Sayansi ni msingi wa maendeleo Serikali iwekeze zaidi

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
2,000
Maendeleo katika nchi nyingi duniani yametokana na kuwekeza vya kutosha ktk sayansi na teknolojia kwa watu wake.Serikali iwekeze sana tafiti,walimu,maabara,miundo mbinu ya ufundishaji sayansi toka shule za awali mpaka vyuo vikuu,malipo mazuri kwa wanasayansi n.k ktk uelekeo huu wa nchi ya viwanda.Itafika mahali muda nchi itakuwa na vitu vingi vinavyotengenezwa ndani ya nchi,huduma za kiafya zilizobobea kufanyika nchini,kuwa na maabara kali na za kisasa za kupima magonjwa mbalimbali kwa muda mfupi na karibu na wanainchi,na hata kuanza kurusha setelite anga za juu lakini juu ya yote kuweza kutumia au kuprocess madini mbalimbali tuliyokuwa nayo kuwa bidhaa kuliko kuuza kama raw materials.Watunga sera,sheria,kanuni na taratibu za nchi ni jambo la kupanga tu na kupanga ni kuchagua.Hongera kwa wanafunzi wa kidato cha sita 2016 matokeo yanaonesha kuwa sayansi tunaiweza pale tu tukiamua kuipa kipaumbele.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom