Say no to piracy, nunua software, game na movies original

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
This is toomuch yaani karibu kila computer ninayoiona hapa bongo windows yake ipo pirated yaani imechakachuliwa itumiwe bure bado haitoshi karibu kila software kuanzia IDM, Photoshop, dc-unloacker, microsoft word zote nazo zimechakachuliwa ilimradi tu mtu asilipie,

Ukienda hadi kwenye games hali ni ile ile ukitaka kucheki movies bado unakuta tita la pirated movies, haya sasa antivirus ambaye ni ulinzi wa computer bado nayo imechakachiliwa.

Wakuu hivi vitu vya bure its too much, say no to piracy at least ununue hata antivirus genuine, ikumbukwe kuwa hizi software na games zimetengenezwa kwa jasho linaohitaji kufutwa kwa pesa utayotoa ukizinunua, so guys my point ni kwamba tupunguze piracy at least uwe na hata software moja tu hata anti virus iwe genuine.
 
Bajeti ya Kompyuta na Software zake;

Laptop-600,000 (Mtumba) nimekuta ina Old Windows na nataka Mpya.......

Windows mpya-150,000 hadi 250,000 (Makadirio tu)

Ulinzi(Ant-Malware)-15,000 hadi 40,000(Makadirio tu)

Office MS-100,000-400,000 (Kulingana na aina)

Software nyingine, zisaidie katika matumizi ya kila siku;

Video, Photo n Audio editor,viewer na burning prog. bora-angalau kwenye 400,000 hivi zote kwa pamoja

Games za missions, sports na nyingine nyingi-400,000 kwa mpya kuanzia 5, zamani kuanzia 10 hivi

Bado vijisoftware vidogo vidogo kama idm,archivers prog. ,DJ prog., vpn prog. , torrent prog. , pdf ,data recovery prog. , na kwa wale wanaotumia Win 8 kuna apps zinauzwa kwa store kule.

Nimesahau hizi prog za tiatia huruma a.k.a kudonate.

Unatimiza yote hayo halafu System Inakorofisha......................
 
kwa mujibu wa torrentfreak wanaoongoza kupirate ni marekani, uingereza, australia, nchi za asia, hii ni kuanzia movies, tv shows, softwares na vinginevyo. sisi huku afrika kwanza internet tu ni tatizo, kwa kifupi ni asilimia ndogo sana inayoweza kupirate huku afrika hasa tanzania.

sababu kubwa za kupirate ni upatikanaji wa bidhaa, mie ukiniuliza bei ya windows siijui. season premier ya game of thrones ilisababisha server za hbo kuzima baada ya kuzidiwa, watu hawakuwa na jinsi zaidi kuingia kat.ph

sababu ingine ni uwepo wa pirate sites, yani huwezi niambia ninunue huku naona kitu kipo bure. nani asiependa bure?

method of payment ni tatizo, mtanzania wa kawaida ni cash au mobile payments, sasa ntanunuaje sasa?

cracks, na njia za kubypass kulipia nyingi zinatoka mbele, sisi tunatunatumia tu coz vipo... in real sense sisi tunasindikiza tu ila wezi wako ulaya huko

zipo sababu nyingi, mi sishabikii wizi wa kazi za watu, uwa nanunua nnapoweza na nnatumia open source softwares pale nnapoweza.
 
Kwa namna ambavyo wamarekani na wachina wanavyofanya piracy ya rasilimali za afrika ni lazima nasie wenye maunjanja tupakue tu expensive software, books na electronic resources zao, at least at individual level. Sio jambo jema lakini inapunguza machungu...
 
Tunajikuna tunapoweza.....mi naona poa tuh cuz kihalali hatuwezi kuafford, kuchakachua kwa pirate poa tuh ukizingatia makampuni uliyoyataja tayari yana profit za kutosha duniani
 
shiny c

Turud kwanz kwako mkuu hadi leo hii ushawah nunua windows au Ms office? I know jibu litakua HAPANA.

Mi binafsi cwez nunua ki2 kama windows kwa 150,000-400,000 wakat zipo za free tena znafanan na hzo za kuuzwa.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo unaniambia ninunue Cinema 4D kwa $4000?? au Unity kwa $1500... software za muhimu zote zina bei mtanzania wa kawaida unamuumiza..

Hata nje wanachakachua wanaonunua ni maprofessional wanaokula hela ndefu au makampuni.

Software ambazo huwa nalipia sanasana ni za mobile, android nimelipia nyingi tu price yake iko very low...
 
Kwa upande wangu sijaona NO kwenye matumizi ya softwares/applications zote za computer isipokuwa YES pekee. Kwa kipato changu na mahitaji ya matumizi ya technolojia katika maisha yetu, bado nitatumia vya kupakua bure sana tu. Games ndo aijawahi waza hata kidogo kununua ama kudhania nitakuja nunua.

Afadhari yako Dreson4 wewe unanunua za android ambazo mimi hata hizo natumia zilizokuwa cracked! Marekani waliipakua The Expendables 4 kabla hata haijazinduliwa ikashusha mauzo sembuse bongo!!!!!!
 
Mkatanyasi

Sometimes support si mbaya ukizingatia kama mobile games zenyewe dollar mbili tatu, mimi mwenyewe developer najua ugumu wa kutengeneza game na ikahit hasa sehemu kama Android na iOS store ambapo only 1% ya top apps ndo wanatengeneza pesa....

Huu uchakachuaji ndo sababu developers wengi wanakuja na freemium model siku hizi afu wanawajazia matangazo
 
Ombenichelsea,

Mbadala wa microsoft office ni libreoffice...ni open source na ina kilakitu kama microsoft!! by the way nataka iweka kwenye pc nianze itumia!!!

This is toomuch yaani karibu kila computer ninayoiona hapa bongo windows yake ipo pirated yaani imechakachuliwa itumiwe bure bado haitoshi karibu kila software kuanzia IDM, Photoshop, dc-unloacker, microsoft word zote nazo zimechakachuliwa ilimradi tu mtu asilipie,
Uko sahihi, ila kuna ubuntu!! nadhani hii ni chaguo bora hasa kama huwezi nunua windows!!
 
Last edited by a moderator:
kwa hiyo unaniambia ninunue Cinema 4D kwa $4000?? au Unity kwa $1500... software za muhimu zote zina bei mtanzania wa kawaida unamuumiza.. Hata nje wanachakachua wanaonunua ni maprofessional wanaokula hela ndefu au makampuni.
Ngoja niichukulie post hii kama mfano.

Tatizo watu wanapenda vya gharama ilhali mfuko mdogo. Mfano $4000 kwa anayeitumia C4D kwa kusudi halisi la developer sio kubwa maana atapata faida mara myingi sana ya hiyo fedha. Kwa kazi nyingi wanazofanya Wengi (non commercial kuna alternative nyingi tu.

Nitaweka baadhi
  1. MS Office Suite -- LibreOffice/Apache OOo
  2. Maya and Co -- Blender
  3. FL Studio -- LMMS
  4. CakeWalk et al -- Ardour/Audacity
  5. Photoshop -- Gimp
  6. Zend Studio -- Eclipse/Netbeans PHP

Utaona karibu essentials zote zina alternative. Non essentials kama game zipo pia ingawa sijui extent (Not a gamer). Kama unataka vya kulipia, lipia.
 
Stefano Mtangoo,

Unajua mkuu tatizo ya hizo softwares nyingine ni support, kama LibreOffice ni sawa, lakini Blender ukijaribu hata kujifunza hupati resources nyingi kama ilivyo software kama 3DS Max,

Mfano mimi textures zote za sprites zangu hua natumia photoshop, na any graphics related sababu ndo kitu nimekaa nacho miaka kama kumi sasa, kuanza kujifunza kingine ambacho sio equally powerful itanichukua miaka tena kufikia nilipo sasa...

Kazini natumia paid softwares sema nikibeba project kuja nayo nyumbani au freelance job yoyote most times hamna jinsi.. Afu still najua haya makampuni mengine yanaacha kubana sana security wakijua fika kua watu hasa wanaotaka kujifunza hizi software wanacrack,

Mwisho wa siku mtu akiwa expert kama anataka kufanya hiyo kua kazi yake atanunua.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom