Sauti ya Mama wa Liwale na Dada wa Morogoro si za kupuuza

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,218
25,630
Kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku huu kupitia ITV,kuna sauti mbili kutoka vijijini ambazo hazipaswi kupuuzwa. Wote wawili wanawalaumu wanasiasa kuwatumia wakati wa uchaguzi na kuwasahau uchaguzi unapoisha.

Mama wa kutoka kijijini huko Liwale Lindi,kijiji chenye shida kubwa ya maji,amesema na kumaliza na swali. Amesema wananchi wa vijijini huwa mbele sana kwenye uchaguzi na kutumika,kwanini husahauliwa uchaguzi unapoisha? Mama wa Liwale aliongea kwa uchungu mkubwa.

Dada wa kimasai wa Morogoro aliyekuwa akizungumzia migogoro ya wakulima na wafugaji, ametumia maneno ya wananchi kupewa kisogo baada ya uchaguzi. Dada huyo wa Morogoro amesema kuwa wakati wa uchaguzi,wananchi hujazwa ahadi za kufanyika hili au lile. Uchaguzi unapopita wananchi hao hupewa kisogo.

Sauti hizi zinabeba ujumbe mzito kisiasa. Kwamba hata wananchi wa vijijini sasa wameanza kujua kuhusu kutumiwa kwao wakati wa uchaguzi. Wanasiasa myajue haya na myafanyie kazi.
 
Liwale wamechagua Mbunge wa CUF wakitaraji kuwa atawaletea maji. Sasa imekuwaje tena wameanza kulia lia?
Mbunge ni Mwakilishi wa wananchi ambae anawatumikia wananchi kwa kufikisha kero na matatizo yao serikalini kwa hiyo Ujumbe serikalini ushafika Ila tatizo la Serikali yetu imekuwa ikibana sehemu wanazotawala wapinzani ili kesho ije kuonekana wapinzani hawajafanya kitu ila tutakomaa na ninyi mpaka kieleweke.
 
Mbunge ni mtanzania kama alivyo mtanzania yeyote. Utekelezaji wa miradi ni jukumu la serikali iliyopo madarakani. Tusiaminishwe kuwa mbunge analeta maendeleo....
 
Tuache uchama mama Tanzania tumuweke mbele ujumbe huo hauna chama tafadhali usitaje chama fulani kwa ajili ya kujipatia ushawishi jadili hoja sio chama. Kama ni mapungufu kwenye majimbo na utekelezaji wa sera + ahadi chama hakikumtuma mwakilishi kuwasusa wananchi wake tuwe makini.
 
Hata huku Monduli tumechagua machadema lkn hamna mabadiliko yoyote . maji hakuna ,barabara shida, maji hakuna hali imekuwa mbaya zaidi.
 
Liwale wamechagua Mbunge wa CUF wakitaraji kuwa atawaletea maji. Sasa imekuwaje tena wameanza kulia lia?
Ndugu kila siku huwa nakwambia uelewa wako wa mambo ni mdogo sana,
Hvi umeelewa hoja hapo? Tafadhali usiuache uchi ubongo wako namna hii,

Mana hujui hata kama RC ni mtumishi wa umma au la.
 
Kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku huu kupitia ITV,kuna sauti mbili kutoka vijijini ambazo hazipaswi kupuuzwa. Wote wawili wanawalaumu wanasiasa kuwatumia wakati wa uchaguzi na kuwasahau uchaguzi unapoisha.

Mama wa kutoka kijijini huko Liwale Lindi,kijiji chenye shida kubwa ya maji,amesema na kumaliza na swali. Amesema wananchi wa vijijini huwa mbele sana kwenye uchaguzi na kutumika,kwanini husahauliwa uchaguzi unapoisha? Mama wa Liwale aliongea kwa uchungu mkubwa.

Dada wa kimasai wa Morogoro aliyekuwa akizungumzia migogoro ya wakulima na wafugaji, ametumia maneno ya wananchi kupewa kisogo baada ya uchaguzi. Dada huyo wa Morogoro amesema kuwa wakati wa uchaguzi,wananchi hujazwa ahadi za kufanyika hili au lile. Uchaguzi unapopita wananchi hao hupewa kisogo.

Sauti hizi zinabeba ujumbe mzito kisiasa. Kwamba hata wananchi wa vijijini sasa wameanza kujua kuhusu kutumiwa kwao wakati wa uchaguzi. Wanasiasa myajue haya na myafanyie kazi.
Wao ndo magala ya kura za kijani. Watakula walipopeleka mboga
 
Mbunge ni mtanzania kama alivyo mtanzania yeyote. Utekelezaji wa miradi ni jukumu la serikali iliyopo madarakani. Tusiaminishwe kuwa mbunge analeta maendeleo....
na serikali hiyo hiyo inapompa mbunge hela za mfuko wa jimbo 100m ni kwa ajili ya nin? miradi midogo ya maji hata visima anashindwa kuchimba??. nashukuru watu washaanza kuelewa, wanasiasa hawapo kwa ajili ya sisi wapiga kura. ni kwa maslahi yao tu. si ccm wala ukawa. wote wale wale,
 
Hawa ndio mtaji mkubwa wa chama chetu, maji ndio ajenda muhimu ya kupatia kura wakati wa kampeni, ukisolvu tatizo utapata wapi mahindi mengine ya kuwadangania kuku? Waendelee kukata mauno na ule wimbo wa chama mbogamboga.
 
Back
Top Bottom