Habari wana JF,
Tumeacha njia, tupo ukingoni.
Nchi ipo pabaya sana, Kwa viashiria vyote!
Hakuna mjadala, wala hakuna mwenye majibu.
Si UMOJA wetu, wala.......Si UZALENDO wetu......., vyote vimetikiswa nyang'anyang'a.
Kutoka hapa Mwitongo - Butiama, haya mambo ndio "KANSA" zinazolitafuna Taifa letu kwa sasa:
1. CCM hawawezi kutofautisha Chama na Serikali.
Hili limekita mizizi, na sasa limefika pabaya sana,
Wapo watakaobisha, lakini nawaambieni, Taifa linaangamizwa na huu ujinga.
Serikali ni Kwa ajili ya Taifa, lakini eleweni CCM sio kwa ajili ya Taifa!
Watu wanapenyeza mambo yao binafsi ndani ya CCM, halafu wanataka hayo hayo mambo yao ndio yapenyezwe ktk Taifa. Haiwezekani! Mnaua Taifa Kwa Tamaa zenu.
Mfano; ni mwana CCM gani anaweza kuikosoa serikali?! Hakuna..
Ukiikosoa serikali, au kauli ya Rais, unaonekana umeikosea CCM, unaitwa kwenye Kila kikao.
Watu hawaoni hili ni hatari. Inakuwaje maoni juu ya serikali ni kuikosea CCM.
Si mlisikia walisema eti Rais hakosei?! Na watu wakatulia tu.
Saivi mmekusanya wafanyabiashara wanajilipa walivyopoteza wakati wa Jiwe, Kwa gharama za wananchi?! Eti bei zimepanda hata katika soko la Dunia?! Justification ya Kijinga kabisa.
Mmewafanya Watanzania majuha!
Na yupo mfanyabiashara, ifikapo 2025 atafunga biashara/na kubadili jina, ataondoka Tanzania.
Sasa hivi anavuna Kwa kasi ya ajabu.
Watu wanaumiza sana Watanzania!
Wazee wote mmeufyata, mmetulia tu kisa nyie mnakula pensheni.
Serikalini mmejaa maigizo, huku wananchi wako hoi wanavuja damu!
Ninajisikia hasira sana ..
Nitaendelea kuandika, .......