Sauti ya Power Lufunga kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Elice Elly

Elice Elly

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
1,146
2,000
SIKIA SAUTI YA POWER LUFUNGA KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA* 2019.

Na Power Lufunga, the living philosopher;

UCHAGUZI Ni Jambo la heri, nalo Ni jema hivyo washiriki Wote, wale wanaonyukana kupigiwa kura, wanaopiga kura na mamlaka zinazoratibu uchaguzi yawapasa kuliheshimu Jambo Hili Ni kuliendesha kwa mujibu wa taratibu za wazi zilizowekwa na Bila hisia binafsi Wala upendeleo wala uonevu wowote kwani kwa kufanya hivyo, demokraisia na viongozi makini wanaopendwa na wengi hupatikana na hiyo ndiyo iletayo maendeleo na amani.*

Kuyapuuza mambo hayo maana yake Ni baadhi ya Vyama kujitutumua kukiuka kanuni aidha kwa msaada wa vyombo vya dola ama kwa utashi wa wanachama wake, aidha mamlaka za uchaguzi kuwa sehemu ya baadhi ya wagombea, mambo haya ndiyo huua demokrasia, viongozi makini wanaopendwa na wengi hutangazwa kwa hila na ushetani kuwa wameshindwa na huu ndio uchochezi hatari Sana katika jamii iliyostaarabika. Tuyaache haya.

Nukuu hizi, busara za Mwana wa Lufunga, zijenge nchi yetu sasa;

1. Hakuna Viongozi Safi bila mazingira na mifumo safi ya kuwapata, kwa maana aliyetokana na rushwa, unafiki na hila hawezi kuukana uovu kwani ili kuisema ile kweli itambidi ajikane Kwanza yeye mwenyewe*

2. Hakuna Uchaguzi huru na wahaki wenye usawa, Utu na kuvumiliana bila kuwa na tume huru isiyopokea ama kushiriki amri za serikali ama baadhi vyama vya siasa vinavyonyukana.

3. Hakuna upinzani imara wenye mikakati yenye kurekebisha kasoro za watawala bila kuwa na wananchi imara wasio na Usakatonge, unafiki na ubinafsi wa kumulika manufaa binafsi.*

4. Upinzani imara na Hatari Ni ule utakaotokana na mwanafamilia atakayeasi akaungana na washindani, huyo ndiye ajuaye mikakati na nyenzo za chama hivyo atasumbua Sana atakapohamia upande wa pili.

5. Kiongozi bora, mgombea Bora wa chama atatokana na wanachama wenyewe kwani wao ndio wajuao falsafa Yao, Hali Yao Kisiasa na ushindani wanaokabiliwa nao, kwa maana chama kingine Ni Kama adui, adui hawezi kukupangia kikosa imara ili umwangamize mwenyewe.

6. Nguvu ya Nani awe kiongozi katika jamii ya kidemokrasia iko kwa wananchi, hivyo mchochezi na mchafuzi wa amani pekee Kipindi Cha Uchaguzi Ni yule ajaribuye kuipora haki hii ya waliowengi kwa kulazimisha kuwatangaza ama kuwaapisha washikaji waliokataliwa na wananchi kwenye masanduku ya Kura*.

7. Uchaguzi Ni Haki na jukumu muhimu Sana kwa wananchi ili kuweza kujipatia viongozi watakaoweza kusimamia shughuli za maendeleo Yao, mwananchi kususia uchgauzi hupenyesha mianya kwa washikaji wasio na sifa kupata nafasi za kusaamulia mambo yenu and hivyo kuumiza jamii na taifa kwa ujumla.

8. Wapinzani siyo maadui, serikali siyo adui, mtu kuwa upinzani ama chama kinachoongoza serikali haimaanishi ndiye Bora ama asiyefaa; kinacho mata hapo Ni Nani amegombea katika chama chenye sera zipi, ana Nini kichwani mwake na ana mpango gani kwetu akipata nafasi hiyo, tusitafute nafasi kwa mabomu ama maandamano, sanduku la kura liwe huru kutuamlia matakwa ya wengi*.

9. Katika Uchaguzi kila mmoja huwaza kushinda, Bali palipo na washindani lazima mmoja tu ndiye ataibuka mshindi hivyo ukichaguliwa mshindi Basi usiwabeze uliowashinda Bali wapongeze kwani ndio waliokufanya kuwa mshindi na pasipo wao, kukubali Kushindwa ama kushiriki shindano usingekuwa mshindi. Nawe unayeshindwa, kukubali Kushindwa Ni hekima na Jambo la kiungwana.

10. Je Wewe Ni mgombea ama mpiga kura?, Umejiandaaje kushindana kishiriki Uchaguzi? Je umetegemea figusu na mbinu za kutangazwa kiuonevu Hata Kama utashindwa ama kuandamana na kuvuruga Chaguzi ukidai kuibiwa kwa kura?

kushinda ama Kushindwa ikiwa ni kwa halali siyo agenda kwa maana yapo maisha baada ya uchaguzi, tafadhali tuheshimu natutimize wajibu wetu kwa maslahi mapana yetu na vizazi vyetu*

Tafakuri jenzi na ndivyo Mwana wa Lufunga natua pen;


POWER LUFUNGA@THE VERY CRITICALLY ARGUING FORESIGHTED LIVING PHILOSOPHER*

Email address; *lufungapower22@gmail.com*

Facebook. *//Power Lufunga//*

Phone. *0622263599*.
 
state agent

state agent

JF-Expert Member
Jul 1, 2019
1,777
2,000
Huu uchaguzi hata kabla haujaanza chadema wapinzani wamesha weka mpira kwapani

CCM inakwenda kuwapiga kipigo cha paka mwizi

State agent
 
Top Bottom