SAUT wameanza kwa mfano huu bora naomba sasa UDSM, Mzumbe, CBE na hasa hasa IFM nanyi Muwaige

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,401
2,631
Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT), Mwanza kimewafuta kazi wahadhiri watatu kwa makosa ya kujihusisha na rushwa ya ngono na wanafunzi kwa nia ya kuwapa upendeleo kwenye mitihani. Chuo hicho kimesema vitendo hivyo havikubaliki na kuwataka wanafunzi kuendelea kuvifichua.

Chanzo: Swahilitimes

Kuna Vyuo kama viwili hapa hapa Jijini Dar es Salaam kama Uongozi Wao ukiiga kilichofanywa na SAUT hakuna Mhadhiri wa Kiume atakayebakia.
 
Hio inshu kuimaliza ni kazi sana labda waziri wa elimu aji commit haswa kupambana na hio mishe kwa kupandikiza wadada fake ili wawalipue hao lecturers
 
Kesi kibao za unyanyasi wa kingono wanafunzi wenyewe huwa wanaogopa kutoa ushahidi. Nadhani vyuo viunde kamati maalumu za kusikiliza hizo kero za unyanyasi wa kingono kwa wanafunzi.

Then mwanafunzi achukue ushahidi wa huo unyanyasaji, then anaukabidhi kwa kamati then yeye anakuwa nyuma then kamati inakuwa front kushughulika na mhusika na kumfuta kazi
 
Kesi kibao za unyanyasi wa kingono wanafunzi wenyewe huwa wanaogopa kutoa ushahidi. Nadhani vyuo viunde kamati maalumu za kusikiliza hizo kero za unyanyasi wa kingono kwa wanafunzi...

Ndugu mbona katika haya Maelezo yako kuna then nyingi sana? Vipi ulipokuwa Chuo ulikuwa huhudhurii Somo la Communication Skills?
 
  • Thanks
Reactions: p2k
Kama lectures wataendelea kuwa na 100% mandate kwa ufaulu wa mwanafunzi hata shetani akae pembeni rushwa ya ngono haiwezi kuisha.

Tudada chuoni tumekuja kuuza sura na kutamba tupo chuo halafu hatusomi......tukifeli lectures akitugusia tu ngono tufaulu wala hatunaga longolongo kuvua chupi.
 
Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT), Mwanza kimewafuta kazi wahadhiri watatu kwa makosa ya kujihusisha na rushwa ya ngono na wanafunzi kwa nia ya kuwapa upendeleo kwenye mitihani. Chuo hicho kimesema vitendo hivyo havikubaliki na kuwataka wanafunzi kuendelea kuvifichua.

Chanzo: Swahilitimes

Kuna Vyuo kama viwili hapa hapa Jijini Dar es Salaam kama Uongozi Wao ukiiga kilichofanywa na SAUT hakuna Mhadhiri wa Kiume atakayebakia.
Kongole SAUT. Tatizo kubwa ni pale wakubwa wenyewe wanapo jihusisha na ujinga huu au wanapotaka kuwatetea watu wao.
Kama lectures wataendelea kuwa na 100% mandate kwa ufaulu wa mwanafunzi hata shetani akae pembeni rushwa ya ngono haiwezi kuisha.

Tudada chuoni tumekuja kuuza sura na kutamba tupo chuo halafu hatusomi......tukifeli lectures akitugusia tu ngono tufaulu wala hatunaga longolongo kuvua chupi.
Kila inapowezekana vyuo vingetafuta mbinu za kutompa mhadhiri nguvu kwa kiasi hicho. Je inawezekana kwa somo kuwa zaidi ya mhadhiri mmoja? Je inawezekana kwenye research process kuwe na supervisors 2 au zaidi.
Wanafunzi wapewe mikakati ya kukihami na vyuo-hii itasaidia.
Lakini pia kuna tatizo la kujilengesha kwa mabinti-hadi darasa zima linafikia hatua ya kumwita mhadhiri SHEMEJI.
 
Mmmmh hili suala naomba lishughulikiwe kweli, inaumiza sana ndoto za wanafunzi .
 
Back
Top Bottom