Scandal: Wakati Watanzania milioni 3 wana njaa, serikali inauza chakula Kenya!

Apr 20, 2011
28
29
Mashirika kadhaa ya misaada kwa jamii yametoa tahadhari ya kuwepo kwa dharura ya upungufu mkubwa wa chakula Tanzani na kusema zaidi ya watu milioni 3 nchini wanakabiliwa na njaa.

Wakati mashirika hayo yanaomba msaada wa chakula kwa Tanzania, serikali imesema kuwa Tanzania ina ziada ya chakula.

Serikali hivi karibuni ilitoa msaada wa chakula kwa Somalia na kuanza kuuza mahindi kwa Kenya kutoka kwenye hifadhi kuu ya nchi ya chakula (SGR), kumbe Watanzania milioni 3 wanakabiliwa na njaa!

Source: TANZANIA files
 
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: Mawasiliano Ikulu
Fax: 255-22-2113425





PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.

Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania na Kenya zimekubaliana kukomesha biashara ya miaka mingi ya magendo ya chakula kwenye mpaka wa nchi hiyo kwa kuamua kuuziana chakula rasmi kwa njia halali kuanzia sasa.

Kwa kuanzia, Tanzania imekubali kuiuzia Kenya tani 10,000 za mahindi ili kuiwezesha nchi hiyo kukabiliana na baa la njaa linalowakabili mamilioni ya wananchi wa Kenya hasa katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Makubaliano hayo ya aina yake baina ya nchi za Afrika yamefikiwa leo, Ijumaa, Septemba 9, 2011, mjini Nairobi, Kenya wakati wa mkutano kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mwai Kibaki wa Kenya.

Mkutano kati ya Rais Kikwete na Rais Kibaki umefanyika pembeni mwa mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa kujadili zahama ya ukame na baa la njaa katika nchi za Pembe ya Afrika uliomalizika leo mjini Nairobi.

Rais Kikwete aliwasili Nairobi jioni ya jana, Alhamisi, Septemba 8, 2011, kuhudhuria mkutano huo ambao kwa leo umewakutanisha wakuu wa nchi za eneo hilo kwenye eneo la Umoja wa Mataifa, Gigiri, nje kidogo ya Nairobi.

Katika mazungumzo yao, Rais Kikwete na Rais Kibaki, wametafakari faida za kuanzisha biashara rasmi ya kuuziana chakula baina ya nchi hizo mbili na umuhimu wa kukomesha magendo ya chakula ambayo imekuwa inafanyika kwa miaka mingi katika mpaka wa nchi hizo.

Katika miezi ya karibuni imekuwapo magendo makubwa ya chakula, na hasa mahindi, kutoka Tanzania ambako makumi kwa makumi ya malori ya chakula cha magendo yamekuwa yakivushwa mpaka kuingia Kenya ambayo baadhi ya sehemu zake zinakabiliwa na baa la njaa.

Kiasi cha wananchi milioni 3.7 wa Kenya, wakiwamo wakimbizi 477,000 kutoka Somalia wanakadiriwa kukumbwa na ukame na hivyo kuhitaji msaada wa chakula na misaada mingine ya kibinadamu kaskazini mwa nchi hiyo.

Chini ya makubaliano kati ya Rais Kikwete na Rais Kibaki, nchi ya Kenya itatakiwa kutathmini mara moja mahitaji yake ya chakula na kuiarifu Tanzania ambayo kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na hasa kupitia taasisi ya chakula cha akiba ya SGR itafanya maandalizi ya kuuza chakula hicho kwa Kenya.

Ujumbe wa Kenya unatarajiwa kuwasili nchini wiki ijayo ukiwa na takwimu za mahitaji yake tayari kwa mazungumzo na maofisa wa Tanzania wanaoshughulika na masuala ya chakula na biashara.

Katika mazungumzo hayo, maofisa hao pia watakubaliana utaratibu wa kukisafirisha chakula hicho, wasafirishaji wenyewe wa chakula na njia zitakazotumika katika kukisafirisha kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania kukipeleka Kenya.

Miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) Tanzania ni nchi pekee yenye akiba ya chakula, na hasa mahindi, wakati nchi nyingine zilizobakia za jumuia hiyo zinakabiliwa na njaa na ukosefu wa chakula kwa viwango vinavyotofautiana.

Tanzania imekuwa inajitosheleza kwa chakula kwa miaka mitatu iliyopita bila kulazimika kuagiza chakula kutoka nje na kimsingi hayo ni matokeo ya sera ya sasa ya Serikali ya kutoa ruzuku ya mbegu, mbolea, dawa za kuulia wadudu na mahitaji mengine ya kilimo kwa wakulima.

Ruzuku hiyo, kimsingi imekuwa inatolewa kwa wakulima kwa mikoa inayozalisha chakula, na hasa mahindi, kwa wingi. Ruzuku hiyo ilianza kutolewa kwa mikoa ya Iringa, Mbeya, Ruvuma na Rukwa hata kama mikoa sita inayozalisha chakula kwa wingi inashirikisha pia mikoa ya Morogoro na Kigoma.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

09 Septemba, 2011
 
Tanzania yakaribisha majirani kununua chakula

Na Mwandishi wetu
22nd July 2011

Huku janga la ukame likisambaa katika ukanda wa Afrika Mashariki na maeneo ya Pembe ya Kaskazini ya Afrika, Tanzania imefungua milango kwa akiba yake ya chakula ikitaka mataifa yanayohitaji chakula kuzungumza nayo moja kwa moja kupitia makubaliano ya kimataifa.

Ukame unaokabili ukanda huo unaelezwa haujawahi kutokea katika kipindi cha miaka 60 iliyopita.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika wa Tanzania, Prof. Jumanne Maghembe, akizungumza mjini hapa, alisema nchi jirani ambazo zianakabiliwa na baa la njaa zinatakiwa kujadiliana na serikali ya Tanzania moja kwa moja na wala si wakulima, wafanyabiashara au mawakala kwa ajili ya kununua chakula.

Prof. Maghembe aliliambia Shirika Huru la habari la Afrika Mashariki (EANA), kwamba nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo zinakabiliwa na njaa zinatakiwa kukutana na serikali badala ya kutegemea biashara za mpakani kupitia wafanyabiashara.

Alisema Tanzania ina ziada ya tani milioni 1.7 za chakula na kwamba serikali imekuwa ikifikiria kuuza ziada hizo kwa nchi jirani za EAC zinazokabiliwa na uhaba wa chakula.

Hatua hiyo ya serikali ya Tanzania inakuja wakati kuna taarifa ya uvushaji mkubwa wa nafaka kwa njia za magendo katika mpaka wake wa Kaskazini.

Polisi nchini Tanzania wanasema kwamba tani za metriki 400 kila siku zinavushwa kupitia mipaka ya mikoa ya Mara, Arusha na Kilimanjaro kupelekwa nchi za Kenya, Sudan Kusini, Somalia na Ethiopia.

Mikoa 16 (sawa na asilimia 76) ya nchi inakabiliwa na njaa na inahitaji msaada wa chakula cha dharura.

Nchi ambazo zinakabiliwa na hali mbaya ya chakula kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Pembe ya Kaskazini ya Afrika kutokana na ukame ni Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia, Kenya, Madagascar , Msumbiji, Somalia, Sudan na Uganda .

CHANZO: NIPASHE
 
Hii kashfa kubwa, serikali inadai kuwa ina ziada ya tani 1.7 milioni za chakula, mashirika ya misaada yanasema Watanzania milioni 3 wana njaa...
 
Hivi kila kitu humu kinaitwa kashfa mpaka neno hilo limepoteza maana halisi. Waziri ameonyesha wazi kwamba SGR ina ziada na ni lazima itumike kuwasaidia wale ambao hawana chakula. Sasa hiyo ni tofauti na kusema kwamba kuna watanzania milioni 3 ambao wanakabiliwa na uhaba wa chakula lakini siyo kwa sababu SGR haina salio la kutosha. Hapa unazungumzia usambazaji kutoka SGR kwenda kwenye maeneo yenye upungufu wa chakula. Kwa taarifa yako tayari serikali ilishatoa vibali vya kusambaza vyakula kwenda maeneo hayo yenye upungufu.

Hicho kinachoitwa kashfa kwa serikali ni creation ya wakosoaji wasio na malengo tofauti na yale ya detractors wengine waliosheheni humu na kule nje.
 
Kuna jambo halijaeleweka hapa. Ni kweli Tanzania ilizalisha chakula cha ziada, lakini kutokana na njaa kubwa iliyokumba nchi zote zinazoizunguka Tanzania -- DRC, Kenya, Somalia, Sudan, etc -- chakula hiki cha ziada chote kiliuzwa na wafanyabiashara wajanja kwa nchi hii kupitia mipakani. Kutokana na jambo hili, Tanzania sasa haina tena chakula cha ziada, badala yake ina uhaba wa chakula. Serikali haiko makini, haijafanya latest assessment kujua hali halisi ya chakula ikoje. Wangefanya wangegundua kuwa chakula cha ziada hakipo tena na sasa kuna ubaba mkubwa wa chakuka. Serikali inatakiwa iache kugawa chakula kwa Somalia na kuuza Kenya kwani wananchi wake wenyewe wanakabiliwa na njaa.

THIS IS A MAJOR SCANDAL!
 
Kweli wewe ni kichwa nazi. Serikali ndiyo yenye SGR na inajua maghala yetu yana kiasi gani. Sasa wewe kama unazungumzia wakulima binafsi kuuza chakula kwa njia za panya hiyo haimaanishi kwamba akiba ya chakula, ambayo ndiyo inayozungumziwa na serikali baada ya kutathmini hali ya chakula kwa sasa. Utofautishe kati ya maeneo kukumbwa na njaa kwa sababu ya chakula kutosambazwa na njaa inayotokana na ukosefu wa chakula kabisa. Kilichopo hapa ni kutosambazwa kwa chakula. Kama wewe hujui what a scandal is basi usidandie hoja hapa.
 
Back
Top Bottom