Sayari nyingine saba sawa na Dunia zagunduliwa

Kuna chombo cha exploration kinaitwa Kepler pia kimeshagundua maelfu ya sayari na nyota (kama jua) mpya huko kwenye anga za mbali.. Skuiz hadi kwenye ma tv humo kama mfatiliaji wa vipindi vya nat geo au discovery science channels wanaonyesha sana tu.. Ukigoogle tu exoplanets utakutana na nini wenzetu wanafanya wakati sisi tunahangaika na siasa..
 
Mkuu hizo sayari zilizogunduliwa zipo nje kabisa na mfumo wetu wa jua(solar system).. Pluto iko ndani ya mfumo wetu wa jua so hizo sayari zipo mbali mno.. Ukifuatilia utajua kuwa hizi sio sayari za kwanza kugunduliwa kuna mifumo yenye sayari inaitwa Kepler ina sayari nyingi tu zinazofanana na dunia na kuna moja ndo imelingana kwa karibu kila kitu sawa na dunia(wanaitwa twin Earth) inaitwa Kepler 186f (ipo 500 light years away) ila zote zipo mabilion ya kilomita huko na iliyokaribu nakumbuka ni kama 40 light years away.. Sasa 1 light year kumbuka ni umbali ambao mwanga unasafiri kwa mda wa mwaka mmoja sasa pigia mara 40...
Kepler-186f - Wikipedia
Umu jf kuna watu very smart aisee
 
MKuu neno sayari lipo siku nyingi tu huo ni muendelezo wa kuona na kuona kitu si ugunduzi, wewe umewahi kuona vingapi ! hivyo wewe ni mgunduzi au? Sikatai uzi wako ila tofautisha kuona na kugundua.

labda kama hujui maana ya neno 'kugundua'.
na inawezekana kabisa unachanganya neno ugunduzi (detection) na neno uvumbuzi (invention) yaani kugundua na kuvumbua.
jipange
 
labda kama hujui maana ya neno 'kugundua'.
na inawezekana kabisa unachanganya neno ugunduzi (detection) na neno uvumbuzi (invention) yaani kugundua na kuvumbua.
jipange
Kweli kabisa.. Mtu unaweza kugundua kitu ambacho kilishavumbuliwa ila kilifichwa(kukiona_detecting) ila huwezi kuvumbua kitu ambacho kilishavumbuliwa.. (invention)
 
Nasikia Kuna Sayari moja Kati ya mpya zilizogunduliwa Viumbe hai wataishi Milele, sasa wanahangaika Na mchakato WA kupeleka Binadamu huko!
 
Haha mkuu habitable earth like planet zipo tena nyingi tu ishu ni jinsi ya kuzifikia maana zipo umbali wa billiion light years yaani safari ikianza sasa hata baada ya vizazi kumi mpaka mia bado hatutavifikia kwa vyombo hivi tulivyonavyo sasa.
Kutokana na hili la kutoweza kuzifikia, haimaanishi uchunguzi wa anga za mbali ndio ukome la hasha bali kuna mengi yenye faida na yanayoinfluence uwepo wetu hapa duniani.
 
Allah anasema "“Allah is He Who created seven Firmaments and of the earth a similar number…”
[Quran 65.12]
 
Mnazikumbuka hadithi za alifu lela ulela???? Basi jamaa akatembea mpaka kiatu cha chuma kikaisha usiku na mchana kwa miaka 7..............,Sayari ipo umbali ambao mwanga unasafiri miaka 40??????? sisi acha tudeal na nanihino kwanza hayo hayatuhusu kwa sasa.
 
View attachment 473548

Wataalamu wa masuala ya anga za juu wa Marekani wakishirikiana na wengine duniani, wamefanya ugunduzi mkubwa wa sayari saba zenye ukubwa sawa na wa Dunia ambazo zinaizunguka nyota mojawapo kama ilivyo kwa dunia kulizunguka jua.

Wanasayansi hao wa anga za mbali kutoka Marekani, Uingereza na Ubelgiji, wamebainisha kuwa sayari hizo saba walizozigundua zinaizunguka nyota ijulikanayo kwa jina la Trappist One.

Hata hivyo wanasayansi hao wamesisitiza kuwa kwa teknolojia iliyopo sasa inaweza kuwachukua maelfu ya miaka kuzifikia sayari hizo.

Thomas Zurbuchen kutoka shirika la NASA lenye makao yake makuu Washington nchini Marekani, amewaambia waandishi wa habari kuwa haya ni mafanikio hayo ni makubwa kisayansi na yanajibu maswali makubwa ya kisayansi

"Ugunduzi huu unatupatia vidokezo muhimu vya kuitafuta 'dunia ya pili', na kwamba sasa si jamba la kusema kama ingelikuwa hivi, bali sasa tunasema ni lini. Wanasayansi wanaamini kwamba takribani katika kila nyota moja kuna uwezekano wa kuwepo sayari moja. Chukulia sasa nyota tatu, nne, tano hadi saba, jiulize ni idadi ya dunia ngapi zilizopo pale,'' amesema Zurbuchen.

Michael Gillion ni mmoja wa wanajopo hilo la wana sayansi kutoka chuo kikuu cha anasema sayari tatu kati ya hizo saba zilizogundiliwa zipo karibu na nyota hiyo na zina sifa tofauti.

"Inaonyesha kuwa sayari hizi tatu kati ya hizo saba zilizogunduliwa zipo katika ukanda unaoweza kuruhusu viumbe kuishi, kwani maji yanaweza kupatikana na maisha ya viumbe hai yanaweza kuendelea, chakushangaza zaidi ni kwamba maisha yanaweza kuwepo hata katika uso wa sayari hizo," amesema Gillion.

Ugunduzi huu unatajwa na wanasayansi hawa kuwa ni mafanikio makubwa na umewaingiza katika ukurasa mwingine na kubakiwa na swali moja tu kwamba ni lini watazifikia sayari hizo badala ya kujiuliza kuwa katika anga hillo kuna nini.

Hata kuzifikia sayari hizo ni mtihani mwingine wani umbali wake hata mwendokasi wa mwanga, unaoongoza hapa duniani kwenda kwa haraka, unaweza kuzifikia sayari hizo baada ya miaka 40.

Chanzo: BBC
SAHIHISHO:
Ziko umbali wa 40 million LIGHT YEARS.
Mbali. mbali sana sana.
Sijui kwa kiswahili tutatafsrije
 
Ina maana zipo mbali zaidi ya Pluto? Mbona kuna kifaa kilishafika pluto kwa miaka minne na speed inayoizidi speed ya light.
Au wanadhani tumesahau?
Pluto iko kwenye nyota yetu(jua)ina maana kuifikia hiyo sayari kwanza tuhame kutoka kwenye ulimwengu wetu tuhamie kwenye jua /nyotq ya hiyo sayari tajwa!
 
basi utakuta na hao watu wa sayari nyingine huko nao wamegundua kuwa kuna sayari 9 huku kwetu na wao wanafanya mpango waje watuone eti!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom