say NO kwa serikali 3; YES, to Permanent residency or dual citizenship for Zanzibaris | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

say NO kwa serikali 3; YES, to Permanent residency or dual citizenship for Zanzibaris

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by JokaKuu, Jan 4, 2011.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  ..binafsi sioni umakini ktk hoja ya kuwa na serikali 3. siamini kama hicho ndicho ambacho wa-Zenj wanahitaji kwa sasa hivi.

  ..vilevile naamini serikali 3 zitaongeza mzigo wa matumizi haswa kwa upande wetu wa-Tanganyika.

  ..zaidi sidhani kama ndani ya hiyo serikali ya muungano kutakuwa na maelewano. bado tutaendelea kuwa na magomvi ya wa-Zenj kujiona wanabanwa ktk mambo yao.

  ..wa-Tanganyika wanaona haya kuuvunja muungano. wanaogopa wataonekana watu wenye roho mbaya miongoni mwa jamii. kisingizio ni kwamba hawataki kuvunja undugu uliojengeka wakati wa uhai wa muungano, na hata kabla ya hapo.

  ..sasa kwa kuzingatia ukweli huo hapo juu, bora wa-Zenj waliopo bara sasa hivi wapewe status ya Permanent residency kwa kipindi fulani, na pia iwepo nafasi ya wao kuomba uraia kamili ikiwa watakuwa na nia hiyo.

  ..kwenye masuala ya sarafu, tunaweza kuanzisha a currecy board, kama chombo cha mpito. napendekeza hivyo kwasababu kuna mipango ya kuwa na sarafu ya East Africa.

  ..naamini wakati umefika kwa wa-Zenj kujiamulia mambo yao mengi zaidi, bila ya kuingiliwa na wa-Tanganyika.
   
 2. M

  MLEKWA Senior Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muheshimiwa Joka unaanza kututafuna Wazanziabri hata Muungano haujavunjika au ndio uko mbioni kuvunjika kina Tindu Lisu hawautaki ?
  Wazanzibari wamejaa tele Dubai , UK Maputo , Den Mark , USA , Toronto , ugiriki , South Afrika Zanzibar ni nchi ndogo ila wako kila kona ya Dunia haki zao tunazijua vyema.
  Zanzibar suala la Sarafu sio siri iliwahi kuvujishwa Sarafu ya Zanzibar mitaani kabla ya mfumo wa Vyama vingi kama huyajui hayo waulize wajuvyi watakupa na picha ya hiyo sarafu ilionea kwa wanaharakati wa miaka ya 80. Hilo ni National issue ya Zanzibar na ndio World Bank wakaunda tume wakati wa Dr BEN Mkapa na ndio ukaona leo Zanzibar wanapata angalau visenti kutoka BOT kwani BOT iliundwa kwa pesa za Wazanzibari na Watanganyika zilizotoka kwenye Bodi ya sarafu ya Afrika Masharikiwakati aMkapa alipokua Mbogo kusema Zanzibar haina haki kwenye BOT
  Ukisikia enzi za DR Omar na DR shein kwenye umakamo walipokua wakizungumza matatizo ya Muungano moja ni hili.

  Yako mengi tu ambayo leo hii Zanzibar inajiandaa kujiunga na jumuia ya Afrika MAshariki stay tuned if you are not well informed. Na huko musije mukasema ni Kuvunja muungano ni kuimarisha Muungano kwani Tanzania yenye serikali tatu itakua na votes mbili kwenye East African community hiyo ni nguvu za makaka wawili Tanganyika na Zanzibar.
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  MLEKWA,

  ..tunaweza kuvunja muungano, lakini hatuwezi kuvunja undugu na mashirikiano ya miaka nenda rudi kati ya wa-Zenj na wa-Tanganyika.

  ..kwa maoni yangu, muungano unatumbukiza "nyongo za kisiasa" ktk undugu baina wa-Zenj na wa-Tanganyika.

  ..ndiyo maana mimi napendekeza siasa ziwekwe pembeni na ubakishwe UNDUGU.

  ..tufungue zama mpya za undugu baina yetu kwa kuwapatia hadhi ya permanent residency au dual citizenship ndugu zetu wa Zanzibar.

  ..kama Zenj wataona ni vyema kuwa na SARAFU yao na iwe hivyo. kama watataka kuwa na sarafu moja na Tanganyika pia wasiwekewe pingamizi.

  ..kuhusu suala la kura ktk East African Community, naamini suala hilo lizingatie maslahi ya nchi husika[Tanganyika au Zanzibar] na lisiongozwe na historia yetu kwamba tuliwahi kuwa nchi moja.
   
 4. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Articles of Union zinatambua kuwa ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ni makosa ya kuzoeleka ati serikali ya Tanganyika ndiyo ilijisalimisha kuwa Tanzania. Wa Zanzibar mbona wanakomalia serikali yao hata mipaka? Kwa hiyo italeta maana tu iwapo serikali ya Tanganyika itakuwepo hapo ndipo tutakuwa na serkali ya Muungano.

  Gharama za kuendesha serkali si Tatizo. Dawa ni kuondoa uoza wa kupeana vyeo wa chama Tawala. Nakupa kutokana na uzoefu wanaofanyakazi serikalini si zaidi ya asilimia tano. Watu wanashinda wanacheza karata kwenye komputa. Halafu kazi zenyewe ni mpaka ije crisis ndipo utaona kila mtu yuko bize.

  Wazanzibar (guo guo) wana uhuru wa kuvinjari bara, ila watakabiliwa na upinzanini kwa kutaka kuinfluence mambo ya Tanganyika. Yaani Chao ni chao na chetu ni chao. Hapo patachimbika.

  Mbona wameunda serikali ya kiana huko kwao na huku bara wanajiita wapinzani. It is awkward and unrealistic. Mimi nitajitolea kufanya kazi bila malipo angalau kuwajenga vijana kiwa miaka miwili kwa ajili ya serikali ya Tanganyika.

  I am saying YES kwa serikali 3; YES to Permanent Residency for either party in their borders NO to duel citizenship for Zanzibaris kwanza wana vitambulisho vya uraia huko kwao.
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Unaongea vizuri sana lakini hapo kwenye red naona jazba zilikuzidi nguvu. kama Tanganyika au Tanzania itakuwa na sheria ya dual citizenship basi itakuwa na vigezo na yeyote atakaetimiza vigezo na masharti basi hatobaguliwa kupata dual citizenship.

  Usijenge hisia kuwa wenzetu wa zenj ni wakorofi. Nilivyowafahamu ni kuwa wanapigania haki yao ndani ya muungano ambao unaendeshwa kimabavu mabavu. Pia kama Joka Kuu alivyosema kuna udugu wa kidamu wa miaka na miaka kati ya Nchi hizi mbili,Tanganyika na Zanzibar. Mimi nimesema kama tungebakia na jina la awali, Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar basi tungekuwa tunajadili chachu ya mambo ya msingi ya muungano kuliko hivi ulivyo mkorogo leo.

  Pili, vitambulisho vya uraia kwa Zanzibar haviko.Au vimekuja karibuni? Hapa unapindisha ukweli mkuu, vitambulisho vilivyotolewa Zanzibar ni vitambulisho vya mkaazi Zenj na vinatumika kwa ajili ya Ushiriki wa Chaguzi za ZEC.
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Joka Kuu,

  Kule ulikoibua ile article ya Katiba haina baraka ya wazanzibari,
  kuna articles nzuri zenye hoja...kama Tanganyika ipo kisheria na nyengine tutekeleze mkataba wa Muungano.
  mimi hutembelea pia huko na unakutana na hoja ambazo zinakufanya ufikiri vipi sehemu hizi mbili zinavyoutizama Muungano.

  Joka Kuu, Likija shirikisho la afrika mashariki unafikiri kutakuwa na serikali ngapi? Au umesahau kuwa huo mchakato upo? Kila territory itakuwa na serikali ya ndani na ile ya shirikisho, au vipi?

  Niliwahi kusikia hotuba moja ya Jusaa akisema kuwa kuna mambo ambayo yamo katika makubaliano ya Afrika mashariki lakini si mambo ya mUUngano kwa hiyo alikuwa analalamika kuwa Zanzibar inakosa kuwakilishwa huko na Tanganyika inawakilishwa katika mambo yasio ya Muungano na serikali ya Muungano. nafikiri kuna hitilafu nyingi katika muungano wetu na zikikosa kusawazishwa basi huko siku za mbele tunakaribisha matatizo ambayo si ya lazima.
   
 7. M

  Mesaka Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  kwanza nadhani maana ya muungano haukueleweka na haujaeleweka vizuri! mimi ninavyo jua maana ya muungano ni kwamba vitu zaidi ya kimoja huungana pamoja ili kuwa kitu kimoja, tofauti na Ushirikiano/ shirikisho ambako kila kimoja hubaki kilivyo zaidi ya kukubaliana mambo ya kushirikiana.

  Hivyo tunapoongelea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa Tanzania (ambapo ukweli ni Tanzania + Zanzibar) si dhani kama ni muungano halisia, nasema hivi kwa maana kwamba kama ungekuwa muungano halisi tungekuwa na serikali moja ya Tanzania, wala kusengehitajika kuwa na serikali nyingine (serikali ya mapinduzi Zanzibar) ndani ya serikali. Nchi zikiungana sharti ibaki nchi moja. Huo ndiyo muungano.

  Nionavyo mimi ili tuwe na muungano wa kweli, basi yatupasa tuwe na nchi moja yenye serikali moja. Kuwa na serikali mbili au tatu, kamwe naamini hakuna muungano. Ila kwa serikali mbili au tatu basi tuite serikali ya shirikisho.

  Nchi yetu ni kubwa mno, kwa mapendekezo yangu Tuunde Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayo gawanywa ki-majimbo, Zanzibar ikiwa mojawapo ya Jimbo. Wanzibari kama watabaki kung'ng'ania serikali yao nitajua ni wabinafsi.

  Nawasilisha yangu,

  Good Day to all
   
 8. N

  Nonda JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mesaka,

  Huu msimamo wako ni msimamo wa sisi huku Tanganyika ambao pia tunashindwa kuikubali Zanzibar kama nchi tuliyoungana nayo kwa baadhi ya mambo tu. Hiki ni kipengele ambacho kweli inaonekana sisi watanganyika wengi hatutaki kukiona na kukielewa.


  Tanganyika na Zanzibar hazikuungana kwa maana ya nchi moja, ndio maana hadi Nyrerere anakufa still kuna mambo ambayo hayajafanywa ya Muungano. Mimi ninapofikiria sana naona ugumu uko wapi kwa wazenji kukubali Nchi moja serikali moja. Ni kukataa kumezwa katika Muungano unaoendeshwa kuhuni huni tu, kimaguvu na siyo kwa ku-nigotiate baina ya members wa Muungano.

  Zanzibar wana population max. 2 million. Tanganyika 39mil. Pili wewe pia unaona Zanzibar ni ndogo na haistahili hata kuwa mkoa. Unasahau kuwa duniani kuna nchi ndogo ndogo nyingi tu kama Mauritius, Seychelles, Maldives, Cape Verde, Equatorial guinea nk na zinajitawala zenyewe na hakuna anayewambia uwe jimbo au mkoa.

  Kuna kitu kinaitwa Muungano wa nchi za ulaya(European Union) .Huu unaitwa umoja wa ulaya na sio shirikisho la Ulaya. kwa hiyo, ufahamu unatupiga chenga sisi Watanganyika. Wazanzibar wanajua vyema kitu gani wanazungumza na wanataka. Sisi ndio hatutaki kuwafahamu.

  Kimfumo , Tanzania ilipaswa iwe ni shirikisho. Hata jina lake la asili linaashiria hivyo, Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sote tunajuwa kuwa kuna mambo exclusively ya Tanganyika, Kuna mambo exclusively ya Zanzibar na kuna mambo exclusively ya Muungano(Tanganyika na Zanzibar kwa pamoja). Sasa niambie nchi moja inawezekanaje katika hali hii? Na hivyo ndivyo Mkataba wa muungano unavyosema.
  Ubaya wa mambo ni kuwa hata huu Mkataba wa Muungano umefanywa kuwa ni siri kubwa, basi hata copy kuwekwa makumbusho ya Taifa ili watu wajionee hiyo hati haifanywi. Kunafichwa kitu gani?

  Anyway, watanzania tumezoea kuongozwa kama kondoo, lakini katika hili la Muungano viongozi wetu wamekuwa wasiri sana sijui ni kwa faida ya nani!!???
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,982
  Trophy Points: 280
  Nonda,

  ..Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda nchi moja, dola moja,Tanzania.

  ..uthibitisho wa hilo ni ukweli kwamba ktk medani ya kimataifa, Tanzania ndiyo inayotambuliwa, siyo Tanganyika au/na Zanzibar.

  ..muungano wetu ni unique, hivyo ukiulinganisha na muungano mwingine wowote ule utaishia kuchanganyikiwa akili tu.

  ..historia ya Zanzibar, pamoja na udogo wake kiidadi na kieneo, imekuwa ni kikwazo cha kuelekea kuwa na nchi moja serikali moja.

  ..matatizo tuliyonayo hayawezi kuisha kwa kuundwa kwa serikali 3, yaani serikali ya Shirikisho la Tanzania, itakayokuwa juu ya serikali za Tanganyika, na ile ya Mapinduzi Zanzibar.

  ..tutatumia hoja gani kuwa-convince wa-Tanganyika milioni 40 kwamba wao ni sawasawa na wa-Zanzibari milioni 1.5? hivi mnafikiria historia peke yake kwamba Zanzibar ilikuwa dola kamili sawa na Tanganyika inatosha kujenga hoja ya usawa?

  ..I dont see Zanzibar gaining anything kwa kuanzishwa kwa serikali ya shirikisho. sana sana ni sisi wa-Tanganyika ambao tutapatiwa serikali inayofafana na ile waliyonayo wa-Zanzibar sasa hivi.

  ..serikali 3, au muungano wa shirikisho, ni kutuongezea walalahoi layer nyingine ya watawala, bila kujibu maswali na matatizo ya msingi ya muungano wetu.

  ..ninachowaomba wachangiaji wenzangu ni kwamba tuangalie hata solutions ambazo hazijapendekezwa bado. wazungu wanasema "thinking outside the box."

  ..tudumishe undugu na ujamaa kati ya wa-Zenj na wa-Tanganyika ktk masuala ya KIJAMII na KIUCHUMI, bila kufungamana kisiasa. Tanganyika iwape permanent residency wa-Zenj wote walio na makazi ktk ardhi yetu, pia utaratibu uanzishwe wa kuwapatia dual-citizenship. baada ya hapo muungano[wa kisiasa] uvunjwe na tuendelee kuwa majirani wema.

  NB:

  ..Zanzibar waachiwe waamue wenyewe kama wanataka kuwa member wa EAC au la.

  ..sitarajii kama nchi za Afrika Mashariki zitakuja kuunda dola moja yenye serikali moja ya shirikisho.

  ..hata kama hilo litakuja kutokea basi Zanzibar waachiwe waamue wenyewe kujiunga au la.
   
 10. M

  Masonjo JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 2,725
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Itakuwa vigumu sana kwa serikali ya Tanganyika yenye almost 98% ya ardhi ya Tanzania na about 97% ya raia wa Tanzania kukubali kuiheshimu na kuipa stahiki yake serikali ya Muungano ambayo kwa kiwango kikubwa hivi ni Tanganyika na hivyo kupelekea kuvunjika kwa Muungano huu.

  Nadhani solution nzuri ilikuwa ni kuundwa kwa serikali moja lakini kwa kuwa zanzibar haielekei kuwa tayari kulikubali hilo nafikiri solution pekee iliyobaki ni kuimega Tanganyika na kuunda majimbo ndani yake na hivyo Federal Republic of Tanzania iwe na majimbo ya Zanzibar, Jimbo ya Kanda ya Ziwa, Jimbo la Kanda ya Kati, Jimbo la Kanda ya Mashariki, Jimbo la Kusini na Jimbo la Nyanda za Juu Kusini,nadhani hii itakuwa ni solution ya kudumu kuliko hizo zingine.
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  "..Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda nchi moja, dola moja, Tanzania."…

  Inawezekana kabisa kuwa kijina inaonekana hivyo,lakini jee wakati nyerere na karume wapo hai, muungano uliendeshwa kama nchi moja ,dola moja?

  Kama ni hivyo kwa nini serikali ya zanzibar iliendelea kuwepo wakati wote ambao karume alikuwa kiongozi huko Zanzibar?

  Pili, kuna hii kauli kuwa mkataba uliweka kikomo.kuna member hapa JF hivi karibuni alidokeza kuwa ulikuwa uwe renewed kila 10years kama pande zote, yani Tanganyika na Zanzibar zingeridhia na inatajwa kuwa sababu moja ya Karume kukutana na mauti. Kama hoja hii ina ukweli basi definitely haiwezekani kusema muungano uli-envisage nchi moja ,dola moja, serikali moja.

  Tatu, Zanzibar ilikuwa na hali nzuri kiuchumi wakati huo na ilikuwa ikiongozwa na kiongozi asiye na elimu ya kutosha, aliongoza kwa ubabe tu, na kila aliyemuona tishio kwa utawala wake alipotezwa. Lakini katika kuingia makubaliano na nyerere Karume hakumshirikisha Mwanasheria mkuu wa serikali ya Zanzibar Jaji Dourado. Kwa hiyo Karume hakuwa akizuiliwa na yeyote ,hata Nyerere kufanya lile alilolitaka kuhusu Zanzibar. Muungano haukuathiri utendaji wa serikali ya karume. Yeye alijua kuwa ana nchi yake na Nyerere ana nchi yake ndio maana ile kauli uliyoikariri,"azimio la Arusha mwisho chumbe" ni kiashiria cha huo msimamo wake!

  JokaKuu,
  Mimi naamini kugeuza jina asilia la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa (Tanzania) pia imeongeza utata katika kulipoteza jina Tanganyika, pamoja na serikali yake na katiba yake kwa mambo ambayo si ya Muungano. Sioni "uniqueness" ya muungano huu, ninachokiaona mimi ni ujanja wa msomi Nyerere, dhidi ya Mbabe Karume. Alichofanya Mwalimu ni sawa na kuiba kwa kutumia kalamu kwa kumtia hofu Karume. Ushahidi ni kuwa Mwalimu aliwachukua wale wasomi wote akawapa nafasi katika serikali ya muungano na wale aliowaona kuwa asingeweza kuwashawishi kukubaliana naye katika mpango wake akawapeleka zanzibar kuuawa.

  Tafsiri ya serikali tatu pia ilikuwa tafsiri ya Jumbe, akina seif Sharif, salmini Amour sasa hii tafsiri ya nchi moja ,dola moja ,serikali moja iko huku Tanganyika tu?
  Katika kuanzisha taasisi za muungano Zanzibar ilikuwa inachangia kama member wa muungano na pia katika kuanzisha mashirika ya umma Zanzibar ilikuwa ina-share katika mashirika hayo , hiki ni kiashiria chengine kuwa Tanzania haikutarajiwa kuwa nchi moja, dola moja, serikali moja. Mkuu, huu muungano tulionao hata sijui ni kitu gani?
  Mimi naona tuna-delay matatizo tu ambayo ni lazima yatakuja pale tutakapolazimisha serikali moja.

  Mambo ya kufikiri nje ya box, tunaweza kufanya mimi na wewe lakini viongozi wetu wako kuelekea nchi moja,dola moja,serikali moja bila kujali athari zake.

  Mkuu, serikali ya shirikisho la Afrika mashariki linakuja, halikwepeki kutokana na mchakato wa EAC ,la muhimu ni kujitayarisha vizuri tu ,ili tuwe na uwakilishi mzuri siku litakapokuja. Tusije na sisi kullamika kama wanavyolalamika wazenj.
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Jan 6, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  JokaKuu,

  Umeiona hii?

  http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27
   
Loading...