Sauti ya Mnyonge!

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
Watanzania wenzangu,

Uchaguzi umeisha na sasa tunajiandaa kuanza safari ndefu ya miaka mitano, kwa ukweli safari hii binafsi naiona ni ndefu sana kiasi nahisi kukata tamaa mapema hasa nikiwakumbuka watanzania maskini walioko vijijini na hawa wa mijini wanaoishi chini ya dola moja.

Katika safari hii hakuna tena kuvaa kofia wala fulana za ushabiki wa vyama, ni safari ndefu ya kavu kavu ambayo sasa tunavuna tuliyoyapanda. kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.

Tulitegemea kupata dereva mpya lakini ni yule yule, shida ni zile zile, wasafiri sisi ni walewale, matatizo yaliyokuwepo tulivyoanza safari mwaka 2005 ni yale yale na yatakizidi kuwa magumu hasa kwa wenzetu wa vijijini,(waliokaa siti za nyuma) naamini kabisa hakutakuwa na changes zozote zile bali kufunga mikanda kuanzia Jumatatu hii. Kwa wazazi wenye watoto wawili / watatu kama huwezi kuwasomesha Private basi tena, mzigo wote umeachiwa wewe na wakati huo huo tuombe mungu apunguze maradhi kwa watoto wetu maana hospitali za serikali madawa hakuna.

Nikiangalia list ya viongozi wetu tuliowachangua juzi ni wale wale, sioni nuru mpya ya kunipa matumaini, moyo umefifia nahisi kufa kufa vile. Sioni raha ya kitu cha kujivunia katika nchi yangu kusema ukweli, ubinafsi wa viongozi wetu umezidi kiasi watu wenye nafasi zao wanajifikiria wenyewe tu.

Nuru kidogo naiona kwa viongozi wachache (60 Wabunge wa Upinzani) ambao wanatutetea sana lakini matumaini si makubwa sana kwani hawatashirikishwa katika uundaji wa serikali, kwa hiyo hoja zao zitawekwa makapuni bila sababu za msingi.

Safari hii kufikia 2015 naona ni ndefu sana, jua ni kali na mchanga umechemka mno ukizingatia hatuna hata kandambili miguuni. natamani kurudi nyuma nitafute kivuli nipumzike lakini haiwezekani.

Mungu wangu waingie hawa watu wanaoapiswa kesho watukumbuke sisi wananchi tulio maskini hasa kwenye elimu, makazi na afya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom