Sauti hizi hospitali ya taifa muhimbili haziwezi tafutiwa ufumbuzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sauti hizi hospitali ya taifa muhimbili haziwezi tafutiwa ufumbuzi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mnyamahodzo, Sep 24, 2009.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kama ulikwisha wahi kwenda katika Hospitali yetu, kubwa kuliko zote hapa nchini Tanzania,yaani Hospitali ya Taifa Muhimbili muda wa saa saba mchana au saa kumi kasoro jioni utakuwa umekutana na hili nalolitaka kulisema.

  Ndiyo! Ziko sabababu nyingi zinzoweza mfanya mtu akaenda Muhimbili, yawezekana ugonjwa au unasindikiza mgonjwa, kuchukuliwa kipimo,kumwona mgonjwa ama kuweka au kuchukua maiti.

  Karibu na chumba cha maiti pana nyumba mbili kubwa za ibada, yaani msikiti na kanisa. sasa ukiwepo Muhimbili masaa hayo niliyoyataja wakati ibada inaanza msikitini, inapigwa adhana. Sauti yake yakuzwa na kipaza sauti. Inatupwa mbali sana.

  Sasa tatizo hapa ni hili, nikijua ile ni hospitali yenye wagonjwa wanaolazwa na wasiolazwa na nikijua kuwa hata magari hayaruhusiwi kupiga honi ndani ya eneo la hospitali;iweje sauti hizi katika kipaza sauti ziwe zinaendelea kuwa kero kwa wagonjwa hasa wa zile wodi za wazazi na watoto(maana zipo umbali wa chini ya mita 100 toka msikitini)?

  Hivi adhana ikipigwa bila ya kutumia kipaza sauti, ibada inakuwa batli? Kama hilo ni kweli. Je! Maeneo ambako hakuna umeme wala kipaza sauti ibada zao ni batili? Je! Ibada walizofanya wakina Mtume Mohamad (S.A.W) bila kutumia kipaza sauti zilikuwa batili?

  Kama ibada inaendelea kuwa halali hata kama adhana itapigwa bila kipaza sauti,kwanini basi tuendeleee kuwasumbua wagonjwa? Hivi inamaana hata wanaokwenda kuswali hapo miaka yote hiyo, wameshindwa kuliona au wanaifurahia hiyo hali?

  Kama hujawahi kuwa na mgonjwa Muhimbili katika masaa hayo huwezi jua ni kwa kiasi gani sauti hizo ni karaha;hili linawahusu watu wote bila kujali dini wala rangi yake.

  Wana-jamvi hebu tulijadili na watu wa Muhimbili wachukue maoni yetu.
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mnh, huenda wanawakumbushia wagonjwa wazidi kuwa karibu na muumba wao, si umesema ni karibu na chumba cha maiti?

  Kwani lile kanisa pale nao hawagongi kengele?
   
 3. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Sauti inayotoka ktk nyumba yoyote ya ibada si KELELE!
   
 4. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu angalia usije pondwa mawe.
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,473
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280
  hii kali adhana leo hii inakuwa kelele, sasa na sie wa uswahilini tunaoamshwa usiku bila ridhaa yetu na hizo adhana tusemeje au tuandamane
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,026
  Trophy Points: 280
  Mkuu wewe si uko home. Hapa inasemewa wagonjwa ambao hawapo mbali na maiti zilizopo mochwari. Inawezekana sauti zinazotoka kanisani/msikitini zisiwe kelele, kwa waumini. Lakini kuna wagonjwa ambao si wakristo au waislam, kwao hizo ni kelele. Kwangu mimi kwa mfano, adhana ni kelele ila kengele si kelele. Ukweli ni kuwa, vyote viwili (kengele na adhana) ni kelele kwa wagonjwa. Vipigwe marufuku hospitalini.
   
 7. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu, ukweli ni kuwa wale wakiristu wamekuwa wastaarabu,hapana kengele wala alama ya kengele(maana waweza sema zamani ilikuwapo).

  Wasio wakiristu wala waislamu sijui wanafanyia wapi ibada zao. Kwanza, sijawahi liona jengo lao lakini pili, kama lipo inamaanisha wanafanya bila ya kutoa sauti zinazoweza wasumbua wagonjwa.
   
 8. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu, huu utakuwa wendawazimu unaozidi kichaa kinachotokana na dini. Yaani, kusema jambo jema na kufanya marejeo ya ilivyokuwa huko nyuma lakini nikifikiria mustakabali wa afya za watu walioletwa eneo maalumu kwa matibabu ndiyo waje kunipiga mawe kama kafiri(mpinga maneno ya Mwenyezi Mungu).

  Jamani, tusiseme kwasababu tu wazima tunakula, tunakunywa na kupata usingizi mzuri. Hebu jaribuni kujiweka katika nafasi ya ugonjwa, nakwambia si redio tu utakayoichukia bali hata kengele.
   
 9. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kusema ukweli kupiga kelele ya aina yoyote ile kwenye hospital yoyote ile duniani huwa ahiruhusiwi, wagonjwa wanatakiwa kukaa sehemu yenye utulivu ili waweze kupumzika sasa ukipiga kelele tena inakuwa tabu kidogo wengine wanamatatizo yasiyohitaji kelele za aina yoyote hapo tunawasaidia aje hawa wagonjwa??

  Ningependa kuwashauri hawa ndugu zetu kwenye huo msikiti mdogo waendeshe ibada zao bila ya kupiga hiyo adhana mathalani inajulikana pale ni hospital hivyo kutoweka spika kwa ajili ya adhana haitoleta maana mbaya, wawafikiria wagonjwa kwanza hata mwenyezi mungu ataona ni haki pia kutoweka hizo spika
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Sep 27, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Aslm'Alykm...!
  Mnyamahodzo, swala lako ni zuri sana ila wakati mwingine sisi raiya huwa hatuangalii haki zetu za msingi na huwa tunapenda kulalamika kabla hatujachuwa hatua zinazopaswa kwanza.

  Wewe ukiwa ni raiya mwenye mgonjwa au Mwenye kuelewa haki wagonjwa kule Muhimbili au Hospitali yoyote ile, na wakati wa Swala au kwa sababu yoyote ile utokea sauti yenye kusababisha kero au usumbufu kwa wagonjwa, wewe ulipaswa kuwaona au kuzungumza kwa uzuri uongozi wa huo Msikiti na kuwafahamisha hiyo kero wanayo ipata wagonjwa wanao fikiwa na hiyo Sauti ya Adhana.

  Kulalamika tu kwenye tovuti utakuwa ujawasaidia bado ndugu zetu wanao pata usumbuvu na hiyo Sauti ya Adhana.

  Waislam wanaweza kuadhini Bila kipaza sauti na Swala ika-sihi.

  Basi fanya hima kuwasiliana na uongozi wa msikiti wa hapo Muhimbili, ni matumaini yangu kuwa watakusikiliza na kufanyia kazi malalamiko yako Insha'Allah.

  X-Paster.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, you have nailed it!!!! umeeleza haswa jinsi ya jama'a inavyotakiwa kuwa. sijui nikushukurje.... nikiwa pale muhimbili nilikuwa na the same questions, lakini nikajua kwamba hata viongozi wa pale [au na penginepo kama hapo, wale wa LAKAIRO MNANISIKIA!], hawajui kinachotakiwa

  nakupa tano mkuu
   
  Last edited: Sep 28, 2009
 12. M

  Mpenzi wa Islam JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 2,295
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Mnyamahodzo shukran kwa kutuletea habari yenye kuwakera wagonjwa wa Hospitali ya Muhimbili.

  Mimi kama Mwislamu nachangia maoni kama ifuatayo.

  Kama Kweli sauti ya adhana inawakera wagonjwa wa pande yeyote ya Muhimbili basi lazima Viongozi wa hiyo Msikiti wa arifiwe kwa njia ya ustaarabu ili wafanye juhudi ya kuondoa kero ya kipaza sauti kwa wagonjwa hao wa karibu na mbali.

  Napenda ifahamike sio lazima adhana isemwe kupitia kipaza sauti wala sio moja wapo ya nguzo za Ibada kuadhini kupitia kipaza sauti.Kwahiyo adhana ikiadhiniwa bila kipaza sauti Ibada haitakuwa batili wala kupata dosari yeyote.

  Adhana inaweza kuadhiniwa bila kipaza sauti kama kweli inawakera wagonjwa au

  kipaza sauti itumiwe kwa sauti ya chini isiyo weza kukera wagonjwa wa karibu na mbali ya Muhimbili.

  Nataraji mpaka hapa maoni yangu niliyo changia italeta manufaa japo kidogo.

  Wako katika Utu
  Mpenzi wa Islam
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, umenipa faraja kubwa kwa uelewa na wisdom yako!!!! i wish wengi tungekuwa kama wewe
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,739
  Likes Received: 82,676
  Trophy Points: 280
  Wakuu Mpenzi wa Islam, X-PASTER na MTM mmenifurahisha sana kwa kulijadili swala hili kwa ustaarabu, hekima na uungwana wa hali ya juu. Muendelee hivyo hivyo katika mijadala mbali mbali hapa ukumbini. Mwenyezi Mungu awajalie wote katika kila mlitakalo~AMIN.
   
 15. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ndugu, ushauri wako ni mzuri ninauafiki. Lakini suala la kuweka mawazo/maoni ambayo ni KERO YANGU katika JF haimaanishi kuwa ni kulalamika hapa. Ukiwauliza web-moderators hivi imliiweka forum ya kero ilikupokea malalamiko ya watu tu, jibu, si kweli. Ndiyo sababu katika KERO YANGU wanapofafanua wanataja kero/malalamiko na dukuduku. Haimaanisha kila kero na dukuduku ni malalamiko.

  Pamoja na hili hilo ninaamini wapo viongozi na wadau wa Muhimbili wanaosoma hapa, hivyo wao watakua miongoni mwa watu watakaolifikisha hili kama marudio kwa viongozi wenzao wa juu wanapojadili masuala ya maendeleo ya Hospitali na mahusiano na jamii ya watanzania.
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Sep 29, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nashukuru mtu wangu kwa maelezo yako, ila mimi binafsi nilimaanisha kuwa Sisi wananchi tunapaswa kuwa majasiri zaidi na kuyashughurikia mambo yetu ya kijamii kwanza kabla ya kulalamika, ila nashukuru tena kwa maelezo yako, wakati mwingine inawezekaa sifahamu haswa nafasi yako kiasi ya kwamba inaweza kuwa si rahisi kwako kuwasiliana na uongozi husika, ili kutatua ilo jambo ulilo liweka hapa.

  Nami ni matumaini yangu kuwa wale wahusika wanweza kulitatua hilo tatizo.

  Kila la kheri mkuu, tupo pamoja.
   
 17. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #17
  Sep 29, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Dua yako iwe makbur, kwa sote Insha'Allah

  Jazakallah Khair

  'May Allah grant you goodness'.
   
 18. w

  wasp JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Why not borrow a leaf from Rwanda that these disturbing noises are stopped forthwith.
   
Loading...