Sayansi imethibitisha mwanaume akiwa na sifa hizi 10 huwa na mvuto zaidi kwa wanawake

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
x7-ways-to-let-him-know-your-interested-3.jpg.pagespeed.ic.2TyfcTBKJ2.jpg

1. Sura Nzuri

Muonekano mzuri kwa mwanaume huwa ni kigezo cha kwanza katika maamuzi ya mwanzo kwa mwanamke lakini hata hivyo huwa ni katika mapenzi ya muda mfupi tu zaidi ya yale yanayodumu.

2. Ucheshi

Ucheshi kwa mwanaume si muhimu tu kama wenyewe bali humfanya mwanaume aonekane mwenye akili

3. Mwanaume anayetoa msaada


Wanawake hupenda wanaume wanaotoa msaada, wasio wachoyo pale wanapotafuta uhusiano wa muda mrefu

4. Utajiri/Uwezo wa kifedha


Ile imani kuwa wanaume wenye uwezo wana mvuto zaidi kwa wanawake ni kweli. Utafiti ulionesha kuwa wanawake huona wanaume wanavutia zaidi pale wanaposimama tu kwenye magari ya kifahari au nyumba, hata kama vikiwa sio vyao.

5. Umri Mkubwa

Wanawake hupenda wanaume wenye umri mkubwa kwasababu mara zote huamini kuwa wamekusanya vitu vingi na uzoefu katika maisha.

6. Ndevu


Ndevu zimekuwa zikichukuliwa kama zinazokera na kuvutia kwa wakati mmoja – yote hutegemea na mapenzi ya mtu.

7. Wagumu

Wakati utafiti wa zamani unasema kuwa wanawake huvutiwa na wanaume wanawaopenda, tafiti mpya zimedai kuwa kujifanya mgumu, kutojali kunawavutia wanawake. Kifupi, wanaweza kutaka kile wanachodhani hawawezi kupata.

8. Tafiti zinaonesha pia kuwa wanaume wenye mbwa huwavutia wanawake. Duh!

9. Wanawake kwenye tamaduni zote wameonesha kuvutiwa na wanaume wanaovaa rangi nyekundu

10. Wanawake wamethibitishwa pia kuwapenda wanaume majasiri na wasiogopa
 
Ongezeko:
-1 Utafiti wangu pia umeonyesha wanawake wengi huwapenda wanaume warefu...na si kina anduche..
-2Utafiti wangu pia umeonyesha yote yaliyosemwa hapo juu yanakuwa applicable kwenye nchi za Ulaya na America huko ila kwa hapa Bongo ni Pochi yako tu hata kama we ni kibogoyo utavuta mzigo wa maana mbya na watakugombania pia...
 
Zote mbwembwe tu hapo, hakuna dawa ya wanawake inayozidi pesa,
Kuwa na sura baya kama mimi hapa Lakini uwe na noti uone,
Mfano mdogo tu Diamond wa tandale na huyu Baba tiffa wako sawa?

Pesa ndo Kila kitu
 
Watakuwa wanawake wa zamani hebu warudie tena utafiti wao wa kizazi hiki,naamini hakuna kizuri kuliko pesa na hakuna mwanamke asiyetaka pesa..pesa ndo kila kitu bro
 
Nimeachana na wanawake kadhaa hiv kisa siwahudumii na huyu mwngne nw ugomvi kila kukicha anaomba pesa ila kiukwel mimi ni mbahil sana nataka kujiweka sawa kwanza kiuchumi ndio maana sihongi ila huwez kuishi bila kuila papunch najikuta natongoza na jins nilivyo lazma akubali nina kigezo no:1 sasa ikifka hapo no4 demu lazma asepe maana anaona analiiwa bila kula hiyo no4 inapaswa iwe no1 nikijichukulia km mfano na tutafute pesa ndugu zangu vyote vitakuja lasivyo ukubali kugongewa na wenye pesa
 
Back
Top Bottom