Sauti Kutoka Khartoum

lidoda

JF-Expert Member
Apr 27, 2008
641
574
SAUTI KUTOKA KHARTOUM SUDANI
.
Nilifika hapa Sudani mwaka jana mwezi wa nane, na kama tujuavyo nci hii iko ktk vita ya mda mrefu. Nilikuja kwa sababu mke wangu anafanya kazi UN na ilibidi nije nikae na familia yangu hapa. Tunaishi hapa Khartoum na hali ya hapa kwa mda wote haikuonyesha kabisa kama kuna vita na kama huangalii vyombo vya habari kama BBC,CNN,ALJEZIRA na vinginevyo utadhani kuwa nchi hii inafanyiwa propaganda na nchi za magharibi na kutaka kuchafua jina la Sudani.

Kuna watanzania kama 100 ambao wanaishi hapa hawana passporti na hawana hata nauli ya kurudi nyumbani Tanzania. Hawa hapa wanabaguliwa kwa sababu ni wageni. Walikuja hapa kama mabaharia. Wengine wanasimulia walikuwa wakitupwa ktk Port Sudani na mwishowe wakaja mpaka huku Khartoum, wengine walitokea Egypty nk.
Kuna wengine wamekata hata tamaa na matokeo yake wanakunywa pombe kali na kutumia madawa ya kulevya kusudi tu wasahau ugumu wa maisha. Watu wengi wamekufa na wamezikwa hapa sababu hawana uwezo wa kurudisha maiti nyumbani. Kiufupi hawa walikuwa ni watafutaji kama wengine walioko nchi mbalimbali za Ughaibuni na hapa wengine walikuwa wanatumia kama ni transit ya kwenda Ughaibuni. Kuna hawa mabaharia wamekaa hapa miaka 15 mpaka miaka 30 na wameoa na wana watoto.

Asante, kwa watanzania wanaofanya kazi ktk UN, ambao wanatoa msaada wa hali na mali, wamewasaidi kuwalipia nauli baadhi ya watanzania na wamerudi nyumbani. Lakini mzigo bado ni mkubwa, na msaada bado ni mkubwa unahitajika ambao hawa jamaa wa UN hawataweza kuwasafirisha. Kalibu wote wangetaka kurudi nyumbani lakini hawana hela.

Bahati mbaya hapa Khartoum hakuna ubalozi wa Tanzania na hivyo hakuna msaada wowote unaopatikana kwa matatizo mbalimbali, ijapokuwa Tanzania kuna ubalozi wa Sudani pale DSM. Kulikuwa na ubalozi wa Tanzania hapa Khartoum, lakini sababu ya kisiasa ikabidi ufungwe.

Lakini hali iliokuwa jana ilibadilika kabisa hapa. Kuna kundi ambao wanaitwa lebels(JEM)kutoka Darfur ambao walifika mpaka nje ya Khartoum na kuanza kushambulia sehemu sensitive za usalama. Tuliambiwa tusitoke kuanzia saa 11 jioni jana jumamosi mpaka leo Jumapili asubuhi saa 4. Haijulikani kama mda utaongezwa. Jana tulikuwa tukisikia mizinga na mabomu ya kipigwa huko na hakuna magari yakitembea sababu ya hali ya hatari ambayo imetangazwa. Kutoka ktk eneo la vita mpaka hapa tunapoishi ni umbali kutoka City center Dar mpaka Ubungo.Nafikiri mkiangalia ktk BBC,CNN na Aljezira mtaziona hizo habari.

Wasiwasi mkubwa ni kwa hawa Watanzaia wengine amabao hawana passport na hawana nauli ya kurudi Bongo. Mie na familia yangu tunaweza tukapelekwa nchi zilizo kalibu ya hapa, Misri,au Sudani au Kenya nk.

Kuna mtu yeyote anaweza akajua tunawezaje kuwasaidia hawa ndugu zetu?.Yaani wapate msaada wa kurudi Tanzania moja kwa moja?
 
SAUTI KUTOKA KHARTOUM SUDANI
.
Nilifika hapa Sudani mwaka jana mwezi wa nane, na kama tujuavyo nci hii iko ktk vita ya mda mrefu. Nilikuja kwa sababu mke wangu anafanya kazi UN na ilibidi nije nikae na familia yangu hapa. Tunaishi hapa Khartoum na hali ya hapa kwa mda wote haikuonyesha kabisa kama kuna vita na kama huangalii vyombo vya habari kama BBC,CNN,ALJEZIRA na vinginevyo utadhani kuwa nchi hii inafanyiwa propaganda na nchi za magharibi na kutaka kuchafua jina la Sudani.
Kuna watanzania kama 100 ambao wanaishi hapa hawana passporti na hawana hata nauli ya kurudi nyumbani Tanzania. Hawa hapa wanabaguliwa kwa sababu ni wageni. Walikuja hapa kama mabaharia. Wengine wanasimulia walikuwa wakitupwa ktk Port Sudani na mwishowe wakaja mpaka huku Khartoum, wengine walitokea Egypty nk.
Kuna wengine wamekata hata tamaa na matokeo yake wanakunywa pombe kali na kutumia madawa ya kulevya kusudi tu wasahau ugumu wa maisha. Watu wengi wamekufa na wamezikwa hapa sababu hawana uwezo wa kurudisha maiti nyumbani. Kiufupi hawa walikuwa ni watafutaji kama wengine walioko nchi mbalimbali za Ughaibuni na hapa wengine walikuwa wanatumia kama ni transit ya kwenda Ughaibuni. Kuna hawa mabaharia wamekaa hapa miaka 15 mpaka miaka 30 na wameoa na wanawatoto
Asante, kwa watanzania wanaofanya kazi ktk UN, ambao wanatoa msaada wa hali na mali, wamewasaidi kuwalipia nauli baadhi ya watanzania na wamerudi nyumbani. Lakini mzigo bado ni mkubwa, na msaada bado ni mkubwa unahitajika ambao hawa jamaa wa UN hawataweza kuwasafirisha. Kalibu wote wangetaka kurudi nyumbani lakini hawana hela.
Bahati mbaya hapa Khartoum hakuna ubalozi wa Tanzania na hivyo hakuna msaada wowote unaopatikana kwa matatizo mbalimbali, ijapokuwa Tanzania kuna ubalozi wa Sudani pale DSM. Kulikuwa na ubalozi wa Tanzania hapa Khartoum, lakini sababu ya kisiasa ikabidi ufungwe.

Lakini hali iliokuwa jana ilibadilika kabisa hapa. Kuna kundi ambao wanaitwa lebels(JEM)kutoka Darfur ambao walifika mpaka nje ya Khartoum na kuanza kushambulia sehemu sensitive za usalama. Tuliambiwa tusitoke kuanzia saa 11 jioni jana jumamosi mpaka leo Jumapili asubuhi saa 4. Haijulikani kama mda utaongezwa. Jana tulikuwa tukisikia mizinga na mabomu ya kipigwa huko na hakuna magari yakitembea sababu ya hali ya hatari ambayo imetangazwa. Kutoka ktk eneo la vita mpaka hapa tunapoishi ni umbali kutoka City center Dar mpaka Ubungo.Nafikiri mkiangalia ktk BBC,CNN na Aljezira mtaziona hizo habari
Wasiwasimkubwa ni kwa hawa Watanzaia wengine amabao hawana passport na hawana nauli ya kurudi Bongo. Mie na familia yangu tunaweza tukapelekwa nchi zilizo kalibu ya hapa, Misri,au Sudani au Kenya nk
Kuna mtu yeyote anaweza akajua tunawezaje kuwasaidia hawa ndugu zetu?.Yaani wapate msaada wa kurudi Tanzania moja kwa moja?

Lidoda,
Poleni sana huko Sudan. Hili ni suala gumu na nafikiri ingekuwa rahisi zaidi ukawasiliana na ubalozi wa Addiss Ababa, (251-1) 511063, 612904, 518155. Jaribu kuwapigia halafu usiache kutufahamisha maendeleo yenu.

Haya mambo ya stoaways inabidi yatafutiwe dawa. Ndgu inabidi wabebe gharama za kuwarudisha ndugu zao au wakopeshwe na serikali, maana ni suala linaloongezeka hivi sasa.
 
Lidoda,
Poleni sana huko Sudan. Hili ni suala gumu na nafikiri ingekuwa rahisi zaidi ukawasiliana na ubalozi wa Addiss Ababa, (251-1) 511063, 612904, 518155. Jaribu kuwapigia halafu usiache kutufahamisha maendeleo yenu.

Haya mambo ya stoaways inabidi yatafutiwe dawa. Ndgu inabidi wabebe gharama za kuwarudisha ndugu zao au wakopeshwe na serikali, maana ni suala linaloongezeka hivi sasa.

Tumeshindwa kutafutia dawa matatizo madogo tuliyonayo hapa nyumbani..ndo tutayaweza ya Sudan? you must be kidding!
 
mkuu kwani UNHCR vipi hamuwezi kuwanganisha nao ili waweze kuwasaidia?


poleni sana ila wengi wa mabaharia wa khartoum ni walevi na waliopoteza malengo kuna jamaa yetu mmoja anaitwa OMar yeye kaoa na ana watoto huko tulimpelekea pesa akala na hajafanya lolote la kurudi nyumbani

baadae tukasikia kafungwa kwa kujiingiza kwenye madili ya kipuuzi
 
ungepata majina yao, na sehemu wanazotoka tanzania, isije ikawa wanataka msaada waendelee kuponda maisha hapo, je roughly wanahitaji kiasi gani cha pesa waweze kurudi? kama wapo mia moja sudan kharoum peke yake je nchi nzima inakuwaje? kama wakiweza kusafiri kwenda sudan kusini yaani juba au rumbek ambako kuna usalama zaidi inawezekana, manake wakivuka mpaka wakiingia uganda tayari wamepata msaada
 
Nafikiri sasa vita ya Sudan imefikia palipotakiwa maana darfur walikuwa wakilalamika kuwa serikali ya Sudan imekuwa ikipigana vita ktk eneo lao na walitaka angalau siku moja vita ifike Khartoum sasa naona kweli imefika.

Katika suala la watanzania, jamani watanzania wengi wanashida msione viongozi wetu wakifanya mchezo. Haya yako nchi nyingi hata south Africa kuna wabongo wengi wako ktk hali ambazo haziridhishi.

Ushauri wa Kubwa jinga unafaa sana utasaidia lakini je hata hao ubalozi wa Addiss Ababa watajuaje kuwa hao ni watanzania wakati hawana kitambulisho chochote?

Hii pia inatufundisha kuwa watanzania pasport ni haki yetu au vitambulisho vya uraia. Serikali inatakiwa itoe passport kwa kila mtanzania bila masharti yyoyote.

Poleni sana wakuu lakini pia fuata ushauri wa kuwasiriana na ubalozi wa Addiss Ababa kwa msaada zaidi.
 
mawasiliano ni magumu kidogo hapa,sababu simu zinakatikakatika. Hawa JEM walishambulia sehemu sensitive kama vyanzo vya umeme na kama jana network ilikuwa mbaya sana.
Curfew bado inaendelea na bado hatujaruhusiwa kutoka nje, inasemekana hao wapiganaji wmejificha ktk nyumba za raia.Inasemekana huenda curfew itaendelea mpaka kesho. maduka yote yamefungwa na magari hayatembei.
Kama hali itakuwa nzuri nitakuambieni ni kiasi gani cha nauli kinaweza kutosha mpaka Bongo kwa hao jamaa.
Ni kweli kuwa kuna jamaa huyo Omar alipata nauli na bado yupo hapa lakini kuna wengi wamesharudi bongo, na pamoja na hayo hawawengine nao wasaidiwe warudi. samaki mmoja akioza, basi sio wote wameoza. Kama kuna mtu angeweza kuwasiliana na Ubalozi wa Ethiopia au Misri ingekuwa swala zuri sana, sababu ntashindwa kupiga simu sababu vocha yangu itatosha kwa ajili ya emergency tu. Maduka yote yamefungwa
 
nnakumbuka miaka ya 2002 kuna Deputy Secretary wa WFP wa umoja wa mataifa alikuwa mtanzania jina lake nimelisahau na kuna wazee wengine walilivalia njuga suala hilo la kuwasaidia lkn ikashindikana sijui walimalizia vipi.

unajua wabongo wengi waliopo hapo hawataki kurudi nyumbani, ndoto zao wanataka kutoka zaidi au kukimbilia libya.

sasa wao wanataka uwapatie passport waendelee na mambo yao lkn mkijipanga kuwarejesha nyumbani wataanza kukupiga chenga.

hata hivyo ni miaka mingi tokea nilipopita hapo na kushuhudia visa vya ndugu zetu hao.

kuna mmoja alifariki alikuwa akikaa mayo na alioa msudan na alibahatika kupata watoto nnakumbuka bibi yao alitoka tanzania kuja kuwachukua watoto mambo yalifanyika na wazee waliwasaidia na passport ya sudan ilipatikana ili asafiri mama na watoto kama wanaenda dar kutembea ikifika ndio imetoka maana kwa njia nyengine watoto wasingepatikana tena

cha kusikitisha yule bibi hakuwa na nauli ya kutosha kusafiri na wote ikabidi arudi bongo ili azungumze na wanawe waweze kuchangia nauli aje cha kusikitisha aliporudi familia ilikataa kusaidia na yule bibi alishafariki sijui iko vipi hatma yao. maana mama yao mlevi alikuwa ajabu

sudan kuna mambo si madogo juu ya mabaharia wetu hao. na wewe uwe makini si mara wanaweza kukuingiza mjini


ila nnaungana huenda wakoambao watakuwa tayari kurudi nyumbani

na sasa ni rahisi ni kurudi kupitia juba halafu waingie uganda na kurudi kwao tanzania au hata wapitie kenya na yote inawezekana kwa njia ya bara bara ambayo si gharama kubwa na hata suala la passport sometimes mnaweza kucheza nalo
 
Sudan cuts ties with Chad after attack on Khartoum

Sudan severed relations with Chad on Sunday, accusing it of supporting fighters who assaulted the capital the night before and warned that a top Darfur rebel leader was hiding somewhere in the city.

Khartoum was still under curfew and reeling from the surprise assault late Saturday by Darfur rebels operating hundreds of miles from their bases in the far west of the country.

The government issued several statements claiming to have crushed the rebels and paraded images of captured and bloodied fighters on television.

"I would like to assure people that everything is now under control, the rebel forces have been totally destroyed," said Sudanese President Omar al-Bashir in a televised address Sunday, wearing military fatigues.

"These forces come from Chad who trained them ... we hold the Chadian regime fully responsible for what happened," he said. "We have no choice but to sever relations."

Al-Bashir said he reserved the right to retaliate against the "outlaw regime," raising the specter of a border war between the two countries who have long traded accusations over support for each others' rebels.

The Interior Ministry called on people in Khartoum and its twin city of Omdurman to remain inside while it searched for "infiltrators" -- rebels who had doffed their uniforms in the fighting to hide among the people.

"Security forces need more time to provide full protection for the people and for their property," said the ministry statement.

State television for the first time ever broadcast the picture of Khalil Ibrahim, leader of Darfur's Justice and Equality Movement, which carried out the assault, asking on citizens to call a special hotline if they saw him because he was hiding somewhere in Omdurman.

The JEM has become one of the most effective rebel movements in Darfur, where ethnic Africans took up arms against the government in 2003 to protest discrimination. In the last year it has expanded its operations into the neighboring province of Kordofan, even attacking oil installations.

Saturday night's assault, however, was the first time they had made it anywhere near the capital.

While the rebels declared the assault a success, the government was quick to describe it as a disaster for the rebels, displaying prisoners and captured vehicles on television.

"This attempt was a foolish act and those who carried it out did not take into account the negative consequences -- the attempt was based on lies and disinformation," said military spokesman Brig. Gen. Osman al-Agb
With just a few thousands members, JEM is outnumbered and far less equipped than Sudan's military, which believed to be more than 100,000-strong. Yet the group presents the most prominent military challenge to the Sudanese government in Darfur.

The assault puts greater pressure on the Sudanese government to deal with the festering situation in Darfur, where more than 200,000 people have died and 2.5 million have been chased from their homes. Many of the worst atrocities in the war have been blamed on the janjaweed militia of Arab nomads allied with the government.

Attempts to revive peace talks between Sudan and rebel groups have Other Top
failed to stem the violence. Rebel groups accuse the Khartoum regime of stonewalling the deployment of a United Nations peacekeeping force that would try to establish security before peace talks.

The instability on Sudan's western border has spilled over into neighboring Chad, with armed groups and refugees crossing the remote border on a regular basis and destabilizing both countries and straining relations.

"These forces are Chadian forces originally, they moved from there led by Khalil Ibrahim who is an agent of the Chadian regime. It is a Chadian attack," al-Bashir said Sunday morning.

For its part, Chad has accused Sudanese authorities of arming rebels who launched a failed assault February on the Chadian capital, N'Djamena. The rebels reached the gate of the presidential palace, but fled toward Sudan after Chad's army repelled them in fighting that left hundreds dead.

Though the two countries signed a peace agreement in March promising to prevent armed groups from operating along each other's shared borders, the accusations have continued unabated

Associated Press Writer Maamoun Youssef contribute to this report from Cairo

Source: www.mail.com
 
ungepata majina yao, na sehemu wanazotoka tanzania, isije ikawa wanataka msaada waendelee kuponda maisha hapo, je roughly wanahitaji kiasi gani cha pesa waweze kurudi? kama wapo mia moja sudan kharoum peke yake je nchi nzima inakuwaje? kama wakiweza kusafiri kwenda sudan kusini yaani juba au rumbek ambako kuna usalama zaidi inawezekana, manake wakivuka mpaka wakiingia uganda tayari wamepata msaada

Hapa Chenge he can help am sure badala ya kuficha pesa kule Jersey .Anyway asante kwa taarifa na kwa njia ya JF hata JK naamniwa ameshapata habari hii ila ameshidwa kusema lolote .Ubalozi wa Sudani Tanzania unaweza kuwa na jibu .Waambie serikali yao iwarudishe Tanzania nan bill iende serikalini kwetu simple .
 
Hali ni shwari sasa Khartoum japo kuna mapigano madogomadogo na tumeshaanza kuruhusiwa kutoka nje. magari yameanza kutoka nje, UN stuff hawajaruhusiwa kutoka nje.lakini si unajua sie wabongo hatujazoea hali kama hii,uoga bado. Unajua nimepata uzoefu mdogo, jinsi ya kujiandaa ktk hali kama hii. cha msingi hali kama hii lazima uwe na maji ya kutosha hasa ya kunywa, vyakula vya makopo, dry food, mishumaa na tochi(sababu hapa ulikatika umeme).
 
mbona Mnaenda Mbali?

Apigiwe Simu Huyo Membe Kisha Tuone How Fast Ataweza Kuwasaidia

Kama Mnashindwa Kumpata Balozi
 
atafutwe membe kisha yeye ndo atajua atafutwe nani wakupewa dhamana ya watu hao.
licha ya hao wasiokuwa na passport, kuna wanafunzi pia wengi tu, ambao machafuko yakiendelea ingepaswa kupewa pesa ya kurudia nyumbani.
 
hali haijawa mbaya kiasi cha kuwa na wasi wasi na wanafunzi si muda mrefu nimewasiliana na wanafunzi walioko khartoum wamenieleza wako shuwari kabisa.

la kuzungumza ni la hawa mabaharia jee wanahitaji msaada na kama kweli tuwasaidieje???

ila mie nnaona wengi wa mabaharia wako wako tu na kumrejesha bongo hujamsaidia maana yeye lengo lake ni kuuchinja
 
nimeangalia hapa nimemuona baharia mwenzao ES huenda akatupa data za kutosha kuhusu hali ya hawa ndugu zetu wa huko KRT
 
Lidoda Wakati Mwingine Unaweza Kuacha Namba Yako Ya Simu Kwa Chini Kama Tunataka Kuwasiliana Na Wewe Iwe Rahisi Zaidi
 
Kwa kuanza tu umesema mkeo anafanya kazi UN kwa nini mkeo asifanye mipango ya kuwasaidia hawa vijana kuwaingiza kambini kwa muda huu wakati mkijaribu kuwasiliana na balozi wetu..
Matatizo ya Sudan ni makubwa na hayataisha leo kwa sababu hao lebels wako backed up na nchi za Magharibi kiasi kwamba wanatafuta mbinu ya kuiangusha serikali ya Kartoum ili wapate kumiliki mafuta ya nchi hiyo...
Hii ndio taabu kubwa ya nchi zenye matatizo kuzialika nchi za magharibi kuja saidia wakati wa gharika.., hawa jamaa hiuingia na Askari wa kukodisha wakiongozwa na CIA kujaribu kuangusha serikali iliyopo hasa ikiwa inapingana na ubepari mamboleo. Ndio maana hata Burma wamekuwa wagumu kufungua mipaka yao pamoja na kuwa ktk matatizo makubwa sana..Wanajua fika siku watakapo fungua mipaka yao tu wamekwisha..Burma ni nchi moja tajiri sana lakini utwala wake ndio kama hivyo - kina Mugabe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom