Sauti Kubwa: Ndugai akuza deni la matibabu nje ya nchi adaiwa kulamba milioni 500 ndani ya miezi mitano

Status
Not open for further replies.
hii spika imekula hela mingi kwa matengenezo yake ila bado n mzigo. alafu haitaki wengine watibiwe
 
Nategemea wale waliokuwa wanaunga mkono hoja ya Mr. Jiwe kubana matumizi kwa safari za matibabu nje ya nchi kwa kuondoa urahisi uliokuwepo kwa maafisa wake na wabunge kupata kibali cha kwenda kutibiwa ughaibuni na hasa India watakemea vikali hili na si vinginevyo.
 
Eeeeeee kila mbuzi ale kutokana na urefu wa kamba yake, maana sisi ndio wajinga, mpaka pale mabichwa yetu yatakapotoka uzombi, mtani kukavuuu, watu wanapiga MABILIONI ya hela, ikifika uchguzi vaa dira la kijani au T-shirt ya kijani upumbazike
 
Stahili za spika ni tofauti Na mbunge.Mbunge akifa hata Jamii forum yaweza isitangaze.Spika Hadi CNN,BBC nk watakatisha matangazo kutangaza msiba usilinganishe Spika Na akina LISU,Bulaya,mbatia au Bilago ,Rwamlaza etc he is not their equal
labda kwa kumtandika na gongo kichwani mwanaccm mwenzake .
 
Stahili za spika ni tofauti Na mbunge.Mbunge akifa hata Jamii forum yaweza isitangaze.Spika Hadi CNN,BBC nk watakatisha matangazo kutangaza msiba usilinganishe Spika Na akina LISU,Bulaya,mbatia au Bilago ,Rwamlaza etc he is not their equal
Hivi si juzi tu 2016 serikali ilipiga marufuku kutibiwa nje ya nchi maradhi yanayoweza kutibiwa ndani ya nchi mkuu!? Au umehasahau jinsi mlivyokuwa mkipiga vigelegele na kusema jamaa anabana matumizi!???
 
Nchi ni yetu wote tugawane keki ya taifa letu sawa sio kwa ubaguzi. Kuna vitu vya dharula kama haliyo ipata TL uwezi linganisha na mgonjwa wa kisukari ambaye anakwenda hospital anajitambua tofauti na mtu aliye pigwa risasi 38 za moto zilizo ingia mwilini. Kama utaratibu huo wa rufaa ungefatwa nahisi leo yangekuwa ni mengine kwenye mambo ya dharula ni bora busara iwe inatumia.Sasa mgonjwa wa kisukari wa kukatwa mguu anatumia shilingi zote hizo hama kweli hii nchi wameiona ni yao.
 
Huyo aliyeandika huo uzi huenda akawa yule mzushi wa Kigoma. Anawajua wenye akili za kushikiwa watatoa mapovu
 
Pale unapofikiria kumuombea kifo mpinzani wako
Nakumbuka tu kina Mtikila, Komba,nk
 
Duh,kweli kuna watu wanakula mema ya nchi hii

Mh Spika aliwahi kusema; Wabunge, fuateni utaratibu tu. Mambo yoote yako nje nje. Utatibiwa popote lakini ufuate utaratibu mliouweka wenyewe.
Huwezi kwenda India ukaombe malipo ukiwa India. Si haki. Huwezi kwenda Ubeleji ukaombe malipo ukiwa Amsterdam. Si kweli
 


JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, na Rais John Magufuli wamenyoshewa kidole, wakihusishwa na ongezeko kubwa la deni la matibabu nje ya nchi.

Deni hilo limeongezeka kwa kasi isiyo ya kawaida katika kipindi ambacho watumishi wa serikali wanaotibiwa nje ya nchi wanadhibitiwa na rais, na Ndugai mwenyewe amekuwa “mgonjwa mkuu” aliyetibiwa nje katika kipindi hicho.

Mwaka jana, serikali ililiambia bunge kuwa nchi ilikuwa inadaiwa Sh 28.60 bilioni kwa ajili ya matibabu ya viongozi nje ya nchi, hasa India. Ndani ya miezi sita tu, deni hilo limekua hadi Sh. 45.73 bilioni. Hili ni ongezeko la Sh.17.13 bilioni.

Ongezeko la asilimia 60.71 ya deni ndani ya kipindi kifupi, wakati idadi ya viongozi wanaotibiwa nje imepungua, ni doa kwa dhamira ya Rais John Magufuli ya kupiga vita ufisadi na kudhibiti matibabu ya nje.

Kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG), ongezeko hili ni la kati ya tarehe 30 Juni 2017 na tarehe 31 Desemba 2017.

Kwa kuwa limeongezeka katika kipindi ambacho wagonjwa wanaokwenda nje lazima waruhusiwe na rais, na “mgonjwa mkuu” aliyetibiwa nje ni Ndugai, ongezeko la deni la matibabu linahusu wote wawili – rais na spika.

Taarifa zinaonyesha kuwa sehemu kubwa ya deni hili imesababishwa na Job Ndugai. Kwa mujibu wa takwimu za CAG, Ndugai amekaa India kwa takriban miezi mitano, akiwa na wasaidizi wake na familia yake.

Posho ya mbunge anapokuwa nje ya nchi kwa siku moja ni dola 500; mtumishi wa bunge ni dola 450; mwenzi wa ndoa ni dola 300.

Kwa uchambuzi wa ripoti ya CAG, Ndugai amekaa India kwa miezi mitano, ambayo ni siku 150. Kama kwa siku moja alilipwa dola 500, ina maana kuwa kwa miezi mitano alilipwa dola 75,000. Kwa shilingi za Kitanzania, kwa viwango vya ubadilishaji fedha vya Sh. 2,170 kwa dola moja, Ndugai alitumia shilingi 162,750,000 kama posho ya kuishi India.

Akiwa India alikuwa na wasaidizi wawili – maana alihamishia ofisi yake huko huko hotelini. Kwa gharama ya dola 450 kwa siku, mara mbili, watumishi hawa walilipwa dola 900 kwa siku. Kwa siku 150 walizokaa India, maana yake walilipwa dola 135,000, sawa na Sh. 292,950,000.

Chanzo chetu kutoka Bungeni kimeliambia SAUTI KUBWA: “Kwa ujumla, matibabu ya Ndugai kwa miezi mitano yametumia posho za shilingi 455,700,000, na hapo bado gharama za hospitali huko India, na tiketi za ndege kwa watu wote hao, na bado gharama alizokuwa anatumia mkewe.”

Takwimu hizi ni kwa mujibu wa ukaguzi wa CAG katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika hospitali za India.

Wakati ofisi ya spika inatoa gharama zote hizi kwa ajili ya matibabu ya Ndugai, kuna orodha ndefu ya wabunge ambao wamenyimwa huduma hiyo ambayo ni haki yao kisheria.

SAUTI KUBWA limeelezwa kuwa baadhi ya wabunge walionyimwa huduma hiyo, ni wapinzani, na wamekuwa wakitibiwa ndani na nje ya nchi kwa gharama zao binafsi, mikopo au michango ya ndugu na jamaa zao.

Chanzo kimoja kutoka bungeni kimesema: “Kwa kuanzia na Mheshimiwa Tundu Lissu, ambaye maisha yake yaliokolewa na michango ya watanzania, yupo pia Mheshimiwa Zubeda Sakuru ambaye hadi sasa anajigharamia matibabu, na ofisi ya spika imegoma kutoa chochote. Mheshimiwa James Mbatia alipovunjika mkono, alitibiwa India kwa jitihada binafsi; ofisi ya bunge ikakaa kimya.

“Mheshimiwa Ester Bulaya amegharamia matibabu yake mwenyewe, na Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza amejilipia gharama za kwenda Muhimbili, Nairobi na India, na hadi sasa ofisi ya spika inapiga danadana. Majuzi tu, tulimpoteza Mheshimiwa Kasuku Bilago, ambaye hadi anaaga dunia kwa kukosa matibabu ya uhakika, alikuwa anahangaika kujilipia, huku ofisi ya spika ikiwa imegoma kugharamia matibabu yake.

“Hii yote ni kujaribu kuonesha ni jinsi gani gharama za matibabu zinavyotolewa kwa upendeleo wakati wabunge wote kwa mujibu wa sheria wana haki sawa ya kupatiwa matibabu.”

Kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji wa Bunge ya mwaka 2008, katika kifungu cha 24(1), “matibabu ya mbunge yatagharamiwa na Bunge ndani na nje ya Tanzania.”

Bunge limekuwa limekuwa linatumia kifungu hiki kuidhinisha malipo ya matibabu ya Ndugai na baadhi ya wabunge, lakini limekataa kutumia kifungu hicho hicho kutibu wabunge wengine, hasa wanaotokana na vyama vya upinzani

Wakati mwingine huwa natamani Malaika washuke na moto!
 
Kwenda kutibiwa nje zipo taratibu zinatakiwa kufuatwa, huwezi kurupuka ukaenda nje ya nchi ww mwenyewe halafu utegemee serikali ilipie. Moja ya kigezo cha kugharamiwa ni lazima uende kutibiwa nje kwa rufaa ya hospitali ya Taifa ya muhimbili. Wabunge wote hao wamefuata utaratibu huo? Ifahamike kuwa sheria haisomwi peke yake bila kanuni na miongozo.

Binafsi siungi mkono ubaguzi au ukandamizaji wa kundi lolote lile. Haki za kila mbunge na kila mtanzania na kila mtumishi lazima zizingatiwe na sheria kanuni na miongozo lazima ifuatwe.
lini ulisikia mbilikimo ndugai amepelekwa india akitokea bugando au muhimbili?
 
lini ulisikia mbilikimo ndugai amepelekwa india akitokea bugando au muhimbili?
Mimi sifahamu lkn inawezekana anayo rufaa ya muhimbili. Pia ni vyema tufahamu kuwa wakuu wa mihimili ya dola yaani spika, rais na Jaji mkuu wanazo stahili ambazo hazifanani na viongozi wengine. Usifikiri utaratibu anaotakiwa kufuata rais ni sawa na wa spika na wala usifikiri utaratibu anaotakiwa kufuata spika ni sawa na wa mbunge. Hao wanazo privelege ambazo mtu mwingine hana
 
Kwani hesabu za mwaka 2017/2018 zimeshakaguliwa na CAG? Au kuna special audit imefanyika kwenye deni la matibabu ya nje?

Maana June 2017 to December 2017 iko kwenye mwaka wa fedha wa 2017/2018 ambayo haijaisha na taarifa yake nina hakika tutaipata mwakani mwaka 2019 mwezi wa nne au wa tano.
Mkuu una hoja ya mcng sana,lkn kwa nature ya hili jukwaa kwa saizi ni ngum kujibiwa!!Ebu achana na hii tuendelee kutoa mapovu tu
 
Ingekua vema kama wanachi wa hali ya chini wakumbukwe kwenye hayo matibabu sio viongozi wa serikali pekee wenye hali nzuri za kimaisha hii nchi inatia aibu sana, kuna mama yupo wilaya ya serengeti jicho limeharibika kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu ughaibuni.

Ndugai wamwache apumzika jana nimeona akiosha magari kushika kitambaa shida,kuhusu Lissu apambane kivyake Mchuma janga ula na wakwao.
 
Shida matumizi ya Ndungai au shida kwa sababu wapinzani hawakulipiwa hizo gharama kwahio na wao wangelipiwa ingekua sawa tu???
 
Status
Not open for further replies.
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom