Madudu yanayofanyika katika chuo hiki yamekithiri katika mwaka wa masomo 2017/018. Baada ya kubadilisha system ya kuhifadhia matokeo awali SIMS na kuleta OSIM imeleta vilio kwa wanafunzi wengi huku wengine wakishindwa kugraduate na wengine kushindwa kupata fedha zao za kujikimu kutokana na matokeo kutoonekana.
Kuna ambao hadi sasa wanaingia madarasani kusoma lakini matokeo yao mwaka wa masomo uliopita hawajayaona. Wanapofuatilia hakuna majibu ya kuridhisha juu ya utatuzi wa tatizo hili na watumishi wa department ya IT wamekuwa kama miungu watu hakuna msaada wowote wanaoweza kuutoa.
Continuous ambao ni wananufaika wa mkopo wamekaa tokea chuo kifunguliwe bila kupewa hadi sasa semister inapoelekea kuisha ndo wanapewa tena kwa mafungu sababu ikiwa hii system kutoonyesha matokeo ya watu watu yapelekwe board ya mikopo.
Na pasipo kujali kuwa sababu za watu hawa kucheleweshewa pesa zao ni wao, wanaweka penalty tena kwa anayechelewa kulipa Ada. Jamani kuna watu wanatoka familia duni wanategemea Boom ndo walipe Ada. Unamcheleweshea pesa yake kwa uzembe halafu unampiga penalty ya laki moja kwa kuchelewa kulipa ada! Hii sio sawa hata kidogo, watoto wa masikni wanasoma kwa mateso sana hapa SAUT.
Kuna waliofanya supplimentary na ajabu matokeo yao yakarudi kama mwanzo yalivyokuwa ina maana hakuna mabadiliko yoyote hata baadhi wameshindwa kuhitimu sababu ya hii system. Ukimfuata mwalimu wa somo anakuonyesha hadi booklet kuwa ulifaulu lakini system inaonyesha hujafaulu na mwalimu haruhusiwi kuingilia kwa lolote atakwambia kuna examinationa officers wanafanya kazi hiyo.
Kuna watu wanatazamia kufanya mtihani wa semester ya kwanza mwaka huu wa masomo wakiwa hawajui matokeo ya semester iliyopita. Hapo yakitolewa hayo matokeo ukiwa umefeli unajikuta una mizigo kibao huku wenzio walikwishafanya supplimentary zake kitambo.
Kuna ambaye jina lake lilitoka kwenye kitabu cha graduates na akafanya hadi sherehe ajabu kuja kufuata cheti anaambiwa ana supplimentary ya mwaka wa pili. Inawezekana vipi mtu asome hadi mwaka wa tatu asijue kuwa ana kimeo mwaka wa pili?
Inaumiza sana na kama Serikali italifumbia hili macho bado kuna tatizo kubwa sana maana hata waliopo mwaka wa tatu wanaenda kufanya mitihani ya semester ya kwanza ikiwa matokeo yao ya mwaka wa pili hawajayaona na huku kukiwa na sintofahamu kuna uwezekano mwisho wake wataambiwa warudie mitihani hiyo tena kwa kulipia kila mtihani elfu 75000.
Kwa leo naishia hapa.