‎Sayansi NaTeknolojia‬ Njia ya kuepusha akili bandia kuhatarisha binadamu yatafitiwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
akli feki.jpg
Roboti.jpg
Maroboti.jpg



#‎Sayansi NaTeknolojia‬ Njia ya kuepusha akili bandia kuhatarisha binadamu yatafitiwa

Watu wengi wana wasiwasi kuwa kama akili bandia inaweza kuhatarisha maisha ya binadamu hata kuwaua au la. Kampuni ya Google DeepMind iliyobuni software ya AlphaGo imesema itasanifu swichi ya kuzima akili bandia mara moja, ili kuepusha hali inayoelezwa mara kwa mara katika filamu za sayansi ya kubuni(sience fiction) kwamba roboti zikishamiri sana zitawaua binadamu wote.

Tasnifu iliyotolewa na kampuni hiyo inasema akili bandia inaweza kujifunza yenyewe, baadhi ya wakati inaweza kufanya vibaya. Binadamu anahitaji swichi ya kuizuia isifanye vitendo vya hatari. Jambo muhimu kwa swichi hiyo ni kwamba ingawa akili bandia inaweza kujifunza mambo mengi, lakini haiwezi kujifunza namna ya kuwazuia binadamu kubonyeza swichi hiyo.

Akili bandia inaweza kutafuta njia rahisi ya kutimiza malengo, lakini binadamu hawawezi kujua jinsi akili bandia inavyofikiri. Njia rahisi si nzuri katika hali yoyote, kwani inaweza kuleta matokeo mabaya kwa binadamu.

Mtaalamu wa taasisi ya mustakabali wa binadamu Dr Stuart Armstrong aliwahi kusema lugha za binadamu zina maana nyingi, akili bandia pengine inaweza kuzielewa kwa njia isiyo sahihi. Binadamu wakitoa agizo la kuwazuia watu wasiishi katika maisha yenye

uchungu, lakini akili bandia pengine itafikiri ni agizo la kuwaua binadamu wote; na roboti ikipata agizo la kuhakikisha usalama wa binadamu, huenda itawafunga watu wote. Mtaalamu huyu alisema ni lazima binadamu wabuni akili bandia salama haraka ili wasije wakachelewa kuzuia mambo mabaya kutokea. chanzo.CRI Kiswahili
 
Itakuwa vizuri maana kama robots are programmed to self learn n.k hio pia ni threat kwa binadam.
 
Back
Top Bottom