Scania iko tayari kuleta mabasi yanaoyotumia gesi ya asili nchini Tanzania

Corporate News

New Member
Mar 11, 2020
1
1
SCANIA IKO TAYARI KULETA MABASI YANAYOTUMIA GESI YA ASILI NCHINI TANZANIA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Scania Tanzania Lars Eklund akizungumza katika mkutano na    waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu utayari wa kampuni hiyo kuleta mabasi    yanayotumia nishati ya gesi asilia ambayo ni bora kwa usafiri wa umma mijini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Scania Tanzania Lars Eklund akizungumza katika mkutano na

waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu utayari wa kampuni hiyo kuleta mabasi

yanayotumia nishati ya gesi asilia ambayo ni bora kwa usafiri wa umma mijini.

MBU_7928.JPG

Meneja Masoko wa Kampuni ya Scania Tanzania Eliavera Timoth akizungumza katika mkunato na

waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu utayari wa kampuni hiyo kuleta mabasi

yanayotumia nishati ya gesi asilia ambayo ni bora kwa usafiri wa umma mijini. Kushoto ni Mkurugenzi

Mtendaji wa Kampuni hiyo Lars Eklund.

MARCH 09, 2020. Dar es Salaam. Kampuni ya magari ya Scania Tanzania Ltd yatangaza kuleta mabasi yatumiayo gesi asilia ambayo ni bora kwa soko la Tanzania hasa kwa usafiri wa umma (Bus Rapid Transit). Bidhaa hii ni sehemu ya juhudi ya kampuni kuhakikisha inaongoza katika kuboresha sekta ya usafirishaji nchini. Kampuni ya Scania inaamini kuwa ni wakati sahihi kwa Tanzania kuingia katika mfumo huu na mingine kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu kimazingira na kiuchumi.

Tanzania ina akiba kubwa ya gesi asilia na inahitaji maelfu ya mabasi ya jiji kwa mfumo wa BRT ambayo kampuni ya Scania inaweza kuleta. Kampuni ya Scania imekuwa imefanikiwa kuleta magari ya mfumo wa gesi kwa muda mrefu sehemu mbalimbali duniani kama Amerika Kusini,Ulaya, na Australia.

Moja ya faida ya mabasi yanayoendeshwa na mfumo wa gesi asilia (Compressed Natural Gas) ni kwamba mfumo wake wa injini utasaidia kupunguza hewa chafu (Carbon dioxide) kwa asilimia 20 ambapo CO2 inatajwa kuwa ndio chanzo cha joto kali duniani, itapunguza gharama za uendeshaji, gharama kwa abiria na itaisaidia serikali kuongeza mapatoa kupitia uuzaji wa gesi asilia

Akizungumza na wanahabari katika ofisi kuu iliyoko Vingunguti kando na barabara ya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Scania Tanzania, Lars Eklund amesema Tanzania inaelekea kuwa nchi ya viwanda, hivyo ufanisi unahitajika na kwamba mazingira yasisahaulike.

‘‘Tunaamini ya kwamba Tanzania inahitaji kuwa na teknolojia mpya ili iendane na kasi ya nchi zilizoendelea. Tanzania ni tajiri sana kwa gesi asilia na ni muhimu kutumia nishati hii ya ndani kwa faida ya nchi, nchi itapata faida sana kwani itapunguza kiasi cha mafuta yanayoagizwa nje." na badala yake inaweza kuuza gesi ya ndani kwa waendeshaji wa ndani. Hakuna njia bora na ni ghari sana kujaribu kubadili injini ya dizeli kuwa injini ya gesi’’. Alisema Bwana Lars Eklund.

Kumekuwa na taarifa kupitia vyombo vya habari kutaka kubadili mfumo wa sasa wa magari ya BRT kutoka injini ya dizeli kwenda injisi ya gesi,suala hili halina tija kiufundi na kiuchumi kwasababu injini ya dizeli imeundwa kufanya kazi katika mzunguko wa dizeli wakati injini za gesi na petroli zinaendeshwa kulingana na kanuni ya Otto na ujazo wa kuziba cheche. Kwahiyo ni muhimu sana kuwepo kwa mipango bora ya upanuzi wa miundombinu ya gesi asili ambapo itasaidia wauzaji na waendeshaji kuthubutu kuwekeza katika bidhaa sahihi za gesi asilia zitakazotumiwa barabarani haraka iwezekanavyo. Alisema Bwana Lars Eklund.

Kama sehemu ya kukuza huduma zake nchini, kampuni ya Scania Tanzania inatafuta kushirikiana na taasisi mbalimbali za elimu kufadhili wanafunzi wanaochukua elimu kuhusu matumizi ya gesi asilia (Compressed Natural Gas). Hii itasaidia kuongezeka kwa idadi ya mafundi na wataalamu katika uwanja huo hivyo kuongezeka kwa msaada kwa watumiaji wa mabasi yenye mfumo wa gesi nchini. Mpango huu sio tu sehemu ya kujitolea kuboresha huduma lakini pia ni njia ya kurudisha fadhila kwa jamii zetu zinazotuzunguka. Alisema Bwana Eliavera Timoth,Meneja Masoko Scania Tanzania

KUHUSU SCANIA TANZANIA LIMITED

Kampunia ya Scania Tanzania inafanya kazi kama kampuni ndogo ya Scana CV AB yenye makao makuu yake nchini Sweden. Kampuni ya Scania Tanzania inajihusisha na uingizaji na usambazaji wa bidhaa za Scania nchini. Kampuni hii ina ofisi sehemu mbali mbali nchini
 
Back
Top Bottom