheria mkongwe aliyetajwa kwa jina la Kirk McAllister. McAllister alikutana na Scott kabla ya kufikishwa makahakamani.

Alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Scott alimwabia Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Nancy Ashley kwamba hawezi kumudu gharama za kuajiri wakili wake mwenyewe atakayemtetea. Mwanasheria mwingine wa kumtetea aitwae Kent Faulkner aliteuliwa kumtetea katika kesi hiyo.

Hata hivyo Scott alimuajiri mwanasheria maarufu kwa kesi za mauaji aitwae Mark Geragos pamoja na madai yake ya kutokuwa na fedha za kuajiri mwanasheria wake mwenyewe, hivyo kuthibitisha kwamba anazo fedha.

Mnamo January 20, 2004, kutokana na kuongezeka vitendo vya kutishia maisha ya Scott katika eneo jiji hilo la Modesto, Jaji aliihamisha kesi hiyo kutoka katika mji huo wa Modesto na kuipeleka katika mji mwingine wa Redwood ulioko hapo hapo jimboni California.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa hapo mnamo June 2004 na ilikuwa ikifuatiliwa kwa karibu zaidi na vyombo vya habari.

Kesi hiyo ilikuwa ikiongozwa na mwanasheria aitwae Rick Distaso na Geragos aliongoza timu ya wanasheria waliokuwa wakimtetea Scott.

Kwa upande wa utetezi walidai kwamba upande wa mashitaka hauna ushahidi wa moja kwa moja wa kumtia Scott hatiani, na walikuwa na maoni kwamba kichanga kilichookotwa kilikuwa kimekamilika kwani kimezaliwa baada ya kutimiza miezi tisa na hakikufia tumboni kutokana mama yake kuuawa kama ilivyodaiwa na upande wa mashitaka. Upande huo ulidai kwamba Laci alitekwa nyara na kushikiliwa mpaka alipojifungua ndipo akauawa yeye na mwanaye na kutoswa baharini. Upande wa mshitaka ulileta wataalamu ambao walithibitisha kwamba kichanga hicho kilikuwa hakijatimiza umri wa kuzaliwa na kilikufa sambamba na mama yake.

Geragos alikuja na maoni mengine pale alipodai kwamba Wafuasi wa dhehebu la shetani ndiyo waliyemteka Laci na kumuua kama walivyomteka Evelyn Hernandez na kumuua kwa mtindo huo. Alisema kwamba anakubali kwamba Scott alikuwa na wanawake nje ya ndoa yake, lakini hiyo haihalalishi yeye kuwa muuaji.

Kwa upande wa mashitaka ulidai kwamba sababu ya Scott kumuua mkewe ni kwa sababu ya mahusiano yake na Mwanamke mtaalamu wa masaji aitwae Amber Frey na fedha. Mwendesha mashitaka huyo aliendelea kusema kuwa Scott alimuua mkewe kutokana na kuongezeka kwa matumizi na nia yake ya kuwa mseja (single) tena.

Kesi hiyo iliisha kusikilizwa kwake hapo mnamo March 16, 2005, ambapo Muheshimiwa Jaji Alfred A Delucchi alimhukumu Scott Peterson kunyongwa kwa kuchomwa sindano ya sumu hadi kufa. Jaji huyo alikieleze mkitendo cha mauaji alichikifanya Scott kuwa ni cha kinyama na kisichovumulika katika jamii. Aliamriwa alipe kiasi cha dola 10,000 kama gharama za mazishi ya mkewe Laci Paterson.

Hata hivyo Mwanasheria aliyekuwa akimtetea Scott, Geragos aliomba upande upelelezi makini wa mauaji ya Evelyn Hernandez ufanywe ili kubaini muuaji kwa sababu kuna uwezekano mkubwa kwamba muaji wa Evelyn ndiye aliyemuua Laci, kwa sababu mtindo uliotumika katika kutekeleza mauaji hayo unafanana. Mwanasheria huyo alikata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo, mama yake Laci, Sharon Rocha alisema kwa uchungu, "Ni nini ulichokifanya kuniulia binti yangu…. Laci alikupenda kwa moyo wako wote….. Umeamua kweli kuwaua Laci na mwenenu Conner na kuwatupa kama unatupa takataka.." Alisema mama huyo kwa uchungu, kisha akaendelea…

"Ukweli kwamba humuhitaji binti yangu Laci haukupi haki ya kumuua …. Ni binti yangu, na nilikuamini na umenisaliti, na umemsaliti kila mtu…."

Scott Peterson alipelekwa katika gereza la San Quentin akisubiri kutekelezwa kwa hukumu yake.
 
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Kama kawaida wapenzi wa safu hii ya kila Ijumaa yakesi zilizosumbua na kuleta utata, tunakutana tena leo kwa kesi hii ambayo inasikitisha sana lakini pia inafundisha.

Ni matumaini yangu kuwa wote tutaelimika kwa mkasa huu.
 
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Messages
7,459
Points
1,250
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined May 21, 2012
7,459 1,250
haya mambo yakuua huwa yananiumiza sana ndugu yangu sitakagi kuyasikia
 
Kunta Kinte

Kunta Kinte

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2009
Messages
3,692
Points
1,500
Kunta Kinte

Kunta Kinte

JF-Expert Member
Joined May 18, 2009
3,692 1,500
Hawa wazungu pamoja na kujidai wajanja lakini hawana lolote-yaani unauwa mke sababu tu ya kutaka kuwa na demu mwingine!!?? Waje huku kwetu unajipigia mademu wasio na idadi na mke bado unaye!!
 
cacico

cacico

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Messages
8,386
Points
1,250
cacico

cacico

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2012
8,386 1,250
hizi nyumba ndogo hizi!! demu ni mtaalamu wa massage!1 jamaa alinogewa kabisa mpaka akaona hapa ni kuua tu, typical devil! MUNGU ATUHURUMIE!
 
sosoliso

sosoliso

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Messages
8,461
Points
2,000
sosoliso

sosoliso

JF-Expert Member
Joined May 6, 2009
8,461 2,000
Kutokana na sheria kuwa msumeno kwa wazungu.. inafika wakati (evil minds) ina-justify kuua ili kukwepa kizingiti kimoja cha sheria na blindly kuingia kwenye mkenge mwingine wa sheria.. Imagine this.. umeoa na baada ya miaka kadhaa ya ndoa umekutana na mwanamke mwingine.. uka-fall hard kiaci akili ikasimama kufikiria madhara ya baadae.. Ukifikiria kuomba talaka kwa mke wako itakuwa ngumu.. mtifuano.. mapambano.. hatari ya kunyang'anywa children custody rights.. So kwa kuwa akili yako imekuwa dwarfed kwenye mahaba (crush) maamuzi ya haraka yanayokujia ni kumfutilia mbali huyo "obstacle".. Hapo ndio unapoanza ku-hatch the plot to kill ur partner.. Au kwa kusaidiana na mahaba wako mpya au alone..
Haya ndio mambo ya wazungu.. Naamini sheria zinawabana kiaci zinawalazimisha kuvunja sheria kubwa zaidi.. Na keci za aina hizi ziko nyingi sana.. Nyingi zinatatuliwa na muhucika kupata adhabu stahili.. But chache culprits get off the the hook.. Na hii si kwa wanaume tu.. Hata wanawake wanatenda sana uhalifu wa aina hii..
 
majany

majany

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2008
Messages
1,224
Points
1,225
majany

majany

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2008
1,224 1,225
But mi navyoona ni kama jamaa hakumuua vile....!!!!!Sijui lakini....hii kopi apelekewe Muke ya mzungu
 
Last edited by a moderator:
prianka

prianka

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2012
Messages
684
Points
195
prianka

prianka

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2012
684 195
jamani anyway kila mtu na hukum yake lkn
 
Jiwe Linaloishi

Jiwe Linaloishi

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Messages
3,736
Points
1,225
Jiwe Linaloishi

Jiwe Linaloishi

JF-Expert Member
Joined May 24, 2008
3,736 1,225
dah huruma kweli si angemrudisha tu kwao!!
kwakweli mtu aliyeuwa kwa kusudia ikithibitika na yeye kisu ningekuwa rais kila siku ningekuwa napitia hilo file niwe nazi sign
ila kwa hapa kwetu unaweza kunyonga hata wasiohusika, ila zombe nisingemuacha
 
M

Mponjori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2011
Messages
2,208
Points
0
M

Mponjori

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2011
2,208 0
Kuna uwezekano mkubwa kweli aliua,na pia kutokana na vitu alivyokutwa navyo,kuna uwezekano alitaka amuue kimada wake pia kutokana na maneno aliyomwambia kuwa mkewe alifariki wakati bado mzma!
Du inauma sana ni kama story kumbe yametokea..
 
M

Mponjori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2011
Messages
2,208
Points
0
M

Mponjori

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2011
2,208 0
dah huruma kweli si angemrudisha tu kwao!!
kwakweli mtu aliyeuwa kwa kusudia ikithibitika na yeye kisu ningekuwa rais kila siku ningekuwa napitia hilo file niwe nazi sign
ila kwa hapa kwetu unaweza kunyonga hata wasiohusika, ila zombe nisingemuacha
unanikumbusha waliomuua imran kombe walvyoachiwa.inauma sana ila mfumo wote umeoza..we need changes at top level
 
B'REAL

B'REAL

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2010
Messages
3,604
Points
2,000
B'REAL

B'REAL

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2010
3,604 2,000
Kama kawaida wapenzi wa safu hii ya kila Ijumaa yakesi zilizosumbua na kuleta utata, tunakutana tena leo kwa kesi hii ambayo inasikitisha sana lakini pia inafundisha.

Ni matumaini yangu kuwa wote tutaelimika kwa mkasa huu.
kamanda kwenye makala za kesi kesi uko vizuri...yani na hiyo avetor yako inaonekana walee waze wasomi big up
 
MESTOD

MESTOD

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
4,788
Points
1,500
MESTOD

MESTOD

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
4,788 1,500
God forbid, ila shetani akikuingia na ukamkaribisha kukwepa matamkwa yake ngumu kweli!
 
vanmedy

vanmedy

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Messages
2,432
Points
1,500
vanmedy

vanmedy

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2011
2,432 1,500
Mtambuzi sasa iliishaje.. Jamaa alishinda kesi au walimdunga sindano!? Daah hadi mesisimka aisee
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Messages
8,809
Points
2,000
Mtambuzi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined Oct 29, 2008
8,809 2,000
Mtambuzi sasa iliishaje.. Jamaa alishinda kesi au walimdunga sindano!? Daah hadi mesisimka aisee
Bado yuko jela anasubiri kutekelezwa kwa adhabu hiyo, kwa kawaida wanaohukumiwa kunyongwa nchini Marekani hukaa jela hadi miaka kumi wakisubiri kunyongwa..............
 

Forum statistics

Threads 1,404,969
Members 531,857
Posts 34,473,197
Top